mtetezi wa MAGU
Member
- Dec 15, 2022
- 12
- 71
Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote amekuwa akitafutwa kwa kutekeleza mauaji ya watu mbalimbali katika maeneo ya Longdong, Ungalimited na Sinoni
Kijana huyu alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi, majira ya Leo mchana wananchi wenye hasira kali wamemtia nguvuni na kumpokonya uhai.
---
Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha leo wamejitokeza kushuhudia mwili wa kijana anayetambuliwa kwa jina la Ally Dangote (19) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, akidaiwa kutoroka baada ya kukamatwa.
Dangote kabla ya kutajwa kuhusika na matukio ya mauaji alikuwa rumande Magereza kwa muda mrefu kwa tuhuma za mauaji na hatimaye mwaka huu aliachiwa huru na Mahakama kutokana na kukosekana ushahidi lakini alikamatwa tena baada ya tuhuma za uhalifu mwingine.
Akizungumzia kifo hicho leo Jumatatu Novemba 20, 2023 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salvas Makweli amesema Dangote ameuawa baada ya kupata jeraha la risasi wakati akiwatoroka polisi.
"Ni kweli huyu mtuhumiwa alikuwa anasakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za wizi na mauaji na leo baada ya kuwekewa mitego tulimkamata na wakati anakwenda kuwaonesha wenzake aliruka kwenye gari na ndipo alipigwa risasi na kutokana na kuvuja damu nyingi alifariki akiwa hospitali," amesema.
(Imeandikwa na Mussa Juma)
Pia soma > Kibaka maarufu, Ally Dangote atiwa mbaroni Arusha
Ally Dangote(Kulia)