Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na linamshikilia Selemani Haruna maarufu Kwata (24), Mkazi wa Kimara Temboni mtaa wa Amani, kwa tuhuma za kumuua Editha Charles (22) Mkerewe, Binti wa kazi za ndani na kuuficha mwili huo katika stoo ya vifaa vya ujenzi katika nyumba ya Agatha Stanslaus.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Jumanne Muliro amesema “Uchunguzi wa awali umeonesha Mtuhumiwa tarehe 06/07/2022 asubuhi alifika kwenye nyumba aliyokuwa anayoishi Binti huyo wa kazi akijifanya fundi wa umeme na kwamba alitakiwa kuweka Balbu, alipoingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali Binti huyo na kumuua halafu akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba Tsh 1,800,000 na kutoweka”

“Polisi kwa Kutumia Watalaamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini Mtuhumiwa huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka, baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua Binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000 na mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane”

“Aliweza pia kuonesha kiasi cha pesa alizoziiba eneo hilo na pesa nyingine alidai mara baada ya tukio siku iliyofuata alinunua vitu mbalimbali zikiwemo simu mpya, viatu vya mpira pea 2, na begi la mgongoni lenye nguo mbalimbali mpya ambavyo navyo vimepatikana, kitendo alichofanya Mtuhumiwa ni cha ukatili ulipita kiasi, uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na atafikishwa katika mifumo ya kisheria ikiwemo Mahakamani haraka”
 
Asee wadada wa kazi wamekuwa victim sana wa ukatili majumbani. Sema na wao huwa hawana umakini na wakieleweshwa huwa hawasikii.

Unamwambia dada ukiwa ndani funga geti na mlango wa kuingilia ndani kwa funguo ila walaaaa hajali Unafika home unapita getini hadi unaingia ndani hadi room kwake wala hana habari anafanya kustuka.

Au huko mtaani ana kiboda boda chake au mhuni flani ukiwa haupo basi analetwa hadi home mazingira yanasomwa...mwisho wa siku matukio ya wizi au mauaji... Kwa hali hii jamani kweli watakuwa salama..?
 
Back
Top Bottom