Katibu wa ADC: Kauli ya Paul Makonda inapishana na msimamo wa Rais Samia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Katibu Mkuu wa ADC Taifa, Doyo Hassan Doyo amesema kauli iliyotolewa na Katibu wa NEC – Itikani na Uenezi wa CCM, Paul Makonda kuwa vyama vya Upinzani Nchini havipo ni sawa na kupinga maelekezo ya Rais Samia Suluhu kuhusu maridhiano ya kisiasa.

Doyo ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa chama hicho, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, Jumatatu ya Oktoba 30, 2023, ambapo amesema kauli hiyo haikustahili kutolewa na kiongozi mwenye nafasi kubwa kama ya Mwenezi.
Amesema “Kauli ya Paulo Makonda kuwa kuanzia Oktoba 26 (2023) hakuna vyama vya Siasa vya upinzani Tanzania, yale sio maneno ya mzaha, yanapingana na 4R za Rais, ni jambo kubwa kuitangazia Dunia kuwa Tanzania hakuna vyama vya siasa vya pinzani.

“Tumefanya kikao juzi kuzungumzia jambo hilo kwa kuwa si jambo zuri na hapa leo tupo katika mkutano wa Bodi ya Uongozi kujadili mustakabari wa chama na kujiandaa kuwanyang’anya Dola CCM.”
6acb9fe2-49d9-4801-af8a-5f2d24d34cde.jpeg

a6e53f56-6291-49a5-9b93-78500afe371b.jpeg
Mwenyekiti
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa ADC Taifa, Hamad Rashid Mohamed amewataka Wanachama wenzake kutenda haki katika mchakato wa uchaguzi wa chama hicho, akisisitiza kila mwenye uhitaji na nia ya kuwania uongozi afanye hivyo bila kuwekewa kikwazo chochote.

“Lengo la ADC ni kuwapa nafasi watu wote, hauna haja ya kuogopa kuwa fulani na fulani wakija wanaweza kuchukua nafasi ya mtu fulani, tuwe huru na tutende haki kama ambavyo sera zetu zinavyosisitiza,” amesema na kuongeza

“Chama chetu kimejipambanua kutenda haki, pia naomba viongozi wetu mkasimamie hizi chaguzi, tusiende kuteua viongozi bali twendeni tukachague viongozi, kinyuma na hapo hatutakuwa tunajenga chama.

Ameipongeza Serikali kwa kuhakikisha amani inaendelea kuwepo Nchini licha ya mataifa mengi kutawaliwa na migogoro na mengine kufikia hatua ya kupigana vita.
50335600-be03-42b7-a903-55ade7a3af1f.jpeg

c55ebe38-2d88-406c-8230-cb5eac030b09.jpeg
Amesema “Tunaiomba Jumuiya za Kimataifa kusimamia haki, ni jukumu la Umoja wa Mataifa (UN) kusimamia haki za binadamu kwa kuwa sasa hivi hata taasisi zao zinashindwa kwenda kutoa misaada ya kibinadamu kutokana na mazingira ya vita.”

Akizungumzia maridhiano amesema “Nashauri hivi 4R za Rais Samia zifike hadi ngazi za chini ili watu wafahamu kuwa tunafanya siasa za kistaarabu, anayeshindwa akubali na anayeshinda ashinde kwa haki.

“Chama cheti sio chama cha kususia, tutashiriki katika uchaguzi kwa kuwa ni haki yetu ya Kikatiba, tutaenda kwenye uchaguzi na kama kuna chochote kitatokea basi kitatumika kama ushahidi.”

Aidha, amesisitiza kuwa maoni ya Kikosi Kazi yakifanyiw akazi kama yalivyoendekezwa basi Watanzania watanufaika kwa kuwa kuna mambo mengi mazuri yamefanywa na Kikosi hicho.

Makamu Mwenyekiti
Upande wa Makamu Mwenyekiti wa ADC, Shaban Itutu amesema anashauri Serikali ifanye mabadiliko katika Tume ya Uchaguzi kwa kuwa utendaji wao hautendi haki.

Amesema “Namshauri Rais Samia kuwa huu mchezo wanaofanya Tume ya Uchaguzi unatishia kuvunja amani ya nchi, kuna tabia nyingi za wizi wa kura zinazofanyika kwenye vituo vya upigaji kura, hivyo niombe wanaosimamia uchaguzi kuwa wanachokifanya si haki.”
 
Sio kweli ADC fanyeni kazi yenu ambayo ni siasa,Makonda was right to say that, report zenu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa..alafu ni mwenezi kama Kamwe na Ahmed Ally
 
Katibu wa ADC,aachane na Makonda,

Fuatilia kauli mujarabu za mwenyekiti na makamu wake (ADC) ,hao ni wabobezi wa siasa za nchi hii,hawajamgeuza Makonda kuwa agenda kwenye kikao chao,wamekwepa mtego huo,wameongea ya muhimu kuhusu chama chao

Katibu ADC kaonyesha ni dhaifu sana,rahisi sana kuingizwa mkenge
 
Back
Top Bottom