Kuna hofu gani ndani ya CCM? Hizi kauli zinaashiria mpasuko au mmeguko?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Habari za muda huu ndugu yangu

Huwa sina mtiririko mzuri wa kiuandishi, lakini napenda kujenga hoja kwa ufupi huku ikifuatiwa na maelezo mareeefu.

Kauli ya Katibu Mkuu mpya wa Chama Dkt. Emmanuel Nchimbi kwamba "Utamaduni wa CCM ni Rais wa JMT kuhudumu kwa Mihula miwili hivyo nawaambieni Mapema kabisa tusije kuzinguana huko mbele ya safari, amesisitiza Dr Nchimbi' ni mwendelezo wa kauli za viongozi wa juu wa chama ambao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Bara kuwa fomu ya mgombea urais itatoka moja tu.... na viongozi wengine wamefuata mkumbu huo huo wa kauli zinazofanana kuelekea mchakato wa kupata mgombea wa urais ndani ya CCM

Mwaka jana niliweka bandiko nikielezea namna ambavyo Muumba ameikataa CCM na sasa ameondoa kauli kwenye ndimi zao, hivyo kila wanachokiongea ni kama wanajidhalilisha. Sote tunafahamu kuwa chama kikichukua madaraka kwa njia halali au haramu kama inavyofanya CCM siku zote, basi wanapaswa kusimamia muktadha mzima wa maendeleo mtambuka ya nchi. Ulinzi, Usalama na Ukuaji Uchumi ni jambo ambalo linapambaniwa kupitia sera mbalimbali za vyama shindani.

Nchimbi amekuja na kauli hiyo ambapo kwa sisi wafia chama tulitarajia kupata kauli inayoponya majeraha yaliyosababishwa na michakato ya chaguzi ndani ya vyama. Lakini bila aibu Katibu Mkuu mpya anatoa kauli ya kwanza nzito kuelekea uchaguzi huku akianza kampeni hata kabla Tume ya Uchaguzi haijatangaza kuanza kwa mchakato.

Kuna maswali yanaibuka hapa
  1. Je, sasa ni rasmi kwamba CCM imeshaanza kumeguka?
  2. Je mpasuko wa ndani ya chama umekuwa dhahiri?
  3. Je siasa za makundi na kambi ndani ya CCM zimeanza kuleta athari chanya kwa ukombozi wa nchi?
  4. Je, Katibu Mkuu mpya anajikomba au kudivert mada ionekanike yupo makini ilihali anajua kabisa kuwa mgombea wao ambaye ni incumbert hakubaliki kwa wapigakura?
Mpasuko wowote ndani ya CCM ni dalili njema kwa nchi
 
.

Hakuna mpasuko wowote CCM, kauli ya KM ni kukumbushia tuu utaratibu wa kawaida wa CCM, incumbent huwa hapingwi anapitishwa kwa mserereko!.

Sii kweli kuwa Rais Samia hakubaliki, kwa the political dynamics ya siasa zetu, sheria batili za uchaguzi wetu, time yetu ya uchaguzi, uwanja tenge wa the political landscape of Tanzania, mgombea yeyote wa urais wa CCM, ndiye rais wa Tanzania!.

Hata hivyo ikitokea Rais Samia asisimame 2025, sababu itakuwa ni sauti HII !.
P
 
Sii kweli kuwa Rais Samia hakubaliki, kwa the political dynamics ya siasa zetu, sheria batili za uchaguzi wetu, time yetu ya
Mkuu
Inaelekea huko kukumbushia ni dalili kuna mbinumbinu ambazo zinaendelea ndo maana akili kubwa zinatumika sasa kwenye political setup ili kuokoa jahazi linaloyumba kuekekea kwenye jabali.

Hivi sasa tunachokiona ni kwamba kipaumbele kikuu si utekelezaji wa ilani bali kampeni za wazi kwa uchaguzi ujao.

CCM inatumiwa na dola kutawala nchi. Nilidhani CCM inaitumia dola
 
Kama haya ya CCM ni kweli, na yale ya wana CHADEMA (Team Maridhiano vs Team Sanuka) ni ya kweli, kuhusu migawanyiko na mipasuko ndani ya korido zao za siasa, basi upo umuhimu wa UMOJA party isajiliwe, ianze shughuli ili ije kuokoa "Jahazi".

Umoja Party ichukue fursa hii pronto.

Bye bye CHADEMA bye bye CCM.
 
Hakuna mpasuko wowote CCM, kauli ya KM ni kukumbushia tuu utaratibu wa kawaida wa CCM, incumbent huwa hapingwi anapitishwa kwa mserereko!.

Sii kweli kuwa Rais Samia hakubaliki, kwa the political dynamics ya siasa zetu, sheria batili za uchaguzi wetu, time yetu ya uchaguzi, uwanja tenge wa the political landscape of Tanzania, mgombea yeyote wa urais wa CCM, ndiye rais wa Tanzania!.

Hata hivyo ikitokea Rais Samia asisimame 2025, sababu itakuwa ni sauti HII !.
P
Kumbe ndani ya ccm kila aliyepo lazima anakubalika, na ikiwa hakubaliki anaweza kujiuzulu au itabidi wasiomkubali ndio wamezee tu?

Umenifurahisha sana , nakubaliana nwe ccm huwa hakuna mpasuko wala makundi, wao ni wamoja muda wote. Na incumbent huwa anaendelea tu na hakuna wa kushindana naye.

Ila ccm huwa hawataji KATIBA huwa wanataja ILANI. wanasema ilani yetu inasema..., na tunatekeleza. Uwanja tenge wenu, mgombea wenu, uchaguzi wenu, kwanini asishinde?

Sasa hivi viongozi wa CCM wanjitahidi kuwashawishi CHADEMA washiriki uchaguzi hata kwa kuwahonga.

Na chadema walivyo wajinga watakubali. Binafsi ningeungana na wanaosema HAKUNA KUSHIRIKI UCHAGUZI WOWOTE BILA KATIBA MPYA.

Kwasababu wameshiriki sana na matokeo wanayajua, na HAKUNA kitakachobadirika, kwasababu uchaguzi huu na zilizopita hakuna tofauti, mazingira ni yale yale kwanini washiriki?
 
Kwa nini chadema wasikubali mdahalo bila masharti ili amwulize makonda
…kuhusu yale yaliyotokea dodoma kuhusu Lisu

Kuhusu beni sanane
Maana cdm amekuwa wakimtuhumu kuwa anahusika
 
Habari za muda huu ndugu yangu

Huwa sina mtiririko mzuri wa kiuandishi, lakini napenda kujenga hoja kwa ufupi huku ikifuatiwa na maelezo mareeefu.

Kauli ya Katibu Mkuu mpya wa Chama Dkt. Emmanuel Nchimbi kwamba "Utamaduni wa CCM ni Rais wa JMT kuhudumu kwa Mihula miwili hivyo nawaambieni Mapema kabisa tusije kuzinguana huko mbele ya safari, amesisitiza Dr Nchimbi' ni mwendelezo wa kauli za viongozi wa juu wa chama ambao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Bara kuwa fomu ya mgombea urais itatoka moja tu.... na viongozi wengine wamefuata mkumbu huo huo wa kauli zinazofanana kuelekea mchakato wa kupata mgombea wa urais ndani ya CCM

Mwaka jana niliweka bandiko nikielezea namna ambavyo Muumba ameikataa CCM na sasa ameondoa kauli kwenye ndimi zao, hivyo kila wanachokiongea ni kama wanajidhalilisha. Sote tunafahamu kuwa chama kikichukua madaraka kwa njia halali au haramu kama inavyofanya CCM siku zote, basi wanapaswa kusimamia muktadha mzima wa maendeleo mtambuka ya nchi. Ulinzi, Usalama na Ukuaji Uchumi ni jambo ambalo linapambaniwa kupitia sera mbalimbali za vyama shindani.

Nchimbi amekuja na kauli hiyo ambapo kwa sisi wafia chama tulitarajia kupata kauli inayoponya majeraha yaliyosababishwa na michakato ya chaguzi ndani ya vyama. Lakini bila aibu Katibu Mkuu mpya anatoa kauli ya kwanza nzito kuelekea uchaguzi huku akianza kampeni hata kabla Tume ya Uchaguzi haijatangaza kuanza kwa mchakato.

Kuna maswali yanaibuka hapa
  1. Je, sasa ni rasmi kwamba CCM imeshaanza kumeguka?
  2. Je mpasuko wa ndani ya chama umekuwa dhahiri?
  3. Je siasa za makundi na kambi ndani ya CCM zimeanza kuleta athari chanya kwa ukombozi wa nchi?
  4. Je, Katibu Mkuu mpya anajikomba au kudivert mada ionekanike yupo makini ilihali anajua kabisa kuwa mgombea wao ambaye ni incumbert hakubaliki kwa wapigakura?
Mpasuko wowote ndani ya CCM ni dalili njema kwa nchi
Kweli Huna mtiririko mzuri wa uandishi… na hoja pia
 
Ila wa Tz asee
Katba ya ccmu inaruhusu mwanacham kuchukua fomu ya urais na akachuan nae ambae ameshaongoz kwa term moja

Hayo wanayoongea nn
Mcc kam wao hawawez cmamia katb yao ya mcc watawez simamia katba ya Nchi
 
Washazoea kuvunja katiba ya nchi, hata yao wanaikiuka
 
Habari za muda huu ndugu yangu

Huwa sina mtiririko mzuri wa kiuandishi, lakini napenda kujenga hoja kwa ufupi huku ikifuatiwa na maelezo mareeefu.

Kauli ya Katibu Mkuu mpya wa Chama Dkt. Emmanuel Nchimbi kwamba "Utamaduni wa CCM ni Rais wa JMT kuhudumu kwa Mihula miwili hivyo nawaambieni Mapema kabisa tusije kuzinguana huko mbele ya safari, amesisitiza Dr Nchimbi' ni mwendelezo wa kauli za viongozi wa juu wa chama ambao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Bara kuwa fomu ya mgombea urais itatoka moja tu.... na viongozi wengine wamefuata mkumbu huo huo wa kauli zinazofanana kuelekea mchakato wa kupata mgombea wa urais ndani ya CCM

Mwaka jana niliweka bandiko nikielezea namna ambavyo Muumba ameikataa CCM na sasa ameondoa kauli kwenye ndimi zao, hivyo kila wanachokiongea ni kama wanajidhalilisha. Sote tunafahamu kuwa chama kikichukua madaraka kwa njia halali au haramu kama inavyofanya CCM siku zote, basi wanapaswa kusimamia muktadha mzima wa maendeleo mtambuka ya nchi. Ulinzi, Usalama na Ukuaji Uchumi ni jambo ambalo linapambaniwa kupitia sera mbalimbali za vyama shindani.

Nchimbi amekuja na kauli hiyo ambapo kwa sisi wafia chama tulitarajia kupata kauli inayoponya majeraha yaliyosababishwa na michakato ya chaguzi ndani ya vyama. Lakini bila aibu Katibu Mkuu mpya anatoa kauli ya kwanza nzito kuelekea uchaguzi huku akianza kampeni hata kabla Tume ya Uchaguzi haijatangaza kuanza kwa mchakato.

Kuna maswali yanaibuka hapa
  1. Je, sasa ni rasmi kwamba CCM imeshaanza kumeguka?
  2. Je mpasuko wa ndani ya chama umekuwa dhahiri?
  3. Je siasa za makundi na kambi ndani ya CCM zimeanza kuleta athari chanya kwa ukombozi wa nchi?
  4. Je, Katibu Mkuu mpya anajikomba au kudivert mada ionekanike yupo makini ilihali anajua kabisa kuwa mgombea wao ambaye ni incumbert hakubaliki kwa wapigakura?
Mpasuko wowote ndani ya CCM ni dalili njema kwa nchi
Tukiwa jeshini tulifundishwa kuwa mkiwa kwenye uwanja wa vita, hata kama mambo ni magumu, kwa maana ya kuelemewa na adui, wewe kiongozi usiwaambie wapiganaji kuwa mambo ni magumu sana, utawavunja moyo wapiganaji. Unatakiwa utoe kauli za kuwapa morali, kama vile, kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba askari wa adui hawana chakula, ammunitions zimewaashia, wana ugomvi wenyewe kwa wenyewe, mambo yanayotupa urahisi wa kuwamaliza maadui na kushinda vita. Halafu atamalizia kwa kusema kuwa, endapo mimi kamanda nitauawa, msaidizi wangu atachukua nafasi kuendeleza mapigano. Lakini kiuhalisia, ukisikia kamanda kila mara anarudia kusema kuwa yeye akiuawa, msaidizi wake atachukua nafasi, na endapo msaidizi wake naye akiuawa askari fulani atachukua nafasi yake, unatakiwa ujue kuwa hali ni ngumu. Wala usisikilize zile hadithi za mwanzo kama zile za kusema sijui adui hana chakula n.k.
 
Kama wanashindwa kua na demokrasia kwenye chama Chao watawezaje kuleta demokrasia kwenye nchi nzima 🤔🤔 nilidhani yule mzee atakua na busara angalau ya maneno tuu lakini ni wazi nilisahau kama wajinga na wapumbavu wanazeeka pia, Chawa pro max
 
Kwa nini chadema wasikubali mdahalo bila masharti ili amwulize makonda
…kuhusu yale yaliyotokea dodoma kuhusu Lisu

Kuhusu beni sanane
Maana cdm amekuwa wakimtuhumu kuwa anahusika

..Makonda ni muoga.

..Hakuwa na dhamira ya dhati na huo mdahalo.

..Yeye Makonda si alisema hana masharti, anataka mdahalo na yeyote, mahali popote.
 
Back
Top Bottom