Askofu Bagonza: Tuliyajua, Hatukuyajua lakini hilo zaidi ya tatizo

Bashite, Musiba, Kapilimba, wasiojulikana inatakiwa wajibu waliyowafanyia watz ndugu zetu wako wapi?
Hakuna haja ya kuwafumbia macho hawana kinga tena mungu wao amekwenda hatorudi tena
 
Mh.RAIS Nakupongeza sana kwa hatua uliyochukua Dhidi ya MTEULE Wako SABAYA ya Kumsimamisha Kazi ili kupisha Uchunguzi dhidi ya Malalamiko ya Wanyonge Masikini wa Nchi hii.Pia nampongeza Mkuu wa TAKUKURU Taifa na DPP kwa kuendelea na Uchunguzi wao na hatimae MUNGU MTU SABAYA kufikishwa MAHAKAMANI.
Mh.RAIS usihishie kwa SABAYA kuwa Wateule wako bado wapo na Wengine wapo Nje ya Serikali yako Wanatajwa Kuhusika Na Matukio ya Aina hiyo hiyo ya SABAYA.Tunakuomba Kila Alitajwa tajwa ACHUNGUZWE Kwani Watu hawa WAMEWATESA na KUWAUMIZA SANA WANANCHI.Baadhi ya Watu hao ni Pamoja na Paul Makonda
Msimpangie mama wa kumsweka ndani, Sabaya ametolewa mfano na ndio maana amesema waliofanya maovu kama ya Sabaya wajitahidi waombe msamaha kabla hajadeal nao.

Sabaya kimemponza kiburi na kudharau wanawake. Ule muda aliotumia kujisafisha kwenye media angeutumia ku-make peace na mkulu haya yote may be yasingemkuta.

Atakula jeusri yake, sasa na bashite aendelee kwenda kusalimia kaburi alidhani aliyekuwa anawalinda atafufuka instead ya kutumia muda hii kuhakikisha anaweka mambo sana na mama pamoja na watu aliowadhulumu Mali zao akiwemo mmiliki wa NAS Hauliers na akina manji pamoja na Ridhiwani pamoja na babake na mzee warioba.

Kazi wanayo.
 
Wanachadema na kutaka wale waliowakalia kooni waondoke ,wamesahau kuwa serikali iliyopo ni ya CCM na wateule wake ni watekelezaji tu wa ilani ya CCM, vinginevyo wataangaliwa kama una ushahudu wa hao unaosema waliwaua.
Serikali haipo ili iwakalie watu kooni wala ilani ya CCM haijaagiza hivyo. Wacha waovu washughulikiwe, ndilo jukumu na wajibu wa serikali.
 
Ule wakati wa malipo kwa wale viongozi wa serikali waliokuwa juu ya sheria kipindi cha nyuma sasa dhahiri umefika.

Waliokuwa juu ya sheria si Sabaya peke yake bali ni wengi ila inabidi washughulikiwe mmoja baada ya mwingine kadri taarifa zinapopatikana na heshima ya awamu ya tano itaridhiwa tu baada ya kundi hili ovu kutengwa.

Walikuwepo wakuu wa mikoa na wilaya ambao walitumia nafasi zao za kazi za uongozi wa umma vibaya. Hawa walijipendekeza kwa hayati Rais Magufuli huku wakifanya mambo maovu.

Waliwanyima Watanzania wengine haki zao za kibinadamu na kujifanya wao ni raia wa hali ya juu (first class citizens).

Waliwaweka Watanzania wenzao korokoroni bila uhalali wowote na wakati mwingine walivuruga biashara za Watanzania wanaohangaika huku wakichukua mlungula kutoka kwa wafanyabiashara wenzao wakware.

Kama unayo taarifa au kumbukumbu yoyote ya viongozi waovu waliotenda vitendo hivyo tupia hapo chini ya Makonda mengine yamekwishasemwa kwenye mikeka huku JF na mengine yatajitokeza humu humu sasa tunaanza na mfalme mmoja aliyekuwa mkoa wa Manyara.

Mkoa wa Manyara ni moja ya mikoa kitovu cha rasilimali za madini pamoja na wanyamapori ya madini yamekwishasemwa sana hapa tupo kwenye rasiliamali ya wanyamapori.

Aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti ambaye kwa sasa hivi ni mmoja wa mabilionea vijana yeye alitumia nafasi yake kujitajirisha kwa kufunga jicho moja na kushirikiana na majangili.

Alishirikiana na majangili ya kiarabu kuvuruga maliasili hiyo ni baada ya kuondoka tu na kuja mkuu wa mkoa aliyehamishwa JOSEPH MKIRIKITI ndio tukaona hatua madhubuti ya kuwakabili majangili zimechukuliwa.

Majangili haya yamekuwa yakitumia ukwasi wa fedha kutoa hongo kwa maafisa wa serikali wa ngazi za juu na chini.

Hivi karibuni jangili mmoja aliyekubuhu aitwaye GERALD alitiwa hatiani na kupewa kifungo cha miaka 30 jela na bado kesi nyingine zinamkabili mahakamani.

Kipindi cha nyuma jangili huyu angepangua kesi zote kwa kutumia ukwasi wa waarabu ambao wanamtumia kwenye shughuli zao.

Hatahivyo, kesi aliyepigwa miaka 30 ikipelelezwa kiukweli hao wakware waarabu watabainika hivyo Mh Rais Samia Suluhu Hassan jihadhari na makundi ya waarabu wanaokuja serikalini kujidai wanataka kuleta mitaji kama watu wema na fanya uchunguzi wako mwenyewe utagundua nyuma ya pazia hakuna kilimo wala utalii ni ujangili tu na ushahidi upo wazi.

Huyu Mnyeti anadaiwa kujiingiza kwenye migogoro ya makampuni ya uwindaji kesi ziko mahakamani na alitumia madaraka yake vibaya kuzuia wenye biashara kufanya biashara zao bila kufuata taratibu za kiutawala.

Aliagiza wafanyabiashara kutiwa rumande bila uhalali wowote na haiwezekani haya yote yafanyike bila maslahi binafsi ya upande wake.

Hakuna ajabu yoyote ya yeye kuwa bilionea kijana kwani alipokuwa akifanya vitendo vya kukiuka sheria bila shaka alipata faida ushahidi wa vitendo vya ujangili vilivyokuwa vikifanyika wakati wa utawala wake na upo bayana waliokuwa wakifanya vitendo hivi walipata nguvu ya kujitapa kwamba wako na mkubwa sasa tunataka kujua ubilionea ameutoa wapi?

Tatizo moja tulilonalo ni kwamba vyombo mbalimbali vya umma vilikuwa vikiwalinda aina hii kina Ole Sabaya, Mnyeti na kadhalika walijieleza kama watoto wa hayati Magufuli na walikuwa untouchables.

Kwenye suala la Sabaya tulisubiri hadi mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipomsimakisha kazi na kuagiza uchunguzi ufanyike.

Ni wakati sasa vyombo vya dola vinavyohusika na haki za wananchi na utawala bora kuwashughulikia ipasavyo wote waliofanya maovu kipindi kilichopita na tunampomgeza Rais Samia kuchukua maaamuzi sahihi kuhusu Ole Sabaya.

Tunamshauri Rais Samia awamulike wote ambao kwa njia moja ama nyingine wanawalinda wale viongozi waliofanya maovu kipindi cha nyuma bila shaka na wao kwenye utawala unaokuja wa kufuata haki watapewa nafasi ya kujitetea.

Kama unayo taarifa yoyote ya wakware tupia hapa chini ni baada ya ukweli na uwazi tu ndio tutajenga taifa lenye kuheshimiana kati ya viongozi na wananchi.

Mheshimiwa Rais amechukua hatua nzuri waliokuwa wanapeleka mabega juu siku za nyuma na kujipatia utajiri washughulikiwe bila huruma yoyote maana nia zao zilikuwa kuwafanya watanzania wenzao maskini wakati wao wakijitajirisha kudadadeki.

Mwisho.

D1358E08-6DB8-4059-B141-3757A368841D.jpeg


9989678D-FA25-4845-B3BD-A615E031F2EF.jpeg
 
Kuna huyu DC wa Sengerema anaitwa Emanuel kipole ki ukweli ameumiza watu sana. Wavuvi wamelia sana alitumia madaraka yake vibaya kuwafilisi wafanyabiashara wa samaki. Ikiundwa tume yataelezwa mengi.
Huyo dogo muhuni Sana tunamfatilia vzr Sana

Huyu alimzuia jamaa mmoja asigombee nafasi ya uongoz kwenye chama Chao cha wafanyakaz

Taaarifa zake zipo sehem salama
Ni suala la muda tuu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mama kazi anayo... Uporaji kwa watendaji wa serikali upo kila sehemu... Mfano mdogo ni mapolisi especially wale wanaozunguka na magari kwa majina ya Task force.... Yaani kazi ipo
 
Msimpangie mama wa kumsweka ndani, Sabaya ametolewa mfano na ndio maana amesema waliofanya maovu kama ya Sabaya wajitahidi waombe msamaha kabla hajadeal nao.

Sabaya kimemponza kiburi na kudharau wanawake. Ule muda aliotumia kujisafisha kwenye media angeutumia ku-make peace na mkulu haya yote may be yasingemkuta.

Atakula jeusri yake, sasa na bashite aendelee kwenda kusalimia kaburi alidhani aliyekuwa anawalinda atafufuka instead ya kutumia muda hii kuhakikisha anaweka mambo sana na mama pamoja na watu aliowadhulumu Mali zao akiwemo mmiliki wa NAS Hauliers na akina manji pamoja na Ridhiwani pamoja na babake na mzee warioba.

Kazi wanayo.
Hakumkosea Mkulu aliwakosea Wasio na Hatia MUNGU ndio Kaamua Aadhibiwe
 
Wanachadema na kutaka wale waliowakalia kooni waondoke ,wamesahau kuwa serikali iliyopo ni ya CCM na wateule wake ni watekelezaji tu wa ilani ya CCM, vinginevyo wataangaliwa kama una ushahudu wa hao unaosema waliwaua.
We bwege kweli! Kwani ilani ya CCM ni uuaji, utekaji na ubakaji?
Unataka kumfanya mama Samia kuwa sehemu ya tabia zenu hizo za kishetani?
Hayo mambo yalikuwa ya magu na vijana wake majambazi aliyoyapa ofisi za umma.
 
Bavicha wanashangaza. Eti wanasubiri kuona Mama akinyonga "wanae" baada ya Baba wa "watoto" kufariki dunia. Uliona wapi ikitokea hivyo katika "familia" za kiafrika?
 
Wafuatie wasiojulikana kwa wingi wao ama kwa uchache wao ingependeza zaidi.
 
Inabidi iundwe Tume ya Maridhiano kama walivyofanya South Africa baada ya Utawala wa Kibaguzi kukomeshwa 1994, Tume ilikuwa chini ya Desmund Tutu, tusitumie utaratibu wa Kagame wa kuwapeleka Magakamani wale Wahalifu kwny Mahakama za Gachwachwa.

'Zamani Tajiri alikuwa anaweza kufanya lolote lakin Sasa hivi anaweza 'Kufanywa' lolote'- Kauli ngumu sana hii maana hata Madikteta kina Kagema hawana huu ujasiri wa kutamka haya hadharan

Kwa Niaba ya Wastaafu wa UV CCM Taifa tunawaomba radhi waliopata madhila ya kudhulumiwa Mali na nafsi zao na za Wapendwa wao
 
Bashite, musiba, kapilimba, doto james,Herry James, Henry Kisanduku, makungu wajiande nyumba ni lzm iwe safi.
 
Inabidi iundwe Tume ya Maridhiano kama walivyofanya South Africa baada ya Utawala wa Kibaguzi kukomeshwa 1994, Tume ilikuwa chini ya Desmund Tutu, tusitumie utaratibu wa Kagame wa kuwapeleka Magakamani wale Wahalifu kwny Mahakama za Gachwachwa.
Tume ya mariadhiano ya nini hali wahalifu wanajulikana.

South africa na Rwanda ilikuwa kwa Jamii nzima
 
Tume ya maridhiano kwa lengo la kuombana radhi na msamaha yaishe, Mahakamani yataibuka mengi na mengi na pengine wapo wataochomekewa kesi na Maadui zao wa Kisiasa na kuumizwa kwa kusingiziwa au wapo watakaokuja kuachiwa huru wakati ni wahalifu kweli hivyo kuleta chuki maradufu
Tume ya mariadhiano ya nini hali wahalifu wanajulikana.
South africa na Rwanda ilikuwa kwa Jamii nzima
 
Back
Top Bottom