Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Nyinyi wananchi mlikubali vipi muongozwe na kichaa, au na nyinyi ni vichaa?
Magufuli alikataliwa. Na yeye alijua hilo. Ndio maana pamoja na kufanya mengi, bado alihitaji kupora uchaguzi. Ndio maana hakutaka uhuru wa habari, ndio maana alipiga vita Demokrasia
 
Hicho mnachokiita demokrasia , matokeo yake ndio zile fujo za South Africa, nyie demokrasi ya makelele haiwafai
 
Kilicho muhimu ni kwamba Diallo ameuelezea utawala wa awamu iliyopita katika uhalisia wake.

Tatizo la afya ya akili ya marehemu ni dhahiri, na wengi walikuwa wanajua. Juu ya yeye kutibiwa Mirembe na Ujerumani, inafahamika. Lakini kwaajili ya heshima ya mgonjwa, miiko ya kitabibu inasema ugonjwa ni siri ya mgonjwa. Hata hivyo illikuwa siyo sahihi mtu mnayefahamu ana tatizo linaloweza kuleta madhara makubwa kwa Taifa na wananchi, mkampa nafasi ya uongozi wa juu kabisa.
Nafurahia kuona CHADEMA wanavyowashabikia wana CCM.
 
Hicho mnachokiita demokrasia , matokeo yake ndio zile fujo za South Africa, nyie demokrasi ya makelele haiwafai
Tatizo Afrika Kusini siyo Demokrasia. Kwa wenzetu, rais mstaafu ana HAKI ya kufungwa jela. Kwetu rais mstaafu hana HAKI hiyo.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, bwana Anthony Diallo amewaomba radhi watanzania kwa kauli zake alizozitoa kuwa viongozi wa Serikali waliopita walikuwa na mafaili mirembe.
View attachment 1849688

========

Diallo: Mimi nadhani ufafanuzi unatosha, nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya, kuna kunielewa nilivyomaanisha lakini kuna kunielewa vibaya mtu mwingine akaona nimeleta ukakasi, hiyo ni nature ya binadamu inaweza kutokea kwamba naweza kuelewa kidogo au tofauti na aliyesema.

Mtu anaetafsiri uelewa ni yule anayesikiliza kulingana na principle ya communications, mara nyingi inatokea mtu anaweza akakuelewa vibaya, katika muktadha wa aina hiyo mimi sina shida ya kusema wanisamehe kwasababu nimewapa uelewa ambao sivyo walivyotarajia

Kuhusu akaunti ya mtandao ni Akaunti feki, hiyo post nimeiona sio mimi.

=======

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dkt. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dkt. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dkt. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dkt. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Mwanahalisi

Zaidi, soma: Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?
Wewe jiuzulu tu, mchumia tumbo mkubwa. Mbona hayo maoni yako hukusema akipokuwepo?. Na kwenye mikutano yake yote hapo mwanza ulikuwa ukipata nafasi unamsifia leo hayupo unaponda. Mnafiki mkubwa.
 
Ukitaka kujua kuwa CCM Ni manafiki sikiliza mazungumzo yake yote halafu ujiulize huyu ndiye kichaa au wale aliowasema!
 
CHADEMA mmebaki kuwa wacheza Ngoma za CCM tu kwa sasa, hakuna operation haki, maandamano Wala wabunge wa covid 19, kila sehemu mnaangukia pua.
Mchukueni sasa huyo Dialo wenu
Hatuwashangai maana mliongozwa na kichaa nyie
 
Kufungwa sio HAKI

Rekebisha maelezo yako
Kwa kweli tunawakosea HAKI marais wetu, kwa kuwanyima HAKI ya kushitakiwa na hata kufungwa jela. Nchi nyingine wana haki hizo. Hata Israel mkuu wa serikali alifunguliwa mashitaka akiwa madarakani
 
Magufuli alikataliwa. Na yeye alijua hilo. Ndio maana pamoja na kufanya mengi, bado alihitaji kupora uchaguzi. Ndio maana hakutaka uhuru wa habari, ndio maana alipiga vita Demokrasia
Nitajie nchi moja tu iliyopiga hatua katika maendeleo kwa kutumia demokrasia
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, bwana Anthony Diallo amewaomba radhi watanzania kwa kauli zake alizozitoa kuwa viongozi wa Serikali waliopita walikuwa na mafaili mirembe.
View attachment 1849688

========

Diallo: Mimi nadhani ufafanuzi unatosha, nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya, kuna kunielewa nilivyomaanisha lakini kuna kunielewa vibaya mtu mwingine akaona nimeleta ukakasi, hiyo ni nature ya binadamu inaweza kutokea kwamba naweza kuelewa kidogo au tofauti na aliyesema.

Mtu anaetafsiri uelewa ni yule anayesikiliza kulingana na principle ya communications, mara nyingi inatokea mtu anaweza akakuelewa vibaya, katika muktadha wa aina hiyo mimi sina shida ya kusema wanisamehe kwasababu nimewapa uelewa ambao sivyo walivyotarajia

Kuhusu akaunti ya mtandao ni Akaunti feki, hiyo post nimeiona sio mimi.

=======

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dkt. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dkt. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dkt. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dkt. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Mwanahalisi

Zaidi, soma: Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?
Alichoongea Diali ni ukweli mtupu, hii kuomba radhi ni kufunika kombe wanaharamu wapite
 
Back
Top Bottom