Alichokizungumza Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Plasduce Mbossa, kwenye mahojiano na TBC

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
ALICHOKIZUNGUMZA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA)PLASDUCE MBOSSA, KWENYE MAHOJIANO NA TBC

“Bandari ya DSM iko kwenye hatua ya kufanyiwa maboresho, na utaratibu wa kutafuta kampuni kuendesha bandari ni utaratibu wa kawaida na tulikua na kampuni inaitwa TICS ambayo mkataba wake umeisha Disemba 2022, na sasa tumeanza hatua nyingine za kuboresha zaidi"

"TPA bado haijasaini Mkataba na kampuni yeyote, Mkataba uliosainiwa ni kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ni kuhusu ushirikiano kwenye masuala ya bandari kuhusu tehama, mafunzo ya uendelezaji na uendeshaji wa bandari, baada ya hapo ndiyo kutakua na mikataba ya utekelezaji"

“Kinachoongelewa sasa mtandaoni ni mikataba ya utekelezaji ambayo bado haijadiliwa na wala haijasainiwa, kwa mtu anayesema kuna mwekezaji kapewa miaka 100, atakua anatatizo kidogo hakuna nyaraka yeyote iliyosema tumesaini miaka 100."

"Kilichosainiwa ni Framework Agreament baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai halafu baadaye kutakua na mikataba ya utekeleza kati ya Serikali na Kampuni ambao Mkataba wa Uwekezaji, halafu kutakua na mikataba ya uendeshaji kwa hiyo sasa hivi ni mapema sana kusema atakaa miaka mingapi au atapewa eneo gani"

“Sisi tuna gati 12 na kila gati Kwa wastani tunakua na Meli 10, lakini kila wakati tunakua na meli zaidi ya 20 zinazosubiri na huwa wanatuchaji gharama za kusubiri unaweza kulipa mpaka Dola 3000, sasa lazima tuchukue hatua za kumaliza tatizo kwa kutafuta mwekezaji ambaye anaweza kumaliza hali hii"

“Kampuni ambayo itapewa nafasi ya kuendesha lazima itakua na na uzoefu wa kufanya hii kazi, iwe na mahusiano mazuri bandari kavu za nchi za jirani lakini muhimu zaidi iwe na mahusiano mazuri na Makampuni mengi ya Meli Duniani"

SOURCE: TBC - ARIDHIO

FB_IMG_1686164274029.jpg
 
It is too early to say any thing about the saga so long as CCM peope are in power.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa akizungumza na Clouds FM amesema:

“Kwenye mkataba hakuna sehemu kuna miaka 100, nafikiri walioleta hilo wana malengo yao, ni upotoshaji wa hali ya juu, mkataba uliopo una kifungu kinachosema kwamba baada ya mkataba kuridhiwa na ikapita miezi 12 bila kufanya chochote maana yake mkataba utakuwa umekwisha.

"Pia kama tutaingia kwenye majadiliano tukashindwa kufikia muafaka na kusaini mikataba ya utekelezaji maana yake mkataba utakuwa umekwisha.

“Mkataba huu mkubwa (mkataba mama) si wa utekelezaji, kuna taratibu za kuingia mikataba ya utekelezaji tukijadiliana tutajadiliana terms zote pamoja na suala la muda, hivyo watu waelewe kuwa muda tutaupata katika mikataba ya utekelezaji ambayo itafuata.”

"Kuna mkataba Kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Emirates ya Dubai ambao unahusu masuala ya Bandari. Mkataba huu unahusu Mashirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo Mafunzo katika masuala ya Bandari.

"Ushirikiano katika masuala ya TEHAMA na ushirikiano katika masuala ya uendelezaji na uendeshaji wa bandari. Mkataba unaotajwa ni Inter-Governmental Agreement.

"Mkataba huu pamoja na mambo mengine unaelekeza kwamba kama tunataka kushirikiana ni lazima tukubaline katika mikataba mingine ya tofauti na huu.

“Kwa kawaida utekelezaji wa shughuli za bandari haufanywi moja kwa moja na Serikali Kuu lakini imekasimu kwa Taasisi kwa upande wetu ni TPA na kwa wenzetu ni DP WORLD.”

"Mkataba huu moja kati ya masharti yake unatakiwa kuridhiwa ni kwa kuwa ni Mkataba wa nchi na nchi, ni mkataba wa Kimataifa ili uweze kutumika unatakiwa kuridhiwa na pande zote mbili.

“Utaratibu wetu wa kuridhia kama nchi ni utaratibu ambao unatolewa na Katiba Ibara ya 63, Ibara Ndogo ya 3E. Ambapo unataka kwamba mkataba Wenye masharti ya kuridhiwa ni lazima ipeleke bungeni kwa ajili ya kuridhiwa.

“Kwa ufupi ni kwamba kuna mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai unaohusu mashirikiano katika sekta ya Bandari! Mkataba huo unaelekeza kama tunataka kushirikiana ni lazima tukubaliane katika mikataba mingine tofauti na huu

“Kilichosainiwa ni mkataba huu, lakini ili mkataba huo uweze kutumika ni lazima uridhiwe na pande zote mbili! Utaratibu wetu wa kuridhia kama nchi unatolewa na katiba, katiba yetu inaeleza mkataba wenye masharti ya kuridhiwa ni lazima upelekwe Bungeni, na changamoto hizi zimetokea baada ya hatua hiyo, nadhani ni uelewa tu wa baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii.

"Kushauri ni Kati ya moja ya kazi za bunge. Bunge ndio linaridhia na kuangalia Serikali imesaini na upande mwingine likiangalia kilichoandikwa mule kwenye mtakaba kama uko sawa kulingana na utaratibu. Na kinachofanyika sasa ni utaratibu wa kuridhia na hilo linapelekwa Bungeni na bungeni kuna taratibu nyingi kupelekwa kwenye kamati na baadae litafika bungeni.

"Miaka yote tumekuwa tukifanya wenyewe, tunachotaka ni kupata manufaa tunavyoweza kuyapata kutoka kwao lakini pia mkataba huu unasema ni kuwajengea uwezo Watanzania.

"Sasa hivi tuna Kampuni kubwa za Watanzania. Kipindi cha nyuma Kampuni nyingi za usafishaji zilikuwa zikitoka Kusini mwa Afrika ndio zilikuwa zikifanywa kazi hapa lakini sasa hivi tuna Kampuni kubwa kabisa za Kitanzania na wafanyabiashara wakubwa.

"Kampuni hii ya DP WORLD ana vitu ambavyo tunadhani tukishirikiana naye vitatusaidia sisi kupiga hatua kutoka hapa tulipo.
 
Baada ya miezi 12 bila kufanya chochote ndio nini sasa? , aseme huo mkataba waliosaini ni wa miaka mingapi?, au mkataba huo hauna ukomo?
 
Mbona sijaona aliposema wakianza kazi itakua ni kwa muda gani,
Hili swala kwa alivyoongea huyu jamaa ni kwamba mtake msitake waarabu watachukua bandari au labda kama sijaelewa
 
bandari ni mali ya umma , tunamaslahi nayo kama umma WA WTZ , Akodishe bandari ya zenji siyo Bandari za Tanganyika , hana uzalendo huyo mtu wenu wa kijani kutoka zenji , ameshauza mbuga za wanyama sasa bandari zetu....
Kwani haikua imekodishwa kabla!?
 
Ni ngumu sana kumwamin anachosema, maana nimejaribu kumsikiliza ni kama vile msimamizi wa Shamba anavyowatetea Nyani kwa mwenye Shamba kuwa hawana madhara.
 
Katika maelezo yake yote hakuna sehemu aliyotaja kuwa DP World kupitia huu mkataba watapewa haki za kuendeleza na kuratibu shughuli zote za uendeshaji.
 
Hapo mwisho kasema kuna kampuni kubwa za usafirishaji za watanzania, inashindikana nini hizo kampuni za kitanzania kupewa kuendesha bandari hadi atafutwe mwarabu.

Maana hizo kampuni za kitanzania zitakuwa na uwezo kwenda kujifunza shughuli zinavyoendeshwa huko dubai na hata kununua au kukodi teknolojia kutoka huko.​
 
Back
Top Bottom