Kada wa CCM awavaa viongozi wala rushwa atoa msimamo mzito 2024

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
VIONGOZI WALA RUSHWA BAADHI KWA NJAA ZAO WANAJITOA UFAHAMU NA KUSIMAMA HADHARANI KUPOTOSHA KAULI ZA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA TUWAONYE WAACHE UJINGA .

Nilisikika nikiunguruma katika Ulimwengu wa kiroho huko Ndotoni kukemea Ujinga wa kupenda Rushwa Kisha watu kujitoa ufahamu kutetea maovu hadharani. Nikaanza kuupeleka Moto kuelekea kwao hao wanafiki baadhi Nakumbuka July 2020 Katika Uwanja wa Uhuru Hayati Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alisema
Wakati tunazaliwa huwa tunalia wakati watu waliotuzunguka wakifurahi.

Kwa hiyo tunatakiwa tuishi vizuri ili siku tukifariki sisi tufurahi Wakati Dunia na watu wengine wanaotuzunguka au kutufahamu watulilie Mwisho wa kunukuu. Kuna Baadhi ya Viongozi wakifa watu Walio wengi hawasikitiki kutokana na Matendo Yao ya hovyo yanayo onyesha kuwapendelea Baadhi ya watu na kutumia nguvu kadhaa kuwadhoofisha wanaojiinua kuipigania haki.

Tumekubaliana ndani ya nchi Chama kinachounda Serikali ni lazima nacho kiwe na uadilifu. Ni lazima wote tuwe chini ya Sheria kusiwepo watu wanaotengenezewa mazingira ya kuonekana very special.Wabunge Madiwani Na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni watu wanao watumikia watu wanaotokana na watu wale wale waliokula viapo kulinda, kuhifadhi na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zote za nchi kwa mujibu wa ibara 26(2) ikisomwa kwa Pamoja na ibara 09 a b f na h kwa kuizingatia ilani ya CCM 2020 uk 01 ibara 04.

Kinachotakiwa Sisi Kama Chama tuwe na Masikiio ya kusikiliza watu Walio wengi tunao watumikia kusikia wanalalamikia Nini .Tusimamie watu wasifanye kampein mapema kwa mujibu wa taratibu .
Ila suala la kukemea kukosoa na kuyaanika maovu ni lazima liwe endelevu na ndilo litakalo imarisha umoja amani na Mshikamano na kuondoa vitabia vya Baadhi ya watu kujiona Vijimiungu watu wasio semwa Wala kuguswa.

Ni lazima tuirudie ibara yote ya nane ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuiishi ili kuacha kutoa matamshi yenye viashiria vya vitisho vinavyolenga kuwaziba midomo Raia wasianike Mauozo ya Baadhi ya Wabunge Madiwani Na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa. Nakumbuka Tarehe 28/10/2021 Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Katika hafla ya Uzinduzi wa kitabu kiitwacho Tanzania Gender Bench Book on Women's Rights Alisema Ibara ya 12 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka bayana kwamba Binaadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa na kwamba Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

Pamoja na usawa wa kuzaliwa, pia ibara 13(1) ya katiba yetu inatambuwa kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria. Hiyo ni katiba yetu. Mwisho wa kunukuu

Katiba hii inakataza vitisho na upendeleo ibara 09(h) Tujiepushe na Matumizi maovu ya vyeo ya kusimama hadharani kuwatisha watu ili hata yule Kiongozi aliyechokwa na watu wasianikwe maovu yake ili hata chaguzi zijazo apitishwe Tena kwa Rushwa azidi kuwaonea Raia kwa tamaa zake za ubinafsi uliopituka mipaka.

Nilichobaini tuna Viongozi wengi baadhi hawana Elimu ya kuwatosha kuhusu Mifumo ya nchi Ndiyo maana wanaonekana vituko wakitoa matamko yanayokinzana na viapo vyao Ipo haja ya kuendelea kuwaelimisha kupitia Mitandao ya kijamii ili wakawe Viongozi wenye kuyaishi Matazamio ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia anayependa kuona watu wote wakiwa na furaha ndani ya nchi Yao.Nakumbuka Tarehe 24/11/2021
Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi Akifanya Mahojiano na ITV Alisema Elimu ni kitu muhimu Sana katika Maendeleo ya nchi yeyote.Mwisho wa kunukuu Tusikubali kuzibwa midomo kwa kutishiwa na Baadhi ya kauli za Viongozi wasio na Elimu wanaopotosha maagizo ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa .Tusiwachekeee kabisa

Sisi tukiona Kiongozi anapotoka ni lazima tuseme Haki ya kusema ni haki ya Kila Mtanzania.
Kutoa matamko ya kutisha na kuwaziba midomo wanyonge sio utu ni unyama unakinzana na matakwa ya katiba Dkt Philip Isdor Nzabayanga Mpango Makamu wa Rais wa Tanzania Nakumbuka Tarehe 08 /12/2023 Alisema Baba wa Taifa (Mwl Julius Kambarage Nyerere na ) Hayati Abeid Amani Karume Ndiyo Taifa walilolijenga Taifa linalo thamini utu Taifa linalo simamia haki ya Kila mtu. Ni Jambo la Muhimu saana.
Mwisho wa kunukuu Tuisimamie haki ya kikatiba ya Kila mtu kusema ili kuvunja cheni ya watu waovu wanaojaribu hata kuteteana kwenye maovu Kinyume na viapo vyao vya kiuongozi.

Nakumbuka Tarehe 27/10/2023 Mheshimiwa Kasimu Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa TanzaniaAkishiriki Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama Cha Management ya kumbukumbu na nyaraka Tanzania
Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema Nataka niwaambie kwa kauli ya Viongozi wetu (yaani Dkt Samia, Dkt Mpango na Dkt Mwinyi) Changamoto mtakazokuwa mnaziibua Tutazifanyia kazi. Mwisho wa kunukuu

Mheshimiwa Waziri Mkuu Changamoto Ndiyo hizo Viongozi Baadhi wa Chama na Serikali wanatoa matamko ya Vitisho kuwafanya mafukara wafyate ili wale Viongozi waovu wawalindie nafasi za kuendelea kuwaongoza wananchi ambao kimsingi wananchi hao wameisha watapika hao Baadhi wanaotetewa kwa vile hawana lengo la kuwasaidia wananchi Zaidi ya kutumia vyeo walivyo navyo kujinufaisha wao na hao wanao wakingia kifua ili maovu yao yafichwe.

Mheshimiwa Dkt Dotto Mashaka Biteko Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati
Akifunga Baraza la Vyama vya Siasa Tarehe 04/01/2024 Alisema Nataka niwahakikishie
Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Makamu wake Dkt Isdor Philip (Nzabayanga) Mpango Na Waziri Mkuu wake Mheshimiwa Kasimu Majaliwa Majaliwa Maelekezo Yao kwetu Sisi tulio wadogo huku (ngazi zilizo chini yao ) ni kwamba tuwafanye Watanzania wawe wenye furaha.

Wawe wenye furaha kweli kweli kwa sababu Wanasikilizwa kwenye nchi Yao
(Wananchi woote) wajuwe wanaongozwa kwa namna gani Na mwisho wa siku (wananchi Hawa) wajenge Taifa lililo Bora Zaidi. Mwisho wa kunukuu Taifa litajengwa na watu wakweli waliojitoa kuisaka haki.

Tuwape ushirikiano Viongozi wote wenye kuviishi viapo na kufuata maelekezo Chanya ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa huku tukiwaanika Viongozi waovu kwa kupaza Sauti na kuyaanika Mauozo Yao wanayotamani yasijulikane ndani ya jamii ili wazidi kuishi kwa hila na ulaghai wakiwanyonya mafukara kwa kuwaonyesha meno meupe yasiyo somana na itikadi za mioyo Yao miovu iliyojificha kwenye kutamka neno Mwenyezi Mungu huku Matendo na Mienendo yao ikiwa haina Mungu kabisa .

Nikashtuka Ndotoni katika Ulimwengu wa kiroho huku macho yakiwa yamegoma kufumba.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mathias Mugerwa Kahinga
+255786596782
 
Bangi za MK hizi, anayechukia rushwa hawezi kubali CCM.
 
Kwamba ulikemea RUSHWA ndotoni!!

Nenda sasa ukawambie CCM wenzio wasiibe tena uchaguzi live.

Wakubali Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Fanya hivyo haraka.
 
Back
Top Bottom