Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa Zelensky na majeshi yake ya Ukraine wamekuwa wakiwatumia raia kama ngao za vita.
Umoja huo umetaja mapigano ya maeneo tofauti tofauti ambapo majeshi ya Ukraine yaliwazuia raia wasio na hatia wakiwemo wanawake, wajawazito, wazee, walemavu, wagonjwa, na watoto...
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeichagua Msumbiji kuwa mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza hilo kwa muhula wa miaka miwili kuanzia Januari 2023
Nchi nyingine zilizochaguliwa ni pamoja na Ecuador, Japan, Malta na Uswizi ambapo watachukua nafasi za India, Ireland, Kenya, Mexico na Norway...
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa (UN), Vassily Nebenzia ametoka nje ya kikao ya Baraza la Usalama baada ya Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel kuishutumu Moscow kwa kusababisha janga la Chakula duniani
Michel ameyashutumu Majeshi ya Urusi kwa uhalifu wa kivita na makosa mengine ya...
Mmoja wa wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa (UN) ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa wote wakiwa ni raia wa Jordan, jana Juni Mosi, 2022 katika shambulio la kigaidi dhidi ya msafara wao katika Jimbo la Kidal, Kaskazini mwa Mali.
Msafara wao ulishambuliwa kwa silaha ndogo katika...
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa watu milioni 18 katika eneo la Sahel barani Afrika wanakabiliwa na njaa kali katika miezi mitatu ijayo kutokana na athari za Vita kati ya Urusi na Ukraine, janga la COVID-19 na mabadiliko ya hali ya hewa
Inaelezwa kuwa idadi kubwa zaidi ya watu wako katika hatari...
Umoja wa Mataifa umesema Vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine imezidisha uhaba wa Chakula katika Mataifa masikini kutokana na kupanda kwa bei. Imeelezwa kuwa, baadhi ya Nchi zinaweza kukabiliwa na njaa ya muda mrefu ikiwa mauzo ya nje ya Ukraine hayatarejeshwa katika viwango vya awali...
Marekani na Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya mwandishi wa habari wa Al Jazeera ambaye alikuwa anaripoti kuhusu operesheni ya jeshi la Israel katika ukingo wa magharibi.
Shireen Abu Akleh, m
Mmarekani mwenye asili ya Palestina mwenye umri wa miaka 51, alipigwa risasi licha ya...
Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu ukiukwaji wa haki za watoto kwa kuajiriwa na magenge ya kihalifu, huku ghasia zinazoongezeka katika mji mkuu wa #Port-au-Prince, zikisabisha vifo vya makumi ya raia na zikiwalazimisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao
-
Naibu msemaji wa Umoja wa...
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu amekosoa uamuzi wa Mali wa kupiga marufuku vyombo vya habari vya Ufaransa na kuwataka watawala wake wa kijeshi kubadili uamuzi wao.
"Tumesikitishwa sana na uamuzi wa Mdhibiti wa Vyombo vya Habari wa Mali kuifungia Radio France...
Leo Baraza Kuu la Umoja wa Màtaifa lilipigia kura azimio lililopendekezwa na Marekani kuiondoa Urusi kwenye tume ya hàki za binadamu ya umoja wa mataifa.
Sababu ni Urusi kudaiwa kukiuka haki za binadamu ñchini Ukraine wanakopigana vita.
Katika kupiga kura Tanzania iliamua kuungana na nchi...
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepiga Kura kuisimamisha Urusi katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja huo (UNHRC) kama adhabu kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine
Kati ya Wajumbe 193 wa Baraza hilo, 93 walipiga Kura ya kuunga mkono kusimamishwa Urusi, 24 walipinga na 58 hawakupiga Kura
Hii...
Umoja wa Mataifa (UN) kupitia ukurasa wake wa twitter wameutaja mtandao wa kijamii wa WhatsApp kama njia rahisi ya kusambaza taarifa zisizo sahihi.
Wameandika ujumbe kupitia WhatsApp huweza kuonekana kama umetoka kwa mtu wa karibu. Wamesema ni muhimu kuhakiki ujumbe kabla ya kuutuma kwa...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vinaweza kusababisha kile alichokiita "kimbunga cha njaa" na uhaba wa chakula kote duniani.
Alisema nchi nyingi za Afrika na maskini zinategemea zaidi uzalishaji wa ngano wa Urusi na Ukraine...
Waziri wa Afya wa Ukraine, Viktor Liashko amesema Vikosi vya Urusi vimeshambulia na kuleta uharibifu kwa Hospitali takriban 61. Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) inasema Raia wapatao 474 wameuawa tangu uvamizi wa Urusi kuanza
Mbali na Vifo, inaelezwa kuwa Raia wengine 861...
Zaidi ya wajumbe 140 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo Machi Mosi, 2022 walitoka nje ya ukumbi baada ya kukataa kusikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.
Waziri huyo alikuwa akishiriki mkutano huo kwa njia ya video kutokana na mipaka ya ndege...
Ni vigumu Umoja wa Mataifa kuichukulia hatua Urusi. Changamoto za Umoja wa Mataifa kupitia baraza kuu la usalama kuichukulia hatua Urusi ni mbili.
Kwanza, tatizo linakuja pale ambapo Urusi ni mmoja wa wanachama wakudumu wa baraza la usalama akiwa pamoja na China, UK, France na USA. Hivyo Ni...
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira ambayo imetolewa leo, imesema uchafuzi unaofanywa na kampuni pamoja na nchi mbalimbali husababisha vifo vingi kuliko hata vifo vinavyosababishwa na janga la COVID-19
Kulingana na ripoti hiyo, dawa za kuwaua wadudu, plastiki na uchafu kutokana na vifaa...
Wataalam wa Umoja wa Mataifa wamesema kwenye ripoti yao kwamba Korea ya Kaskazini inaendelea kuiba mamilioni ya dola kutoka katika taasisi za kifedha na makampuni yanayojihusisha na sarafu za mitandao na ubadilishanaji fedha.
Wataalamu hao waliowanukuu wataalamu wa masuala ya mitandao kwenye...
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya ya Njaa Kaskazini mwa Nchi hiyo ikielezwa zaidi ya 80% ya Familia hazina uhakika wa chakula, hali inayopelekea Watoto chini ya miaka mitano kuwa na Utapiamlo.
Mashirika ya Misaada yamekuwa yakipata changamoto kufikisha mahitaji Mkoa wa Tigray ambapo...
Katika picha hapo juu unaweza kuona umuhimu wa kujua asili ya namba 666 na kwa nininamba hiyo inatumiwa na viongozi wakuu wa umoja wa mataifa. Kwa kifupi kwenye picha hiyo wapo watu 6 wakiongoza mkutano wa umoja wa mataifa na nyuma yao kuna kitambaa kilichoandikwa ‘United Nations 666’ kumaanisha...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.