Watatu wa familia moja waliofariki mafuriko Arusha kuzikwa Ijumaa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Watu watatu wa familia moja kati ya wanne waliofariki juzi baada ya gari walilokuwa wamepanda kusombwa na mafuriko, akiwemo mama, mtoto na mtoto wa kaka yake, wanatarajiwa kuzikwa Ijumaa Aprili 28, 2023 katika eneo la Ilboru, Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.

Tukio hilo lilitokea jana Aprili 25, 2025 asubuhi katika eneo la King’ori wilayani humo, ambapo mbali na hao waliofariki, wawili walinusurika, wakati tukio hilo lilipotokea wakiwa safarini kwenda Kilimanjaro kwenye mahafali ya kidato cha sita.

Leo Jumatano Aprili 26, 2023 akizungumza na waandishi wa habari msibani hapo, Mwenyekiti wa ukoo na msemaji wa familia hiyo Mchungaji Edgad Metili, alisema waliofariki ni Matha Metili (40) na mtoto wake Lisa Metili (8), Colin Lymo (16) mwanafunzi wa Ilboru, aliyekuwa anakwenda kwenye mahafali ya dada yake Shule ya Sekondari Mwika na jirani yao Brenda Amani (25).

Katika ajali hiyo Anjela Metili (36) aliyekuwa anaenda kwenye mahafali ya mtoto wake, pamoja na kaka yake Naiman Metili aliyekuwa anaendesha gari hilo ndiyo pekee walionusurika kwenye ajali hiyo, ambao bado wanapatiwa matibabu hospitalini.

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa kwani ni msiba mkubwa kwenye familia, haujawahi kutokea msiba wa namna hii, tunamshukuru Mungu ameeendelea kutufariji na ameendelea kufanyika faraja kufanyika serikali kwani wametusaidia kwa kiwango kikubwa tangu tukio lilipotokea,”amesema.

“Tuna misiba mitatu kwenye boma la Metili lakini kuna mwingine ndugu wa karibu hapo boma la chini alikuwa amewasindikiza,” amesema.

"Leo ndiyo tumekaa kikao cha familia na tumepanga tutafanya maziko siku ya ijumaa hapa Kanisa la KKKT Ilboru na wote watatu watazikwa kwenye makaburi ya kanisa, tumepanga kuzika Ijumaa kwa sababu miili itakuwa imeharibika kutokana na maji,” amesema.

Alisema kuwa wamelazimika kuharakisha maziko hayo kwani mwanafunzi aliyekuwa anafuatwa kwenye mahafali hayo anatarajia kuanza mitihani yake Jumatatu ijayo.

Naye mmoja wa wanafamilia hiyo, Joyce Metili amesema kuwa msiba huo umeacha pengo kubwa kwenye familia hiyo.

“Aliyefariki ni mke mwenzangu na mara ya mwisho niliwasiliana naye juzi jioni kabla ya kusafiri na siku hiyo alikuwa na raha sana. Akaniambia nitakupa stori. Saa 11 akanipitia akaniambia anachelewa, akaniambia anakwenda atakuja kunipa stori na jana asubuhi nikaamka nimuage na anieleze alichotaka kusema ila nikakuta wameshaondoka,”amesema

“Tukapigiwa simu tunaambiwa wamepata ajali ya kuchukuliwa na maji, tukapata simu ya watu waliokuwa eneo la tukio, wakasema watu waliopo kwenye gari wote wamekufa tumefanikiwa kupata baba mmoja na mama mmoja, nikawaambia endeleeni kuokoa labda tutapata kwa kweli yule kaka akaniambia hawa waliopo kwenye gari watakuwa wameisha, hapo tulishtuka lakini hapo tulikuwa tunaamini watakuwa salama," amesema.

"Lakini baadaye hawakuwa salama wamepoteza maisha ni msiba mchungu kwangu kwa sababu hapa mke mwenzangu mwingine amefariki nimebaki peke yangu na mama kwenye boma ni msiba mchungu na mzito, nimebaki kama mama,”ameeleza kwa huzuni.

MWANANCHI
 
Itoshe kusema HARAKA HARAKA HAINA BARAKA
Mtu una Noah Gari ipo chinichini eti unamfata Cruiser gari ipo juu juu, matokeo yake ndo hayo wakasombwa na Maji.
Noah ni gari nyepesi kulinganisha na Cruiser. Kama mabasi yalisimama, yeye alitoa wapi ujasiri wa kuvuka?
 
Back
Top Bottom