Askofu Bagonza: Tuliyajua, Hatukuyajua lakini hilo zaidi ya tatizo

Naunga mkono hoja , kwani Pascal Mayala anasemaje? Hasa waliomuua Been Saanane , maana taarifa zao zimeanza kuvuja
Screenshot_20210605-203717.png
 
TULIYAJUA, HATUKUYAJUA, HILI NI ZAIDI YA TATIZO.

Kesi iko mahakamani, sitaki kusema yaliyomo ya kesi hiyo. Najipa haki ya kusema jambo zima kwa ujumla wake...
Baba Askofu- ongeza pia kwamba wanaotuhumu nao wachunguzwe sawia.
 

Sabaya pic

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya akiwa chini ya Ulinzi katika mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha wiki iliyopita. Picha na Maktaba

Summary

  • Wakati aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akianza maisha mapya mahabusu kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imesema inaendelea kumchunguza kwa kuwa imepokea malalamiko mengi zaidi dhidi yake.
Dar es Salaam. Wakati aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akianza maisha mapya mahabusu kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imesema inaendelea kumchunguza kwa kuwa imepokea malalamiko mengi zaidi dhidi yake.

Mbali na Sabaya, Takukuru imemtaja aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba hawamshikilii kwa mahojiano kama madai yaliyosambaa mitandaoni, lakini “wakati ukifika wakihitaji wataujulisha umma.’

Sabaya na wenzake watano walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Juni 4, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Alisimamishwa kazi na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, mwaka huu kupisha uchunguzi kabla ya kutiwa mbaroni na Takukuru na hatimaye kufikishwa mahakamani.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu kuendelea na uchunguzi wa Sabaya Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni alisema, “Tunafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya Jinai. Ni kweli tunaendelea na uchunguzi kadiri taarifa zinavyotufikia.”

Hamduni alieleza kuwa watu wengi wamejitokeza kuwasilisha malalamiko yao kuhusu Sabaya na hayo ndio wanayoyachambua na kuyachunguza kun a kama watamshtaki kupitia ofisi ya masktaka.

Alipoulizwa ni malalamiko ya aina gani yaliyowasilishwa na watu wa kada mbalimbali, alisema, “aaaah... tutawajulisha wakati muafaka.”

Katika siku za karibuni kumekuwa madai yanayoibuka dhidi ya Sabaya ikiwa ni pamoja na kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Hai, Simon Mnyampanda kiasi cha kuvunjwa miguu na mikono yote.

Mwingine anayedaiwa kutekwa na kupigwa misumari miguuni ni kada wa chama hicho, Hamisi Massanja ambaye ni katibu wa tawi la Chadema tawi la Rundugai wilayani humo.

“Ilikuwa Oktoba 24, 2020 wakati tunajiandaa na uchaguzi, walikuja nyumbani kwangu usiku na kuanza kunipiga mimi pamoja na watoto wangu.

“Nakumbuka nilimwona Sabaya akiwaamrisha walinzi wake wanipige. Baada ya hapo walinipeleka mahali ambapo sipafahamu kwenye pagale la nyumba na kuanza kunipiga mwili mzina na kunigonga misumari miguuni,” alisema Massanja alipozungumza kwa simu na Mwananchi jana.

Madai mengine ambayo ni ya muda mrefu ni ya mmiliki wa hoteli ya Weruweru Lodge, Cuthbert Swai ambaye mara kadhaa amedai kwenye mitandao ya jamii kuvamiwa na Sabaya akimlazimisha ampe fedha, madai ambayo Sabaya mwenyewe amekuwa akiyakanusha.

Mbatia atia neno
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na baadhi ya viongozi wa kada mbalimbali wenye dhamana usiishie tu kwa Sabaya bali unapaswa kuwaangalia na wengine ambao walijihusisha na matukio kama hayo.

“Jamii yenye migogoro haiwezi kustawi. Kinga ni bora kuliko tiba’ ni vyema kuchukua tahadhari mapema ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanavuruga haki za binadamu,” alisisitiza Mbatia, ambaye aliongeza kuwa matukio yote yenye viashiria vya kutosha vya chuki vilivyofanywa vinapaswa kushughulikiwa.

Uvumi kuhusu Makonda
Tangu juzi katika mitandao ya kijamii ziliibuka taarifa kuwa Makonda naye anashikiliwa kwa mahojiano na taasisi hiyo, ambazo Hamduni alisema izo hazina ukweli wowote.

“Mpaka sasa hatumshikilii Makonda, wakati ukifika tukihitaji tutawajulisha,” alisema Hamduni ambaye amewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.

Kuhusu utaratibu wa wanaohojiwa na Takukuru alisema si wote wanaokamatwa na kushikiliwa.

“Inategemeam si kila anayetuhumiwa anashikiliwa inategemea na mazingira na ulazima wa kuwa na huyo mtu na pia inategemea na aina ya tuhuma,” alisema Kamishna Hamduni.
 
Wakati wa agano la kale huyu jamaa alitakiwa awe kapigwa na yeye misumari ya inchi nne kwenye ugoko wake !! na pia awe na sikio moja.
 
Hakuna ushetani ambao Sabaya hakuufanya kwa wanadamu wenzake, ubakaji, ulawiti, mpaka kugonga watu misumari miguuni, anaemtetea Sabaya kwa namna yoyote ile ana laana.
 
Ni miaka 20 sasa imepita tangu uamuzi wa kuchoma kaya 135 uliotolewa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Serengeti Thomas Ole Sabaya , kuchomwa moto kwa kaya hizo kulitokea siku nne baada ya amri kutoka kwa mkuu wa wilaya kuwataka kuondoka eneo hilo kwa madai kuwa wananchi hao wanaishi katika eneo la Pori ala akiba la Ikorongo.

MAAMUZI YA MAHAKA BAADA YA TUKIO LA KUCHOMA NYUMBA HIZO.
Katika hukumu ya shauri namba 22/2005 lililofunguliwa na kaya hizo mbele ya Mahakama Kuu Kitengo cha ardhi kupitia msaada wa kituo cha Haki za Binadamu ,iliamuliwa kuwa kata hizo ziliondolewa kinyume na sheria na kuamuru warudishwe katika maeneo yao , akirejea Ibara ya 24 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano Tanzania , Jaji Mziray aliamuru kuwa kuondolewa kaya hizo katika maeneo yao ni kinyume na haki za binadamu.

KAULI YA SERIKALI.
Akielezea juu ya jambo hilo Naibu waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema serikali iko tayari kutekeleza maagizo yote ya Mahakama na tayari imerekebisha hati ya makazi ya eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 5000 ambayo ilikuwa inamilikiwa na kampuni bila binafsi kinyume na utaratibu.

Swali nalojiuliza huyu Thomas Ole Sabaya ana undugu na huyo Lengai Ole Sabaya?.....
 
Umeshindwa kumwondoa mbowe madarakani alafu unaota kuondoa ccm madarakani? Shame on you
 
Back
Top Bottom