Ruvuma: Watu 9 wafariki baada ya Gari yao kusombwa na Maji

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
6,116
11,206
IMG_20240312_180119_294.jpg

Watu tisa wamefariki dunia katika kijiji cha Lumeme Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma baada ya gari walilokuwa wanasafiria aina ya Noah lenye namba za usajiri T795 BIS kusombwa na maji kwenye mto Kisimani.

IMG_20240312_180119_505.jpg

Gari hilo lilikuwa limetoka katika kijiji cha Tingi wilayani Nyasa kuelekea kijiji cha Lumeme majira ya saa 12 jioni Machi 11,2024.

Diwani wa Kata ya Lumeme Mheshimiwa Walarick Ndunguru amesema katika ajali hiyo watu wanne wamenusurika huku watu tisa wakipoteza maisha. Diwani huyo amesema ajali hiyo imechangiwa na uzembe wa dereva ambaye alitakiwa kusubiri maji yapungue kwenye kivuko cha Mto Kisimani ndipo avuke.

IMG_20240312_180119_202.jpg

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo kwa niaba ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ametoa pole kwa wafiwa na wananchi wa kata ya Lumeme.

Ametoa rai kwa madereva kuwa makini wanapoendesha vyombo vya usafiri hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika ili kuepusha madhara.

IMG_20240312_180118_621.jpg

Mwakilishi wa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Anselim Chambila amesema watarajia kufanya matengenezo makubwa kwenye kivuko kilichopo katika mto Kisimani mara baada ya kupungua kwa mvua za masika.

1710249126811.jpg

Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma SACP Marco Chilya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

######

WATU 9 WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI YAO KUSOMBWA NA MAJI.

Watu 9 wamekufa Maji baada ya Gari yao aina ya Toyota Noah iliyokuwa ikitokea kijiji cha Tingi kuelekea Kijiji cha Nyoni kusombwa na Maji katika eneo la kijiji cha Lumeme Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akiongea Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chillya, amesema kuwa watu hao walikuwa wakisafiri kwenye Gari aina ya Toyota Noah
yenye namba za Usajili T.770 DBU mali ya John Agaton Kapinga Mkazi wa Kijiji cha Lumecha na kusombwa na Maji baada ya Dereva wake kuchukua uamuzi wa kulazimisha kuvuka katika Daraja hilo la chini ambalo lilikuwa limejaa na kufurika Maji yaendayo kasi.

Kamanda SACP Chillya,
amesema, Dereva huyo ametambulika kwa jina la Edwin Abel Ngowoko (55), ambaye amefariki pamoja na Abiria wake nane baada ya Gari hilo kusombwa na kutumbukia Mtoni kisha kukwama kwenye korongo ndani ya Mto Kisima uliopo Kitongoji cha Lumeme Mpepo Wilayani Nyasa.

Amesema tukio hilo lilitokea Tarehe 11/3/2024 Saa kumi na mbili na nusu jioni ambapo Abiria na Dereva wao walishindwa kujiokoa baada ya nguvu ya Maji kuwashinda na milango kushindwa Kufunguka na wote walipoteza maisha.

Kamanda SACP Chillya amewataja waliofariki na umri wao kuwa, Dereva Edwin Abel Ngowoko (55) Mkazi wa kijiji cha Mbanga, Valeriana Ndunguru (18) Mkazi wa Kijiji cha Mbanga, Innocent Kasian (63) Kijiji cha Mbanga, Saimon Mahai (21) Mkazi wa kijiji cha Kingerikiti, Nathan Kumbulu (39) wa kijiji cha Mbanga, Faraja Daudi Tegete(18) ambaye ni mwanafunzi Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Kilumba Kata ya Lumeme Nyasa.

Pia katika ajali hiyo alifariki mtoto Mwenye umri wa miaka 2 aitwaye Ebiati Daudi Tegete Mkazi wa Kijiji cha Lumeme. Alfonsia Kasian pamoja na Mbele (40) Mkazi wa Kijiji cha Lumecha na Solana Thomas Ndunguru (16) Mkazi wa Mbanga.

Kamanda SACP Chillya amesema Miili ya marehemu Wote imeopolewa na kuhifadhiwa katika Zahanati ya Lumeme Wilayani Nyasa kusubiri Uchunguzi wa Daktari na baadae kuwakabidhi Ndugu kwa mipango ya mazishi.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda SACP Chillya ametoa onyo kwa Madereva Wote wa vyombo vya moto pamoja na watumiaji wengine wa barabara kuacha kabisa tabia za kuyapima maji kwa macho kwani hatari kwa usalama wa maisha yao badala yake amewataka kuhakikisha wanahepuka kuvuka mpaka pale maji yatakapopungua.

Sambamba na hili ametoa pole kwa ndugu jamaa na Wananchi wote Kwa kufikwa msiba huo na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi kigumu wananchopitia wa kuondokewa na wapendwa wao.
 
Gari hilo lilikuwa limetoka katika kijiji cha Tingi wilayani Nyasa kuelekea kijiji cha Lumeme majira ya saa 12 jioni Machi 11,2024 .

Diwani wa Kata ya Lumeme Mheshimiwa Walarick Ndunguru amesema katika ajali hiyo watu wanne wamenusurika huku watu tisa wakipoteza maisha. Diwani huyo amesema ajali hiyo imechangiwa na uzembe wa dereva ambaye alitakiwa kusubiri maji yapungue kwenye kivuko cha Mto Kisimani ndipo avuke.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo kwa niaba ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ametoa pole kwa wafiwa na wananchi wa kata ya Lumeme.

Ametoa rai kwa madereva kuwa makini wanapoendesha vyombo vya usafiri hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika ili kuepusha madhara .

Mwakilishi wa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Anselim Chambila amesema watarajia kufanya matengenezo makubwa kwenye kivuko kilichopo katika mto Kisimani mara baada ya kupungua kwa mvua za masika.
Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma SACP Marco Chilya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

FB_IMG_1710259277732.jpg
 
wajaliwe kupumzika kwa amani.
tahadhari izidi kuchukuliwa dhidi ya vyombo vya usafiri, aheri kukawia kufika kuliko kuwahi ufike kisha usifike salama.
 
Back
Top Bottom