Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Hii ni ile noah iliyozama ilikuwa na watu sita wawili wamepona, watatu wamepatikana wamefariki, mtoto mmoja hajaonekana sijui kapelekwa na maji hadi wapi
=======
Watu wanne wamepoteza Maisha na wengine wawili kunusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya NOAH T 499 DMY kusombwa na waji katika eneo la Malalula Kata ya King'ori wilayani Arumeru wakitokea Arusha kuelekea Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda amewaambia waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili na dakika arobaini asubuhi wakati dereva wa gari hilo Naimani Metili ambae ndio baba akiwa na abiria watano wakielekea katika mahafali ya mtoto wao Moshi.