Pwani: Akamatwa na Polisi kwa kummwagia chai Dada wa Kazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Janeth Dominic(26) mkazi wa Kwamathias Wilaya ya Kibaha kwa tuhuma za shambulio la kudhuru mwili wa dada wa kazi za ndani Filomena Erick (17).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema tukio hilo lilitokea Septemba 14 majira ya saa mbili asubuhi ambapo msichana huyo alishambuliwa na mwajiri wake kwa kumwagiwa chai ya moto na kuunguzwa maeneo ya shingoni, mkononi, kifuani na shingoni.

Amesema Mtuhumiwa anadaiwa kufanya tukio akimtuhumu msichana huyo kuiba sukari na simu katika chumba cha mpangaji mwenzao.

Kamanda Lutumo amesema mtuhumiwa atafikishwa kwenye mifumo ya sheria baada ya upelelezi kukamilika, huku akitoa wito kwa watu wanaoishi na wadada wa kazi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwani tukio kama hilo halikubaliki kwenye na nikinyume na sheria.
 
Back
Top Bottom