Watatu wa familia moja wafariki kwa kugongwa na gari Arusha wakipeleka mtoto hospitali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
1,006
2,703
Watu watatu wa familia moja akiwemo mtoto mdogo, wakazi wa Kata ya Terat katika Jiji la Arusha wamepoteza maisha papo hapo kwa ajali baada ya kugongwa na gari wakitoka hospitalini wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea mapema leo Julai 13, 2022, majira ya saa 10.45 usiku katika Barabara ya Bypass katika Jiji la Arusha wakati marehemu wakitoka kumpeleka hospitalini, mtoto Ebenezer Mollel mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa ameandikiwa sindano za saa.

Wengine waliofariki dunia ni pamoja na mama wa mtoto, Neema Mollel (27) pamoja na mdogo wake, Agustino Mollel (24) ambaye alikuwa dereva wa pikipiki.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo John Mushi marehemu hao walipoteza maisha eneo la tukio baada ya kupata majeraha makubwa na kuvuja damu nyingi.

Alisema walishuhudia miili ya marehemu hao wakiwa wamevunjika na kusagika mikono na miguu huku mtoto na dereva wakipasuka kichwa na kusagika.

Naye kaka wa marehemu Daud Mollel alisema kuwa marehemu waligongwa kwa nyuma wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki na gari ambalo halikujulikana baada ya kutosimama katika eneo la Karvati, Terat.

Alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa juu ya ajali hiyo alifika eneo la tukio na kushuhudia miili ya marehemu wakiwa ikiwa na majeraha makubwa sehemu mbalimbali za miili yao.


Chanzo: Malunde
 

Saint Anno II

JF-Expert Member
Sep 12, 2021
1,295
4,259
Mungu azirehemu roho za marehemu wapate pumziko la milele.

Pikipiki kama mtu una uwezo wa kuiepuka acha usipande ni usafiri hatari sana maana kwanza wote wenye pikipiki Boxer au TVS hata kama ya kwako ni private madereva wa magari wa kibongo wanaona wote wale wale tu wote bodaboda.

Ukiwa na pikipiki kubwa zile Honda XR au hizi BMWs naziona sana mitaani siku hizi hapo ndo utaonekana mtu otherwise wewe yako lami tu then haters ni hawa wenye IST na Paso in short madereva wenye stress ndo wanaouwa sana barabarani.
 

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
5,164
2,904
Ni wiki Mbaya...Watu Nane wamekufa kule Bukoba Kwa Ajali Watano wakiwa ndugu Familia Moja, Kuna Wanne Wamefariki Kwa Ajali huko Simiyu, Kuna Mjeshi Mstaafu ameua DSM Kwa ugomvi wa' Shamba, Kisha Hawa Wa familia Moja Arusha!

Ni wiki ya Majonzi...R.I.P Marehemu Wote...
 

Marathon day

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
324
423
Wangefanya kama Nairobi bodaboda, bajaji, mikokoteni, guta , marufuku barabara kubwa.
Umenitoa tongotongo, sikujua hili kabla, na sisi kwakweli tujifunze Toka huko, ajali za pikpki zimekuwa nyingi na za kutisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Top Bottom