Tujifunze neno Kleptocracy au Kleptokrasia serikali na madhara yake kwa nchi husika

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Wakuu, habari za jumapili na bila shaka kila mwana JF kaimaliza jumapili hii tukufu huku wengine wakienda kwenye ibada, sehemu za starehe, kutembelea ndugu, jamaa na marafiki kama ilivyo kwa tamaduni na desturi zetu wenyeji huandaa maakuli na vinywaji kutukaribisha sie wageni wao.

Sasa basi jana nilipata nafasi ya kwenda kuhudhuria mhadhara wa profesa mmoja wa sayansi ya siasa. Profesa huyu ambae amebobea kwenye utaalam wa siasa za kimataifa hutumia mihadhara yake maalum ambayo humuingiza kiasi kizuri cha pesa na yeye huishi hivyo yaani kupiga lectures darasani na mwisho wa wiki khasa jumamosi hutumia muda wake wa ziada kupiga darasa la mihadhara.

Mapato haya ya ziada kwa profesa huyu ni zile ada wanozilipa wahudhuriaji wa mihadhara yake, na wageni wengine maalum. Akikokotoa kila kitu kuhusu makato ya gharama za ukumbi, msimamizi wa mihadhara na wasaidizi wawili watatu, basi profesa huyu wiki inofuata huenda benki akiwa na furaha sana.

Profesa alianza kutoa mhadhara na alianza na maelezo mafupi kuhusu wanasiasa wapotoshaji na kwanini wanasiasa hupenda kudanyanya. Profesa aeleza tofauti kati ya kudanganya kwa kujinufaisha na udanyanyaji wa kistratejia. Udanyanyaji wa kujinufaisha ni ule wa wanasiasa kujijenga kisiasa kwa kutumia uongo na kuahidi mambo mbalimbali na ahadi hewa.

Udanyanyaji wa kistratejia ni kule kudanganya ambapo mwanasiasa hudanganya kwa minajili ya kuwatuliza wasikilizaji na kuwafanya waamini kuwa udanganyaji ule ni dhahiri na kwa kuwa wananchi hao hawana jinsi ya kumkabili mwanasiasa yule kwa shingo upande huukubali udanganyaji ule na mwisho ule udanganyifu hujisimika ndani ya akili zao.

Lakini pia kuna mambo mawili kusema ukweli na kudanganya . Kusema ukweli katika siasa ni pale mwanasiasa anaposimama jukwaani na kusema ukweli, akitumia vigezo na mifano hai huku akitumia muda kufafanua mambo kadhaa na kujenga hoja kutokana na ukweli huo.

Udanganyifu ni pale mwanasiasa anaposimama jukwaani kudanganya na ni kinyume kabisa na ukweli . Udanganyifu (deception) huu wa kistratejia umegawanyika katika sehemu tatu yaani kuzungusha maneno na kauli za kuchanganya (spining), uongo ( lies), na kuficha ukweli (concealing).

Kudanganya kwa minajili ya kuchanganya au "spining" ni pale mwanasiasa anapotoa kauli kadhaa au kauli mbalimbali kwa malengo ya kumfanya msikilizaji afikie hitimisho lisilo sahihi yaani "false conclusion". Kudanganya kwa kutoa kauli za uongo ni pale mwanasiasa anapotoa kauli za uongo bila aibu huku akifahamu wazi kuwa amesema uongo hadharani.

Kudanganya kwa kuuficha ukweli ni pale mwanasiasa anapotoa kauli tata ambazo zimeficha na hazina vigezo au "facts" lakini hubebwa na wasikilizaji na kusambazwa kuwa ndo kauli ya mwanasisa fulani ambae wakati mwingine huwa mwanasiasa mwandamizi ambae wengi wataamini kauli atazotoa.

Hivyo nikakumbuka kauli kadhaa wanozitoa viongozi hadharani na nikafikia hitimisho kwamba kweli bara letu la Afrika limefikia hatua mbaya sana.

Lakini hilo la profesa wetu nikaliacha na nikadokoa neno moja aloligusia ambalo ndilo kusudio la mada yangu ya leo neno liitwalo "Kleptocracy" au Kleptokrasia. Ni neno kama la demokrasia au "Democracy".

Je, nini maana ya neno hili na je, lina madhara gani huko mbele endapo litaachwa au mfumo wake utaachwa usambae hadi huko duniani?

Neno Kleptocracy latokana na maneno mawili ya kigiriki yaani Klepto ni mwizi au (thief) na Kratia yaani nguvu na kutawala (power and rule).

Kleptokrasia ni mfumo ulotengenezwa na serikali dhalimu na yenye viongozi na watumishi wake ambao wengi ni wezi, mawakala wa nchi za nje na pia wapo kujinufaisha wenyewe, familia na ndugu zao na pia kibaya zaidi kuhamisha mali nje na vyanzo vya uchumi wa nchi husika kwenda nje.

Kwa maana ingine ni kwamba hii ni serikali iliyomo katika nchi iitwayo ya wapigaji na pia hutumika jina jingine kwa kiingereza liitwalo "thievocracy" yaani serikali ambayo ina viongozi mafisadi ambao hutumia nguvu na nafasi zao za kisiasa kutumia vibaya mali za umma na fedha za umma ambao ni walipa kodi. Mara nyingi ikitokea mali na fedha za umma zimetumiwa vibaya au kuibiwa na watumishi au viongozi mafisadi huwa hakuna maelezo yoyote yatotolewa wala hakuna hatua zozote zitazochukuliwa dhidi ya wahusika kesi zote hufungwa yaani "case closed".

Katika nchi inoongozwa na serikali ya wapigaji au Kleptokrasia hazina ya taifa huwa ipo mikononi mwa mafisadi na wengi hutumia kila mwanya kuchota fedha za umma kwa manufaa yao binafsi na familia zao na pia kuwa na akaunti benki khasa nje ya nchi na hata kununua mali nje ya nchi kwa ajili ya maisha yao baada ya siasa za Kleptocrasia.

Ipo mifano ya nchi ambazo zimeongozwa na viongozi au wanasiasa kupitia kleptokrasia. Mobutu Sese Seko wa ilokuwa Zaire sasa Congo DRC alihamisha mali nyingi kwenda Ufaransa, Jenerali Sani Abacha wa Nigeria alihamisha fedha nyingi kwenda katika benki za Geneva na hata kiongozi wa Filipino Ferdinand Marcos nae aliripotiwa kuiba kiasi cha dola kati ya bilioni 5 na 10 kutoka benki kuu ya Philipines.

Je, ni tabia zipi huwepo katika nchi ambazo zina mfumo wa kleptokrasia na ni madhara yepi yatatokea ikiwa Kleptokrasia itaachiwa ishike mizizi?

Lakini kwanza tuangalie tabia za nchi ya wapigaji inoongozwa na mfumo wa Klepokrasia.

1. Nchi nyingi zenye mfumo wa Kleptokrasia zaongozwa na watu walotokana na mfumo upendeleo au "Nepotism" ambao umeundwa na kuimarishwa na mfumo wa Kleptokrasia. Viongozi ambao ni mafisadi wanakuwa wametumia nafasi zao kupitisha majina ya ndugu zao, watoto wao na hata marafiki zao bila kujali uwezo wao ili washike madaraka na nafasi nyeti katika serikali kwa minajili ya kuwalinda mara watapotoka madarakani.

2. Uchumi wa nchi kuyumba kwa maana kwamba serikali ya wapigaji inakuwa inakopa sana katika vyombo vya fedha vya nje kwa kuweka dhamana maliasili na rasilimali za nchi. Uchumi huo huja kugeuka kuwa ni ule uitwao "Economic Rent" kwani nchi haizalishi chochote lakini inalipa madeni yatokanayo na rasilimali zake na kuwanufaisha wachache na wale wanowakopesha ambao wako nje ya nchi hiyo.

Pia uchumi huo husababisha mfumuko mkubwa wa bei kwa wafanyabiashara kujiamulia bei bila kujali serikali ambayo wengi wao wana ushirika katika kuipiga.

3. Kushuka kwa kiwango cha wanoajiriwa. Hii au "Unemployment" hutokea pale ambapo soko la ndani la ajira hupokwa na wale wenye "connections" na makampuni ya nje ambapo kama ni biashara ya hoteli, benki, kapuni za kutoa ushauri elekezi na makapuni mengine ya kigeni huingia mikataba na viongozi mafisadi na watu wao na mwisho makampuni hayo huwa na access na sheria za ajira na uhamiaji.

Jambo hili hupelekea ajira nyingi kutolewa kwa wageni katika mahoteli na makampuni makubwa kwa kuzingatia kuwa waajiriwa wao huwa na elimu na utaalam kuzidi wale waajiriwa watarajiwa wa nchi husika.

4. Kuvurugika kwa mfumo wa fedha au "Financial System". Hii husababishwa na fedha haramu kuingizwa katika mfumo huo na maduka ya fedha za kigeni mengi kuwa hayana udhibiti kutoka katika serikali husika na benki kuu yake. Kupitia njia hiyo fedha nyinig za kigeni huadimika na wakati huohuo fedha nyingi za ndani huhamishiwa nje ya nchi husika na kuiacha haina fedha za kigeni za kutosha ambazo ingezitumai kuagiza bidhaa adimu kama vile chakula cha dharura au madawa.

Pia katika mfumo huu hutokea vitendo vya utakatishaji fedha yaani "money laundering" ambapo viongozi mafisadi huweza kuhamishia fedha nje ya nchi na hata kutumia fedha hizo kununua mali zisizohamishika kama nyumba, kununua vyombo vya habari ili kuwajengea taswira nzuri machoni mwa umma na kuajiri wanasheria ambao watazuia aina yoyote ya kuhoji au kuchunguza jinzi walivyozipata mali hizo.

Hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo hutawala katika mfumo wa Kleptokrasia ambapo wapigaji huwa wameshika kila nyanja ya nchi hiyo.

Sasa tuangalie madhara yanotokana na mfumo wa Kleptokrasia.

1. Kuyumba kwa uchumi.

Uchumi wa nchi kuyumba na kusababisha sintofahamu ambapo serikali ya wapigaji hushindwa kudhibiti mfumuko wa bei. Bei ya bidhaa adimu huzidi kupaa bila kuwepo maelezo ya kina na hatia zilichukuliwa kudhibiti bei hizo ingawa viongozi mafisadi wanaweza kujotokeza na kutoa kauli za kudanyanga kwa minajili ya kupotosha na kufanya spining bila kutoa vigezo yaani facts.

2. Siasa kuvurugwa kwa makusudi.

Katika mfumo huu khasa kuelekea kwenye chaguzi viongozi hutumia rasilimali na fedha nyingi kunadi au kupigia chapuo ahadi hewa au kujaribu kutetea (justfying) masuala na sera mbalimbali ambazo zimefeli au zimekwama lakini bila kutoa ufafanuzi wa kina uloambatana na vigezo. Pia viongozi hutumia muda na mali kuhakikisha wafanya mikutano na kujaribu kuonyesha wananchi kuwa wazijali shida zao huku wakifahamu wazi kuwa hakuna ukweli wowote ule.

3. Kubinywa kwa harakati za kisiasa.

Viongozi wa nchi ya wapigaji katika mfumo wa kleptokrasia huwa makini sana na siasa za upinzani kwa kuhakikisha hakuna kauli za kuelimisha jamii. Wanasiasa wa upinzani huwekwa sawa kwa lazima na hata kutishiwa kufungwa jela endapo hawatakubaliana na mwenendo wa serikali iliyopo madarakani na mawakala wake. Ikitokea kuna jambo la kulijadili kitaifa ni lazima jambo hilo litadhibitiwa na kuhakikisha vyombo vya habari havizungumzii sana jambo hilo.

4. Nchi kutekwa au "state capture".

Hapa simaanishi kwamba nchi imepinduliwa bali namaanisha kuwa nchi inakuwa iko mikononi kwa mafisadi kwa asilimia 101. Mfumo wa kleptokrasia kusababisha nchi ya wapigaji kutengeneza mfumo wa kifisadi ambao hutawala maamuzi mengi kwa nchi husika ambayo hayatawaathiri mafisadi na wapigaji. Mfano wa nchi kutekwa ni Afrika Kusini ambapo mwaka 2016 aliekuwa raisi wa nchi hiyo Jacob Zuma alituhumiwa kuwa na urafiki na familia ya akina Gupta ambayo ilikuwa na uwezo wa kuchagua mawaziri au viongozi wa aina gani wapewe nafasi katika serikali yake.

Hayo ni machache tu lakini yapo mengi mengi ambayo yangejaza mada yangu kama kuanzishwa kwa vikundi vya machawa, kutumia vyombo vya habari na asasi mbalimbali mitandaoni pamoja na kufanya kampeni mbalimbali kuhakikisha wananchi watulizwa kwa maneno mazuri.

Nini cha kufanya au what to do?

1. Mtazamo mpya.

Mtazamo mpya utatokana na serikali makini ambayo itatokana na mfumo mpya wa siasa unozingatia katiba ilorekebishwa na ambayo ndo mwongozo wa taifa hilo.

2. Kujitengeneza upya au reset.

Serikali pamoja na viongozi na kila mwananchi ni lazima wajitambue na watambue kwamba kuna makosa makubwa yanotokana na mfumo wa kleptokrasia.

3. Kufanyia mabadiliko sera za uchumi ili kuendana na mahitaji ya nchi khasa mfumuko wa bei, soko la ajira na huduma za jamii.

4. Marekebisho ya sheria ya uhamiaji ambayo yatazingatia kulinda ajira za ndani na kupunguza au kuzia ajira za kiholela. Makampuni ya nje ni lazima yawe yamejitosheleza na mahitaji ya waajiwriwa wa ndani kabla ya kuanza kuajiri watu kutoka nje.

Hayo ni machache tu katika mfumo huu wa kleptokrasia lakini nafikiri msomaji atakuwa amepata mawili matatu kuhusiana na neno hili na jinsi mfumo huu unavyotumika katika sehemu mbalimbali duniani. Lakini mfumo huu ni mbaya sana kwa nchi na ukiachiwa uote mizizi utasababisha kuwepo na jamii mpya ndani ya jamii iliyopo ambapo jamii hiyo mpya ndio yenye kutoa maamuzi makubwa yanohusu mstakabali mzima wa nchi husika.
 
Haya yote yanawezekana zaidi afrika na hapa kwetu Tanzania ni zaidi.
Mradi unafadhiliwa na Mataifa mengine mwanzo mpaka mwisho, bado utasikia serikali inakwambia tumetumia Bilioni ... kukamilisha mradi. Yani pesa za mfadhili hazitajwi na mradi una bango Donated by to Tanzania by Japan Government.
 
Naona umeichambua awamu ya sita vilivyo!

Hapo namna pekee ni kumuingiza jpm mpya atakaefunga na kufilisi mafisadi na kupiga pin akaunti za makada huko majuu!

Kuna watu lazima watangulizwe Ili kufikia malengo mapya ya kisera!

Mafisadi wameamua Hadi umeme uwake Kwa massa mangapi na ukatike kwenye matukio muhimu!

Ni kweli kabisa awam hii ipo mfukoni mwa elites was kifisadi!

True state capture!

Nataka uchambuzi wako kuhusu Congo DRC M23 na vita inayoendelea dhidi ya majeshi ya wanachama wakisaidiana na ya serikali!
 
Wakuu, habari za jumapili na bila shaka kila mwana JF kaimaliza jumapili hii tukufu huku wengine wakienda kwenye ibada, sehemu za starehe, kutembelea ndugu, jamaa na marafiki kama ilivyo kwa tamaduni na desturi zetu wenyeji huandaa maakuli na vinywaji kutukaribisha sie wageni wao.
at least kuna alternative plans but nani anae aminika wa kuongoza uelekeo wa mabadiliko mbadala 🐒

Almost hakuna,
na kwahivyo hakuna kitisho cha alternative plans kinachoweza kuhatarisha kuondolewa madarakani kwa mamlaka zilizopo 🐒

uchu wa madarka, ubinafsi, kutokuaminiani, kugawanyika, kujipa ujasiri na umuhimu wa kipekee dhidi ya wengine, kutokua na mipango, sauti, dira na uelekeo wa pamoja miongoni mwa oppositions nchini kunafanya kuifanya mamlaka iliyopo madarakani kuwa comfortable zaidi na kufanya chochote itakavyo politically speaking.......
 
Donald Trump aendelea kuzoa kura kwa şababu yeye ndie asemae ukweli.

Na endapo Trump atashinda uchaguzi mwezi November, basi dunia itatikisika mtikisiko mkuu.

Wamarekani wameamua watatumia vema sanduku la kura kumuondoa Joe Biden.
 
at least kuna alternative plans but nani anae aminika wa kuongoza uelekeo wa mabadiliko mbadala 🐒

Almost hakuna,
na kwahivyo hakuna kitisho cha alternative plans kinachoweza kuhatarisha kuondolewa madarakani kwa mamlaka zilizopo 🐒

uchu wa madarka, ubinafsi, kutokuaminiani, kugawanyika, kujipa ujasiri na umuhimu wa kipekee dhidi ya wengine, kutokua na mipango, sauti, dira na uelekeo wa pamoja miongoni mwa oppositions nchini kunafanya kuifanya mamlaka iliyopo madarakani kuwa comfortable zaidi na kufanya chochote itakavyo politically speaking.......
Wakati mwingine kurogwa si ndumba na kazi kubwa za Masangoma.

Mikutano tu na misafara ikipita watu hurogeka.
 
Haya yote yanawezekana zaidi afrika na hapa kwetu Tanzania ni zaidi.
Mradi unafadhiliwa na Mataifa mengine mwanzo mpaka mwisho, bado utasikia serikali inakwambia tumetumia Bilioni ... kukamilisha mradi. Yani pesa za mfadhili hazitajwi na mradi una bango Donated by to Tanzania by Japan Government.
Kuna masuala kadhaa ambayo serikali ikiyazingatia kindakindaki kunakuwa hakuna shida.

1. Uwajibikaji
2. Uwazi
3. Kuwa tayari kuwawajibisha watumishi wanotumia vibaya au kukwiba fedha za umma, miradi, hisani na misaada.
4. Kuwa wakweli.
5. Kukiri makosa na kuwa tayari kuyarekebisha mara moja.

Na mengineyo mengi.

Kuhusu wafadhili nao wengi ni sehemu ya ufusadi na wapigaji kwani si wangeweza kuzuia fedha zao wanapoziona zatumiwa vibaya au wanapopelekewa mchakato hewa wa matumizi?

Au Benki ya Dunia, benki ya maendeleo ya Afrika na IMF si wana data zote kwamba nchi fulani yaendeshwa kwa mfumo wa Kleptokrasia?

Wangeweza kabisa kusema hapana mbona pesa hii na ile hatuoni zimetumika vipi hivyo wangesimamisha kuendelea kutoa mikopo hadi hali ijirudi kwenye nchi husika?
 
Wakati mwingine kurogwa si ndumba na kazi kubwa za Masangoma.

Mikutano tu na misafara ikipita watu hurogeka.
ndrugo mtoa hoja,
Mbona unatupoteza maboya na misamiati, misemo na nahau za wahenge 🐒

si utupitishe relini moja kwa moja tujijue vizur ni wa ndumba, msongamano, kurogwa au msafara 🐒
 
Wakuu, habari za jumapili na bila shaka kila mwana JF kaimaliza jumapili hii tukufu huku wengine wakienda kwenye ibada, sehemu za starehe, kutembelea ndugu, jamaa na marafiki kama ilivyo kwa tamaduni na desturi zetu wenyeji huandaa maakuli na vinywaji kutukaribisha sie wageni wao.

Sasa basi jana nilipata nafasi ya kwenda kuhudhuria mhadhara wa profesa mmoja wa sayansi ya siasa. Profesa huyu ambae amebobea kwenye utaalam wa siasa za kimataifa hutumia mihadhara yake maalum ambayo humuingiza kiasi kizuri cha pesa na yeye huishi hivyo yaani kupiga lectures darasani na mwisho wa wiki khasa jumamosi hutumia muda wake wa ziada kupiga darasa la mihadhara.

Mapato haya ya ziada kwa profesa huyu ni zile ada wanozilipa wahudhuriaji wa mihadhara yake, na wageni wengine maalum. Akikokotoa kila kitu kuhusu makato ya gharama za ukumbi, msimamizi wa mihadhara na wasaidizi wawili watatu, basi profesa huyu wiki inofuata huenda benki akiwa na furaha sana.

Profesa alianza kutoa mhadhara na alianza na maelezo mafupi kuhusu wanasiasa wapotoshaji na kwanini wanasiasa hupenda kudanyanya. Profesa aeleza tofauti kati ya kudanganya kwa kujinufaisha na udanyanyaji wa kistratejia. Udanyanyaji wa kujinufaisha ni ule wa wanasiasa kujijenga kisiasa kwa kutumia uongo na kuahidi mambo mbalimbali na ahadi hewa.

Udanyanyaji wa kistratejia ni kule kudanganya ambapo mwanasiasa hudanganya kwa minajili ya kuwatuliza wasikilizaji na kuwafanya waamini kuwa udanganyaji ule ni dhahiri na kwa kuwa wananchi hao hawana jinsi ya kumkabili mwanasiasa yule kwa shingo upande huukubali udanganyaji ule na mwisho ule udanganyifu hujisimika ndani ya akili zao.

Lakini pia kuna mambo mawili kusema ukweli na kudanganya . Kusema ukweli katika siasa ni pale mwanasiasa anaposimama jukwaani na kusema ukweli, akitumia vigezo na mifano hai huku akitumia muda kufafanua mambo kadhaa na kujenga hoja kutokana na ukweli huo.

Udanganyifu ni pale mwanasiasa anaposimama jukwaani kudanganya na ni kinyume kabisa na ukweli . Udanganyifu (deception) huu wa kistratejia umegawanyika katika sehemu tatu yaani kuzungusha maneno na kauli za kuchanganya (spining), uongo ( lies), na kuficha ukweli (concealing).

Kudanganya kwa minajili ya kuchanganya au "spining" ni pale mwanasiasa anapotoa kauli kadhaa au kauli mbalimbali kwa malengo ya kumfanya msikilizaji afikie hitimisho lisilo sahihi yaani "false conclusion". Kudanganya kwa kutoa kauli za uongo ni pale mwanasiasa anapotoa kauli za uongo bila aibu huku akifahamu wazi kuwa amesema uongo hadharani.

Kudanganya kwa kuuficha ukweli ni pale mwanasiasa anapotoa kauli tata ambazo zimeficha na hazina vigezo au "facts" lakini hubebwa na wasikilizaji na kusambazwa kuwa ndo kauli ya mwanasisa fulani ambae wakati mwingine huwa mwanasiasa mwandamizi ambae wengi wataamini kauli atazotoa.

Hivyo nikakumbuka kauli kadhaa wanozitoa viongozi hadharani na nikafikia hitimisho kwamba kweli bara letu la Afrika limefikia hatua mbaya sana.

Lakini hilo la profesa wetu nikaliacha na nikadokoa neno moja aloligusia ambalo ndilo kusudio la mada yangu ya leo neno liitwalo "Kleptocracy" au Kleptokrasia. Ni neno kama la demokrasia au "Democracy".

Je, nini maana ya neno hili na je, lina madhara gani huko mbele endapo litaachwa au mfumo wake utaachwa usambae hadi huko duniani?

Neno Kleptocracy latokana na maneno mawili ya kigiriki yaani Klepto ni mwizi au (thief) na Kratia yaani nguvu na kutawala (power and rule).

Kleptokrasia ni mfumo ulotengenezwa na serikali dhalimu na yenye viongozi na watumishi wake ambao wengi ni wezi, mawakala wa nchi za nje na pia wapo kujinufaisha wenyewe, familia na ndugu zao na pia kibaya zaidi kuhamisha mali nje na vyanzo vya uchumi wa nchi husika kwenda nje.

Kwa maana ingine ni kwamba hii ni serikali iliyomo katika nchi iitwayo ya wapigaji na pia hutumika jina jingine kwa kiingereza liitwalo "thievocracy" yaani serikali ambayo ina viongozi mafisadi ambao hutumia nguvu na nafasi zao za kisiasa kutumia vibaya mali za umma na fedha za umma ambao ni walipa kodi. Mara nyingi ikitokea mali na fedha za umma zimetumiwa vibaya au kuibiwa na watumishi au viongozi mafisadi huwa hakuna maelezo yoyote yatotolewa wala hakuna hatua zozote zitochukuliwa dhidi ya wahusika kesi zote hufungwa yaani "case closed".

Katika nchi inoongozwa na serikali ya wapigaji au Kleptokrasia hazina ya taifa huwa ipo mikononi mwa mafisadi na wengi hutumia kila mwanya kuchota fedha za umma kwa manufaa yao binafsi na familia zao na pia kuwa na akaunti benki khasa nje ya nchi na hata kununua mali nje ya nchi kwa ajili ya maisha yao baada ya siasa za Kleptocrasia.

Ipo mifano ya nchi ambazo zimeongozwa na viongozi au wanasiasa kupitia kleptokrasia. Mobutu Sese Seko wa ilokuwa Zaire sasa Congo DRC alihamisha mali nyingi kwenda Ufaransa, Jenerali Sani Abacha wa Nigeria alihamisha fedha nyingi kwenda katika benki za Geneva na hata kiongozi wa Filipino Ferdinand Marcos nae aliripotiwa kuiba kiasi cha dola kati ya bilioni 5 na 10 kutoka benki kuu ya Philipines.

Je, ni tabia zipi huwepo katika nchi ambazo zina mfumo wa kleptokrasia na ni madhara yepi yatatokea ikiwa Kleptokrasia itaachiwa ishike mizizi?

Lakini kwanza tuangalie tabia za nchi ya wapigaji inoongozwa na mfumo wa Klepokrasia.

1. Nchi nyingi zenye mfumo wa Kleptokrasia zaongozwa na watu walotokana na mfumo upendeleo au "Nepotism" ambao umeundwa na kuimarishwa na mfumo wa Kleptokrasia. Viongozi ambao ni mafisadi wanakuwa wametumia nafasi zao kupitisha majina ya ndugu zao, watoto wao na hata marafiki zao bila kujali uwezo wao ili washike madaraka na nafasi nyeti katika serikali kwa minajili ya kuwalinda mara watapotoka madarakani.

2. Uchumi wa nchi kuyumba kwa maana kwamba serikali ya wapigaji inakuwa inakopa sana katika vyombo vya fedha vya nje kwa kuweka dhamana maliasili na rasilimali za nchi. Uchumi huo huja kugeuka kuwa ni ule uitwao "Economic Rent" kwani nchi haizalishi chochote lakini inalipa madeni yatokanayo na rasilimali zake na kuwanufaisha wachache na wale wanowakopesha ambao wako nje ya nchi hiyo.

Pia uchumi huo husababisha mfumuko mkubwa wa bei kwa wafanyabiashara kujiamulia bei bila kujali serikali ambayo wengi wao wana ushirika katika kuipiga.

3. Kushuka kwa kiwango cha wanoajiriwa. Hii au "Unemployment" hutokea pale ambapo soko la ndani la ajira hupokwa na wale wenye "connections" na makampuni ya nje ambapo kama ni biashara ya hoteli, benki, kapuni za kutoa ushauri elekezi na makapuni mengine ya kigeni huingia mikataba na viongozi mafisadi na watu wao na mwisho makampuni hayo huwa na access na sheria za ajira na uhamiaji.

Jambo hili hupelekea ajira nyingi kutolewa kwa wageni katika mahoteli na makampuni makubwa kwa kuzingatia kuwa waajiriwa wao huwa na elimu na utaalam kuzidi wale waajiriwa watarajiwa wa nchi husika.

4. Kuvurugika kwa mfumo wa fedha au "Financial System". Hii husababishwa na fedha haramu kuingizwa katika mfumo huo na maduka ya fedha za kigeni mengi kuwa hayana udhibiti kutoka katika serikali husika na benki kuu yake. Kupitia njia hiyo fedha nyinig z akgeni huadimika na wakti huohuo fedha nyingi za ndani huhamishiwa nje ya nchi husika na kuiacha haina fedha za kigeni za kutosha ambazo ingezitumai kuagiza bidhaa adimu kama vile chakula cha dharura au madawa.

Pia katika mfumo huu hutokea vitendo vya utakatishaji fedha yaani "money laundering" ambapo viongozi mafisadi huweza kuhamishia fedha nje ya nchi na hata kutumia fedha hizo kununua mali zisizohamishika kama nyumba, kununua vyombo vya habari ili kuwajengea taswira nzuri machini mwa umma na kuajiri wanasheria ambao watazuia aina yoyote ya kuhoji au kuchunguza jinzi walivyozipata mali hizo.

Hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo hutawala katika mfumo wa Kleptokrasia ambapo wapigaji huwa wameshika kila nyanja ya nchi hiyo.

Sasa tuangalie madhara yanotokana na mfumo wa Kleptokrasia.

1. Kuyumba kwa uchumi.

Uchumi wa nchi kuyumba na kusababisha sintofahamu ambapo serikali ya wapigaji hushindwa kudhibiti mfumuko wa bei. Bei ya bidhaa adimu huzidi kupaa bila kuwepo maelezo ya kina na hatia zilichukuliwa kudhibiti bei hizo ingawa viongozi mafisadi wanaweza kujotokeza na kutoa kauli za kudanyanga kwa minajili ya kupotosha na kufanya spining bila kutoa vigezo yaani facts.

2. Siasa kuvurugwa kwa makusudi.

Katika mfumo huu khasa kuelekea kwenye chaguzi viongozi hutumia rasilimali na fedha nyingi kunadi au kupigia chapuo ahadi hewa au kujaribu kutetea (justfying) masuala na sera mbalimbali ambazo zimefeli au zimekwama lakini bila kutoa ufafanuzi wa kina uloambatana na vigezo. Pia viongozi hutumia muda na mali kuhakikisha wafanya mikutano na kujaribu kuonyesha wananchi kuwa wazijali shida zao huku wakifahamu wazi kuwa hakuna ukweli wowote ule.

3. Kubinywa kwa harakati za kisiasa.

Viongozi wa nchi ya wapigaji katika mfumo wa kleptokrasia huwa makini sana na siasa za upinzani kwa kuhakikisha hakuna kauli za kuelimisha jamii. Wanasiasa wa upinzani huwekwa sawa kwa lazima na hata kutishiwa kufungwa jela endapo hawatakubaliana na mwenendo wa serikali iliyopo madarakani na mawakala wake. Ikitokea kuna jambo la kulijadili kitaifa ni lazima jambo hilo litadhibitiwa na kuhakikisha vyombo vya habari havizungumzii sana jambo hilo.

4. Nchi kutekwa au "state capture".

Hapa simaanishi kwamba nchi imepinduliwa bali namaanisha kuwa nchi inakuwa iko mikononi kwa mafisadi kwa asilimia 101. Mfumo wa kleptokrasia kusababisha nchi ya wapigaji kutengeneza mfumo wa kifisadi ambao hutawala maamuzi mengi kwa nchi husika ambayo hayatawaathiri mafisadi na wapigaji. Mfano wa nchi kutekwa ni Afrika Kusini ambapo mwaka 2016 aliekuwa raisi wa nchi hiyo Jacob Zuma alituhumiwa kuwa na urafiki na familia ya akina Gupta ambayo ilikuwa na uwezo wa kuchagua mawaziri au viongozi wa aina gani wapewe nafasi katika serikali yake.

Hayo ni machache tu lakini yapo mengi mengi ambayo yangejaza mada yangu kama kuanzishwa kwa vikundi vya machawa, kutumia vyombo vya habari na asasi mbalimbali mitandaoni pamoja na kufanya kampeni mbalimbali kuhakikisha wananchi watulizwa kwa maneno mazuri.

Nini cha kufanya au what to do?

1. Mtazamo mpya.

Mtazamo mpya utatokana na serikali makini ambayo itatokana na mfumo mpya wa siasa unozingatia katiba ilorekebishwa na ambayo ndo mwongozo wa taifa hilo.

2. Kujitengeneza upya au reset.

Serikali pamoja na viongozi na kila mwananchi ni lazima wajitambue na watambue kwamba kuna makosa makubwa yanotokana na mfumo wa kleptokrasia.

3. Kufanyia mabadiliko sera za uchumi ili kuendana na mahitaji ya nchi khasa mfumuko wa bei, soko la ajira na huduma za jamii.

4. Marekebisho ya sheria ya uhamiaji ambayo yatazingatia kulinda ajira za ndani na kupunguza au kuzia ajira za kiholela. Makampuni ya nje ni lazima yawe yamejitosheleza na mahitaji ya waajiwriwa wa ndani kabla ya kuanza kuajiri watu kutoka nje.

Hayo ni machache tu katika mfumo huu wa kleptokrasia lakini nafikiri msomaji atakuwa amepata mawili matatu kuhusiana na neno hili na jinsi mfumo huu unavyotumika katika sehemu mbalimbali duniani. Lakini mfumo huu ni mbaya sana kwa nchi na ukiachiwa uote mizizi utasababisha kuwepo na jamii mpya ndani ya jamii iliyopo ambapo jamii hiyo mpya ndio yenye kutoa maamuzi makubwa yanohusu mstakabali mzima wa nchi husika.
Prof.alikuwa anaisema Tz ya Samia,Mafisadi wote ndo wamemzunguka,Samia ni flying president, hakai nyumbani yeye kiguu na njia na kiushungi chake wakati nchi haina maji,umeme shida,ajira hakuna,huduma za afya mbovu etc
Yeye wala hajali zaidi ya kujipaka hina na kuvaa saa za gharama.
We've poor president since Uhuru.
 
ndrugo mtoa hoja,
Mbona unatupoteza maboya na misamiati, misemo na nahau za wahenge 🐒

si utupitishe relini moja kwa moja tujijue vizur ni wa ndumba, msongamano, kurogwa au msafara 🐒
Watu wakiishorogeka huwa lile wingu la ulozi huwafumba na kuwapumbaza kwelikweli.

Na ni lazima waanze kuuluzia kama ile misafara na mikutano yaendelea ama vipi.

Hiyo ni kwasababu ile dawa ilipulizwa na mfumo wa Kleptokrasia inakuwa yafanya kazi yake.

Wenzetu wanofanya maandamano huko kulikoendelea mara nyingi hujidamka mapema asubuhi, hupata kifungua kinywa, wana umeme 24/7, bidhaa kama sukari bei chee na wengi ni wale wenye uwezo kifedha pamoja na wale wanovuta fedha za kusaidiwa kila wiki.

Ndo maana mikutano yao ni ile inohusu mambo kama mabadiliko ya tabia nchi, uchafuzi mazingira, kupinga majaribio dhidi ya wanyama na suala la kuuliwa wapalestina huko Gaza.
 
Kuna masuala kadhaa ambayo serikali ikiyazingatia kindakindaki kunakuwa hakuna shida.

1. Uwajibikaji
2. Uwazi
3. Kuwa tayari kuwawajibisha watumishi wanotumia vibaya au kukwiba fedha za umma, miradi, hisani na misaada.
4. Kuwa wakweli.
5. Kukiri makosa na kuwa tayari kuyarekebisha mara moja.

Na mengineyo mengi.

Kuhusu wafadhili nao wengi ni sehemu ya ufusadi na wapigaji kwani si wangeweza kuzuia fedha zao wanapoziona zatumiwa vibaya au wanapopelekewa mchakato hewa wa matumizi?

Au Benki ya Dunia, benki ya maendeleo ya Afrika na IMF si wana data zote kwamba nchi fulani yaendeshwa kwa mfumo wa Kleptokrasia?

Wangeweza kabisa kusema hapana mbona pesa hii na ile hatuoni zimetumika vipi hivyo wangesimamisha kuendelea kutoa mikopo hadi hali ijirudi kwenye nchi husika?
Nchi hii ngumu sana, Kuna shirika la kijapan wanitwa JICA. Wao wakitoa msaada wana simamia wao huo mradi mpaka uishe wanaikabidhi serikali au taasisi husika kuendesha, ila wanakuwa karibu kuhakikisha mnasimamia vizuri maana wanatoa mafunzo.

Serikali yetu haikubali kusimamiwa wanajidai wajuaji lakini malengo yao ni kupiga pesa, na ku chepusha pesa kwenda kusiko hitajiaka, mfadhili atapewa vitabu vinavyoonyesha matumizi ya pesa lakini mradi haupo au uko nusu.
Teuzi ni za kujuana, mtoto wa fulani utamuwajibisha vipi. Watoto wa watawala wapo serikalini kibao tena nafasi za maamuzi, huyo anawajibishwa na nani?

Li nchi hili liache tu lijipeleke litakavyo.
 
Back
Top Bottom