Dec 15, 2022
11
68
Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote amekuwa akitafutwa kwa kutekeleza mauaji ya watu mbalimbali katika maeneo ya Longdong, Ungalimited na Sinoni

Kijana huyu alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi, majira ya Leo mchana wananchi wenye hasira kali wamemtia nguvuni na kumpokonya uhai.
---
Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha leo wamejitokeza kushuhudia mwili wa kijana anayetambuliwa kwa jina la Ally Dangote (19) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, akidaiwa kutoroka baada ya kukamatwa.

Dangote kabla ya kutajwa kuhusika na matukio ya mauaji alikuwa rumande Magereza kwa muda mrefu kwa tuhuma za mauaji na hatimaye mwaka huu aliachiwa huru na Mahakama kutokana na kukosekana ushahidi lakini alikamatwa tena baada ya tuhuma za uhalifu mwingine.

Akizungumzia kifo hicho leo Jumatatu Novemba 20, 2023 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salvas Makweli amesema Dangote ameuawa baada ya kupata jeraha la risasi wakati akiwatoroka polisi.

"Ni kweli huyu mtuhumiwa alikuwa anasakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za wizi na mauaji na leo baada ya kuwekewa mitego tulimkamata na wakati anakwenda kuwaonesha wenzake aliruka kwenye gari na ndipo alipigwa risasi na kutokana na kuvuja damu nyingi alifariki akiwa hospitali," amesema.

(Imeandikwa na Mussa Juma)

Pia soma > Kibaka maarufu, Ally Dangote atiwa mbaroni Arusha

Dangote.jpg

Ally Dangote(Kulia)​
 
Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote Amekuwa akitafutwa kwakutekeleza mauaji ya watu mbali mbali katika maene o ya Longdong,Ungalimited na Sinon Kijana huyu alikuwa anatafutwa na Joshua la Polisi majira ya Leo mchana wanannchi Wenye hasira kali wamemtia Nguvuni na kumpokonya Uhai...
Kwanini alikuwa akiua watu kama unavyadai? Sababu ya huyu mtu kutekeleza mauaji ya watu hasa ilikuwa nini?
 
Pole kwa familia,ndugu na jamaa,may his soul R.I.P.
Mob justice ni mbaya,wangempeleka mbele ya vyombo vya sheria,haki itendeke,ukute alisingiziwa au kafananishwa.
Ni kweli mob justice ni mbaya. Lakini ukiona katajwa hilo jina inaonekana ni mtu maarufu kwa shughuli hiyo na anafahamika kwa hilo.

Shida kubwa ni polisi huwa wanawaachia wakishahonga.
 
Kwanini hakuna Mob Justice kwa mafisadi wa fedha za Umma na extra judicial killings chini ya baraka za serikali ? rejea watu kuokotwa kwenye viroba, Ben Saa 8, Azori & E.t.c ... Wezi wa kuku na viTVndio wanauwawa wa Matrillion wanasindikizwa na Escort hotelini kupumzika na Michepuko.
 
Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote Amekuwa akitafutwa kwakutekeleza mauaji ya watu mbali mbali katika maene o ya Longdong,Ungalimited na Sinon Kijana huyu alikuwa anatafutwa na Joshua la Polisi majira ya Leo mchana wanannchi Wenye hasira kali wamemtia Nguvuni na kumpokonya Uhai...
Joshua la polisi. Edit hapo
 
Ally Dangote sio vijana wa Sa7ya kweli?
 
Pole kwa familia,ndugu na jamaa,may his soul R.I.P.
Mob justice ni mbaya,wangempeleka mbele ya vyombo vya sheria,haki itendeke,ukute alisingiziwa au kafananishwa.
Huyo janja wacha wamuue ni mhuni mbaya.. nammanya kwetu Arusha ni kimbaka hatari ashakuwa na roho ya malaika izraeli. Amekulia mitaa ya uswahilini in short wananchi wamefanya kazi yao. Jela alishaenda sana na kutoka.
 
Hivi we jamaa upo serious kweli? Au mgeni nchi hii!

Eti may his soul bla bla bla.... kwa jambazi muuaji
Nipo serious mkuu, ukute alifananishwa au labda ni yeye, ndo maana nikasema, ni vema angetiwa nguvuni, halafu afikishwe mbele ya vyombo vya sheria, haki itendeke. Hiyo mob justice, ingekuwa vema ikaelekezwa kwa wezi wa mali za umma, ambao wanajulikana na karibia kila mtanzania, ila sheria hazichukui mkondo wake, jamii ingeheshimika kuliko kumuua mtu tena yawezekana hakupewa hata nafasi ya kusikilizwa lakini ndo hivyo.

Kuna habari za watu wengi tu kuuawa kwa kuitiwa mwizi huku si kweli na watu kuua bila kumhoji wala kumsikiliza, siyo fair kabisa. Anyway ndiyo umma wetu huu.
 
Back
Top Bottom