Kisa cha binti wa field na host supervisor wake

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
Moja kati ya mambo yamezungumzwa sana ni pamoja na rushwa ya ngono katika taasisi za elimu - yaani wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kuombwa au kutoa "utamu" kwa wakufunzi ili wapate alama nzuri na kisha wafaulu mitihani yao. Hili limezungumzwa sana na hadi uchunguzi wa kina umefanyika katika baadhi ya nchi barani Afrika na kuwaweka "uchi" wakufunzi wenye tabia hizo.

Hata hivyo, moja kati ya mambo ambayo pia yanajitokeza na hayajawahi kupata kuelezwa wazi kwa jamii zetu ni pamoja na vitendo wanavyokumbana navyo wanafunzi wanaoenda kufanya mazoezi ya masomo yao kwa vitendo.

Kwa utaratibu wa baadhi ya vyuo (sina hakika ni vyote), ni kwamba kunakuwa na msimamizi (host/immediate supervisor) wa mwanafunzi husika kwenye shirika au taasisi aliyokwenda kufanya mazoezi ya vitendo (field/internship) ambaye yeye ndiye atakayehusika na utendaji wa binti/kijana huyo na atapaswa kutoa ripoti ya utendaji wake kwa mfumo wa alama - A,B,C,D nk.

Supervisor huyo, kwakuwa ana mamlaka ya kutoa alama za utendaji wa mwanafunzi husika, anaweza kuomba rushwa ya ngono ili "amwelezee vizuri" mwanafunzi huyu kwenye ripoti itakayokabidhiwa kwa chuo chake.

Kuna binti yeye alipangiwa kuja ofisini kwetu. Ni moja ya taasisi za masuala ya afya jijini Dar. Ni binti mrembo kabisa. Baada ya kuripoti ofisini, alikabidhiwa kwa supervisor mwanaume, jamaa mwenye umri wa miaka kama 40+.

Baada ya siku kadhaa pale ofisini, bwana huyo alimwalika binti dinner. Binti akaona si mbaya, kwakuwa jamaa aliahidi pia kutakuwa na wafanyakazi wengine (wanawake kwa wanaume) hivyo akakubali. Na ilikuwa hivyo kweli. Tulikuwepo watu kadhaa.

Hata hivyo, baada ya kupata kinywaji kidogo, mshikaji ikabidi aweke dhamira yake hadharani. Akamwambia binti kuwa yupo tayari kumpatia alama A kwenye ripoti yake ya field ikiwa atamkubalia walale naye. Binti akashangaa, "He! Yamekuwa haya?"

Jamaa akamwambia kuwa amemuelewa na angefurahi jambo lake likifikiriwa ili pawe na win-win situation. Siku zikaenda na binti akaendelea kukataa katakata hata baada ya jamaa kuleta vitisho vya kuwa atampa alama chache kwenye assessment.

Kishingo.jpg

Basi bwana, mambo yalivyokuwa ya moto zaidi, hili suala likaanza kusambaa ofisini kiumbea umbea. Baadaye likamfikia bosi na binti akatema cheche kuwa jamaa alikuwa anamtaka kimapenzi ili mwisho wa siku ampe "maksi za kushiba".

Bwana we! Bosi alikuwa ni mmama. You can imagine alivyotokwa na povu. Jamaa akasemwa kwenye kikao na akanyang'anywa hadhi ya u-supervisor wa yule binti, kisha akala barua ya onyo zito. Binti sasa akapewa supervisor wa kike.

Kuanzia pale ikawa akija kijana wa field anakabidhiwa kwa supervisor wa jinsia yake. Jamaa alikuja kuhama kazi na sasa ni bosi fulani kwenye taasisi nyingine ya kimataifa. I hope huko watoto wa field wapo salama.

Rushwa ya namna hii nimeisikia kwa watu kadhaa. Kuna mabinti kama watatu hivi wamewahi kunipa stori za namna hii. Lakini pia nimekutana na majamaa yanajisifu kutumia mbinu hiyo kuwatafuna interns.

Ubaya ni kwamba jambo hili huwa haizungumzwi sana. Je, huenda watu hawalioni kama tatizo? Vipi, wewe umewahi kukutana au kushuhudia jambo kama hili ofisini kwako?
 
Jamaa alizingua kama alimuelewa mtoto angetupia sound kikawaida tu kama mtoto angeingia kwenye mfumo basi ilo suala la kumpata alama nzuri liwe matokeo tu ya mahusiano.
 
Wababa wa maofisini/ mtaani/ wanaume wote kwa ujumla ni walaku wa mabinti…
 
Ilikuwa apigwe gegedo mimi mzazi mwenye watoto wa kike huwa nahuzunika sana. Ndio maana napambana niwajengee uwezo.
 
Hii ipo sana na inaonekana kawaida kabisa, Binti wa watu unakuta akipita koridoni Kila ofisi inamuita imsalimie.
 
Back
Top Bottom