Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
46,835
2,000
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr. Anthony Diallo kwamba alikuwa na jalada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Nawasalimu kwa jina la JMT!

=========
KWA UFUPI

Mahojiano kati ya Mhe Anthony Diallo Mwenyejiti wa CCM Mkoa wa Mwanza na Mtozi Alloyce Nyanda

1. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Biashara yetu ya Star Tv, RFA iliharibika -Diallo

2. Sie hatukulipwa na CCM, waliolipwa ni Crew iliyokuwa inatembea na vifaa kama majukwaa, walipewa hela ya kula na kubeba vifaa, ukitazama vitabu vyetu kuna hela chama hadi leo haijalipa-Diallo Mwenyekiti wa CCM

3. Mgombea wetu wa wakati ule alisema atatusaidia na alisema hadharani tena mara mbili pale Kirumba na furahisha lakini tuliambulia misukosuko

4. Awamu ya 5 iliharibu sana protocal ya Chama, viongozi wa chama walikuwa wanawekwa mstari wa nyuma kabisa gari zinakuwa mwisho hata kama ukifika unakuta mtu amekata utepe-Anthony Diallo mwenyekiti wa CCM

5. Kuna kisa kimoja kiongozi wa CCM mkoa wakati flani tumeenda kumpokea Rais alipigwa kiwiko akadondondoka, awamu ya Tano ilikuwa inazuia viongozi wa CCM hata kuingia uwanja wa ndege wanaelezwa kubaki nje -Antony Diallo Mwenyekiti wa CCM

6. Kuna siku nimemwambia waziri mkuu, hivi unajisikia raha gani kuzungukwa na mabunduki maana umezungukwa na mabunduki kama ishirini sie, tumekuchagua ila unatuogopa ki vipi? -Antony Diallo

7. Swala hapa siyo katiba, swala ni kuchagua watu makini. Unawezaje kuchagua kiongozi katika nafasi kubwa ya uongozi huku ana rekodi ya mirembe? Tuwe makini kuchagua viongozi-Anthony Diallo

8. Kama nchi tumepitia katika kiza kifupi, tumepitishwa katika Black spot hapo Nyuma, Sasa angalau watu wana raha, furaha imerejea-Dkt Anthony Diallo

9. Hata mimi Nimeshughulikiwa kidogo, wakaniacha ila nimepata msukosuko-Anthony Diallo

10. katiba siyi ya Vyama ni ya wananchi kosa tulilofanya ni kugeuza katiba kuwa vyama na kuacha wananchi hata katika lile
bunge walitawala wananchi-Dk Anthony Diallo

11. Katiba siyo Tatizo , tatizo lipo kwa watu mnachagua Rais ambae hataki kufata katiba mtanfanya nini? Kwani katiba ya sasa ilikuwa inaruhusu mtu kuwekwa ndani bila utaratibu? Lakini yamefanyika-Anthony Mwandu Diallo

12. Rais Samia nimefanya nae kazi ni Rais makini na jasiri ni muumini wa utawala wa bora-Anthony Diallo

13. CCM tulijua haitashinda mwaka 2015 na wananchi wamegeuka wiki mbili tu baada ya kuamua hata kuunda makundi ya vijana kwenye maeneo mbali mbali waweke Star Tv ilibidi itumike nguvu

15. Kuna mambo hatukuweza kuyasema kwa sababu mfumo uliharibika kabisa. Tuliamua kunyamaza tuliamua ku play safe mode ili kesho uendelee kuishi na watoto wako.

Zaidi, soma; Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,466
2,000
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr Anthony Diallo kwamba alikuwa na jarada hospitali ya Mirembe ni nani?
Ameanza kwa kusema kabla watu HAWAJAPEWA madaraka makubwa kama urais tuwe tunatafuta na historia zao kwanza. Akamaliza kwa kusema Sasa hivi watu wamepumua kabisa.

Akashangaa kwa kusema mwekezaji gani angeweza kuja wakati anaona kwa mwekezaji mwenzake "Lisu" anakuja na makufuli kufunga biashara yake??!!!

"Lisu" huyu amemtesa Sana mzee Diallo
 

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
5,515
2,000
Usijifanye kichaa. Ni yule kichaa aliyekuwa Ikulu. Akikana kuwa Tanzania kuna corona. Yaani hakuwa na akili hata ndogo ya kujua kuwa kuna corona Tanzania!!
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr Anthony Diallo kwamba alikuwa na jarada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Je, ni TAL wa Chadema?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,466
2,000
Ameulizwa mzee mbona hata ziara za "Lisu" ulikuwa huonekani kuhudhuria?

Mzee Diallo akajibu "Lisu alivuruga pritokali". Viongozi wa chama tukawa tunasukumwa mpk wengine wanaanguka hovyo. Ni kana kwamba sisi viongozi wa chama tulikuwa tishio kwa usalama wake
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,366
2,000
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr Anthony Diallo kwamba alikuwa na jarada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Je, ni TAL wa Chadema?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Huyu Tundu Lissu sijui ndiye aliyewatoa usichana wenu maana kila anayekurupuka kutoka usingizini lazima amuanzishie uzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom