Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Acheni kutafuta umaarufu kwa kudanganya wapuuzi wenzenu. He was a hero and always will be! Hata Nyerere alipotoka madarakani wengi aliowabana kwa ufisadi wao walimnanga pia.
Piga ua Magufuli na Nyerere watakumbukwa daima.
Hero wa kubumba? Labda zero, nachojua mimi hakuna Rais wa hovyo kama Magufuli
 
Kwa nini unafuatilia upuuzi?😝😝😝
Hebu jaribu kufuatilia mambo, usiwe na kumbukumbu kama za kuku maana ana kaubongo Kadogo kiasi anasahau haraka. Kumbuka mimi nilitoa maoni yangu wewe ukajibu upuuzi. Au ulitamani nikuache uholohoje tu. Kama ndivyo unapenda, sitakujibu tena
 
Hebu jaribu kufuatilia mambo, usiwe na kumbukumbu kama za kuku maana ana kaubongo Kadogo kiasi anasahau haraka. Kumbuka mimi nilitoa maoni yangu wewe ukajibu upuuzi. Au ulitamani nikuache uholohoje tu. Kama ndivyo unapenda, sitakujibu tena
Ukiona mtu ni Mpuuzi unapaswa umuache.Kama unaendelea kumjibu mpuuzi unaonekana unawashwawashwa mapaja.Hakuna raha njema kama mpuuzi kujibu upuuzi.😝😝😝😝😝
 
Acheni kutafuta umaarufu kwa kudanganya wapuuzi wenzenu. He was a hero and always will be! Hata Nyerere alipotoka madarakani wengi aliowabana kwa ufisadi wao walimnanga pia.
Piga ua Magufuli na Nyerere watakumbukwa daima.
He was a hero kwa vichaa wenzake kama wewe.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, bwana Anthony Diallo amewaomba radhi watanzania kwa kauli zake alizozitoa kuwa viongozi wa Serikali waliopita walikuwa na mafaili mirembe.
View attachment 1849688

========

Diallo: Mimi nadhani ufafanuzi unatosha, nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya, kuna kunielewa nilivyomaanisha lakini kuna kunielewa vibaya mtu mwingine akaona nimeleta ukakasi, hiyo ni nature ya binadamu inaweza kutokea kwamba naweza kuelewa kidogo au tofauti na aliyesema.

Mtu anaetafsiri uelewa ni yule anayesikiliza kulingana na principle ya communications, mara nyingi inatokea mtu anaweza akakuelewa vibaya, katika muktadha wa aina hiyo mimi sina shida ya kusema wanisamehe kwasababu nimewapa uelewa ambao sivyo walivyotarajia

Kuhusu akaunti ya mtandao ni Akaunti feki, hiyo post nimeiona sio mimi.

=======

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi β€˜kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dkt. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dkt. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna β€˜track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa β€˜milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema β€œnilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema β€œmimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dkt. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

β€œUnakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dkt. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na β€œchama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

β€œChama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema β€œkama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Mwanahalisi

Zaidi, soma: Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?
Hivi Diallo alitoka Mirembe mwaka gani?
 
Wanufaika wake uwaambii kitu.
Leo musiba hawezi hata kulipa mishahara wafanyakazi wake.Unadhani anafurahi mtoa riziki wake akisemwa ukweli
Mbona mbowe alishindwa kulipa mshahara kwenye gazeti lake la Tanzania daima
 
Back
Top Bottom