Afukua mwili wa mwanae na kwenda nao nyumbani kuufanyia maombi afufuke

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Mkazi wa Mtaa wa Kapalangao Manispaa ya Mpanda, Fransis Nilanga amedaiwa kufukua kaburi la mwanaye kisha kubeba jeneza lenye mwili huo kwenda nalo nyumbani kufanya maombi ili afufuke.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumanne Januari 30, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema tukio hilo limetokea Januari 28 saa saba usiku.

"Mtoto wake alifariki na kuzikwa Julai mwaka jana katika makaburi ya Kazima akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu. Sisi tulipata taarifa kutoka kwa dereva wa bajaji aliyejitambulisha kwa jina la Alex, akisema wakati anapita eneo hilo alimuona amebeba jeneza alimuomba amsaidie kubeba kwenda nyumbani," amesema Kamanda Ngonyani.

Pia, amesema baada ya kupata taarifa walimkamata na alipofikishwa Kituo cha Polisi Mpanda kufanyiwa uchunguzi, walibaini mtuhumiwa huyo ana ugonjwa wa afya ya akili.

Source; Mwananchi.
 
kifo cha mtoto kinauma sana asee, Mungu amtie nguvu
 
Back
Top Bottom