Rais Samia anaongoza Nchi kwa ufanisi utafikiri alijiandaa kushika Urais kwa zaidi ya Miaka hamsini iliyopita

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,264
9,715
Ndugu zangu Watanzania,

Nikimuangalia na kumfuatilia Rais na jemedari wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge kwa namna anavyoongoza nchi,anavyofanya maamuzi kwa umakini na ujasiri, kwa namna alivyolileta Taifa pamoja na kujenga umoja wa kitaifa ,kwa namna alivyo leta maendeleo makubwa kwa muda mfupi na namna anavyoendelea kukamilisha miradi mikubwa mikubwa hapa nchini. kwa hakika nabaki kusema kuwa Rais Samia alizaliwa akiwa kiongozi na Karama ya uongozi pamoja na kibali cha Mwenyezi Mungu kuongoza watu na kukubalika mbele za watu.

Licha ya kuchukua Urais ghafla na pasipo kutarajia wala kuwaza katika akili za mtu yeyote yule mtanzania kwamba inaweza ikatokea Rais aliyekuwepo madarakani Hayati Mwalimu Dkt John Pombe Joseph Magufuli akafariki Duniani, tena ndani ya muda mfupi wa awamu yake ya pili lakini Rais Samia aliposhika tu madaraka hayo ya Urais ameonyesha utulivu wa hali ya juu sana kiuongozi,weledi wa kiuongozi,kifua cha uongozi,ulimi wa kiuongozi wenye hekima ,busara,upendo,subira , unyenyekevu na wenye kuchuja maneno Kabla ya kuyatoa hadharani.

Rais Samia mama yetu mpendwa hajawahi kuteteleka wala kutetereshwa wala kufanya mambo kwa pupa au kuonyesha ulimbukeni au ushamba wa madaraka ya Urais. kiukweli haijawahi kutokea kwa mama yetu huyu wakipekee mlezi wa Taifa letu na mboni ya Taifa. Siku zote amekuwa mvumilivu hata arushiwapo mikuki ya maneno kutoka kwa watu waliotaka kujaribu kumyumbisha kwa maslahi yao binafsi.kuna wakati watu walitaka hata kuleta ubaguzi na mpasuko katika Taifa letu kwa kutaka kupandikiza ubaguzi kwa misingi ya Udini,ukabila,ukanda pamoja na jinsia.lakini bado hakuteteleka wala kuyumba wala kupaniki zaidi ya kusimama na kusonga mbele kama komandoo wa jeshi aliyepo katika uwanja wa vita na mapambano.

Hatimaye upepo ulipita na Taifa likabakia imara,salama na tulivu katika mikono yake jemedari wetu na Mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hasssan. hajawahi kufanya maamuzi kwa kukurupuka wala mihemuko wala jazba wala kukimbia.bali hufanya maamuzi baada ya utafiti na uchunguzi wa kina kufanyika. Ni viongozi wachache sana hapa Duniani unaweza kuwapata na wakawa na sifa na uwezo wa kiuongozi kama alionao Mama yetu mpendwa mama Samia.

Haya yanafanyika huku kila mmoja akiwa anafahamu kuwa Rais wetu hajawahi kuchukua Fomu ya Urais wala kutia nia ya Urais wala kutangaza kuwa anataka Urais Kabla ya kuwa Rais mwaka 2021. Lakini anavyoongoza nchi unaweza ukafikiri kuwa alijiaandaa kushika Urais wa nchi yetu miaka zaidi ya hamsini iliyopita, unaweza ukafikiri labda alikuwa darasani akijifunza namna ya kuongoza Taifa letu na kujifunza namna ya kufanya maamuzi kwa nusu karne iliyopita.

Taifa lina amani ,furaha na matumaini tele katika vifua na mioyo ya watanzania.mpaka inafikia hatua Taifa la Marekani kupitia balozi wake hapa nchini akiupongeza Uongozi wa Rais Samia Mama shupavu ,imara na madhubuti katika bara zima la Afrika. ni lazima tumpatie awamu ya pili ya Urais ili kukamilisha kazi nzuri na njema anayoendelea kuifanyia katika Taifa letu hususani katika kukamilisha miradi mikubwa na ya kimkakati katika Taifa letu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Kumbuka impact ya magufuri imechangia haya anayoyafanya
 
Kama Rais Samia asingekuwa na uwezi wa kiuongozi au Karama ya uongozi basi asingeweza kuongoza Tafaletu.mpaka sasa tungekuwa tunaelekea gizani na kila kitu kizuri ambacho kilikuwa kimeanzia awamu ya tano basi kingebaki kama historia na kuishia njiani.lakini mama yetu wa shoka na jemedari wetu ameendelea kuonyesha ushupavu ,uimara na umadhubuti wake kiuongozi kwa kukamilisha kila kitu bila kukiachia njiani pamoja na kuanzisha miradi mingine mikubwa mikubwa .

Ni sawa na mtoto asiye na akili kichwani na kichwa maji akiachiwa utajiri na baba yake ataishia kuutapanya hovyo hovyo na kumaliza mali zote ndani ya muda mfupi hata kabla ya kuisha mwaka. Lakini mtoto mwenye akili akiachiwa mali na baba yake ataziendeleza na kuzalisha nyingine nyingi tu zitakazokutwa na kutumiwa na vizazi kwa vizazi bila kupotea.

Kwa hiyo ni akili,uwezo, uimara,uhodari , ushupavu, umadhubuti na maono pamoja na akili kubwa ya Rais Samia imetufikisha gapa tulipo mahali ambapo hata Marekani yenyewe inatupongeza sana kwa ubora wa kiuongozi uliopo madarakani chini ya jemedari wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hasssan
 
Huna akili, kazi yako kusifu hata hujielewi. Nenda akakuoe huko. Nini cha maana kafanya hadi uache akili zako chooni uanze kumsifu namna hiyo.
Matusi ni dalili ya kuikubali hoja na kushindwa namna ya kupanga hoja kwa hoja. nimekusamehe bure kabisa maana najuwa upeo wa akili yako ni mdogo sana.
 
Back
Top Bottom