Jiji la Dar ni kubwa sana na lina maeneo mengi sana yenye majina tofauti tofauti, Je! Nini kilipelekea mpaka haya maeneo yakapewa majina kama MABIBO, MBAGALA, TEMEKE, UBUNGO, ILALA, KARIAKOO, SINZA, MASAKI, KIGAMBONI, MSASANI, TAZARA, TABATA, TEGETA, BUNJU, MOROCO NK. Ni kwa nini haya maeneo yalipewa hayo majina, mwenye historia nzuri ya jiji hili atujuze.

Mkuu shikamooooo
 
Kulikuwa na mzee maarufu akiitwa Musa Hassan, sasa wamakonde walikuwa wanashindwa kumuita ipasavyo wakawa wanamuita NCHA CHANI, kwa hiyo ndo ikatokea hilo jina la MSASANI.

Kama walivyoshindwa Simon Michael badala yake wakatamka Samora Macheli !
 
Nakumbuka Kariakoo ni kutokana na carrier corp, mahali wapagazi wakati wa vita na Magari yalikuwa yanaazia
Kawe kwa sababu ya kiwanda cha kusindika nyama walikuwa na njia ya kupitishia ng'ombe (cow ways)- kawe
Wailesi ndiyo sehemu ambapo mtambo wa simu na waya za polisi na jeshi zilikwepo (wireless)
Chekereni (check train)
Boma - British overseas military administration
Tukumbushane
 
  • Makunduchi, kisiwasi Zanzibar.
  • Kunduchi, Dar es Salaam
  • Mchambawima, kisiwani Zanzibar
  • Kibanda maiti, kisiwani Zanzibar
  • Boko, Dar es Salaam
  • Kawe, Dar es Salaam
  • Gongo la mboto, Dar es salaam
  • Mbeya, Tanzania
  • Iringa, Tanzania
  • Sumbawanga, Tanzania
  • Kiboloroni, Kilimanjaro
  • Rombo, Kilimanjaro

Naomba kwanza nianze na hii michache tu, na si vibaya na wewe ukaongeza na yako unayoijua. Ila nitafurahi kama nitajuzwa kwa hiyo michache niliyoitaja hapo juu.
 
Musoma imetokana na lugha ya kijita "Omusoma " yaani sehemu ya aridhi iliyochongoka kuingia majini.
 
Musoma imetokana na lugha ya kijita "Omusoma " yaani sehemu ya aridhi iliyochongoka kuingia majini.

siyo kwamba neno "musoma" limetokana na kwamba watu wengi wa mkoa wa mara (musoma) ni wasomi na wanapenda mno kusoma na wameelimika?
 
  • makunduchi......kisiwasi zanzibar.
  • kunduchi.........dar es salaam
  • mchambawima.........kisiwani zanzibar
  • kibanda maiti........kisiwani zanzibar
  • boko.......dar es salaam
  • kawe.........dar es salaam
  • gongo la mboto........dar es salaam
  • mbeya.........tanzania
  • iringa...........tanzania
  • sumbawanga.........tanzania
  • kiboloroni.........kilimanjaro
  • rombo............kilimanjaro

naomba kwanza nianze na hii michache tu na si vibaya na wewe ukaongeza na yako unayoijua ila nitafurahi kama nitajuzwa kwa hiyo michache niliyoitaja hapo juu.

Kawe.........dar es salaam.

Zamani kulikuwa na kiwanda cha kusindika nyama TANGANYIKA PEKASI. Sasa ngombe walipitshwa/kuswagwa kuelekea
huko ikaiwa COW WAY, ila kutokana na ugumu wa Lugha hiyo waswahili wanawa wana tamka KAWE
 
siyo kwamba neno "musoma" limetokana na kwamba watu wengi wa mkoa wa mara (musoma) ni wasomi na wanapenda mno kusoma na wameelimika?

Hiyo ni maana ya ziada mkuu!! ila maana ya msingi ni hiyo hapo juu! ila wengi pia wanajua ni kuhusu kusoma lakin pia imesaidia coz watu wa msoma wanasoma sana kukwepa aibu ya kutoka musoma then uwe kilaza!!
 
NJOMBE - Kulikuwa na miti mingi inaitwa midzombe,MAKAMBAKO - Kuna miti mingi katikati ya mji huu mikubwa inaitwa Mikambako (Midume)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom