Bodaboda amuua mtoto wake kwa kumkata shingo

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja aitwaye Amedius Mfoi (25) dereva bodaboda mkazi wa Muriet Jijini Arusha kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Amani Amedius Mfoi (03) Mkazi wa Morombo jijini Arusha.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 23, 2024 muda wa saa 12:00 jioni mtaa wa Murieti Tarafa ya Elerai katika manisipaa ya jiji la Arusha.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alimkata shingo mtoto huyo na kitu chenye ncha kali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Aidha ameeleza kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi mara moja Jeshi hilo lilianza uchunguzi na kumtafuta mthumiwa huyo kwa kushirikiana na wananchi ambapo walifanikiwa kumkamata muda mchache baadae.

ACP Masejo amesema baada ya uchunguzi Jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Credit-CloudsTv
 
Afu unapost sa hivi hii habari iko huku toka jumatano

Mods futeni huu uzi
Acha kukurupuka kijana, hii habari kiini chake ni kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Habari huwa na muendelezo, na huu ndio muendelezo wa kilichpostiwa huko nyuma. Acha kujifanya mjuzi kwenye habari zinazogusa maisha ya watu.

UWE UNASOMA NA KUELEWA.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Acha kukurupuka kijana, hii habari kiini chake ni kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Habari huwa na muendelezo, na huu ndio muendelezo wa kilichpostiwa huko nyuma. Acha kujifanya mjuzi kwenye habari zinazogusa maisha ya watu.

UWE UNASOMA NA KUELEWA.
Ume like comment jamaa aliyowaomba Mods kufuta huu uzi wako
 
Asee ninavyopenda wanangu sijui ni shetaningani kamuingia dogo mpka anachinja mtoto asee dunia ina unyama mwingi sana wa kutisha
 
Back
Top Bottom