Memba wa Umoja wa Mataifa waondoka ukumbini, wasusia hotuba ya Waziri wa Urusi

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Zaidi ya wajumbe 140 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo Machi Mosi, 2022 walitoka nje ya ukumbi baada ya kukataa kusikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.

Waziri huyo alikuwa akishiriki mkutano huo kwa njia ya video kutokana na mipaka ya ndege kwenda Geneva kutoka Urusi kuzuiwa, ambapo alikuwa akizungumzia mbele yao kuhusu kuhalalisha wa uvamizi wa kijeshi wa taifa lake dhidi ya Ukraine ambao bado unaendelea.

Wanadiplomasia walioshiriki katika mkutano huo hasa kutoka Marekani na Uingereza ndiyo ambao walianza kusimama na kuondoka wakati video ya Waziri huyo ikiendelea.

Source: Reuters

===========================================

EU, US, British envoys boycott Lavrov speech at UN rights forum

GENEVA, March 1 (Reuters) - Dozens of diplomats from the European Union (EU), United States and Britain walked out of a speech by Russian Foreign Minister Sergei Lavrov to the top U.N. human rights forum on Tuesday, according to a Reuters witness.

Lavrov was addressing the U.N. Human Rights Council remotely, having cancelled his attendance earlier due to what the Russian mission in Geneva said on Monday were EU states blocking his flight path.

Eu 1.jpg

Eu.jpg
 
Hawa wazungu mara nyingine kama binadamu kamili utabaki tu kujiuliza, ukamilifu wa ustaarabu wanaojivunia upo wapi.

Hivi waliwahi kususia hotuba za Waziri Mkuu wa Israel aliyepita, licha ya maovu yote aliyoyafanya dhidi ya Palestine.

Hii Dunia imejaa unafiki sana.
 
Wajinga tu uhuru wa kuongea mwache na mwenzako mwenye mawazo mbadala aongee kukubali au kutokubali suala lingine. Hawa wanataka kila mtu afuate wanavyotaka wao. Hope kulikuwa na nchi za Africa na South America najuwa hao wanawajuwa hawa nitashangaa kama Africa nao walitoka labda yule mkenya
 
EU + USA wamegeuka kua chadema,hii hatari sasa
Zaidi ya Chadema wanatisha watu mpaka kwao watu wanaogopa wenye maoni tofauti sasa hivi huko kwao ukisema tu uko na Russia cha moto utakiona hata ukisema vita hapana bila kumsema Putin utapata shida ni kama ukawaseme mayahudi au ukate Holocausts haikuwa kweli basi utapigwa mawe kila sehemu. Ila wakitoka kuja kwetu uhuru wa kuongea haki za binadamu na kushiriki democracy kwao wenyewe democracy wanaikanyaga.
 
Hawa wazungu mara nyingine kama binadamu kamili utabaki tu kujiuliza ukamilifu wa ustaarabu wanaojivunia.

Hivi waliwahi kususia hotuba za Waziri Mkuu wa Israel aliyepita, licha ya maovu yote aliyoyafanya dhidi ya Palestine.

Hii Dunia imejaa unafiki sana.
Kunywa juisi nitalipia...
 
Zaidi ya wajumbe 140 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo Machi Mosi, 2022 walitoka nje ya ukumbi baada ya kukataa kusikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.

Waziri huyo alikuwa akishiriki mkutano huo kwa njia ya video kutokana na mipaka ya ndege kwenda Geneva kutoka Urusi kuzuiwa, ambapo alikuwa akizungumzia mbele yao kuhusu kuhalalisha wa uvamizi wa kijeshi wa taifa lake dhidi ya Ukraine ambao bado unaendelea.

Wanadiplomasia walioshiriki katika mkutano huo hasa kutoka Marekani na Uingereza ndiyo ambao walianza kusimama na kuondoka wakati video ya Waziri huyo ikiendelea.

Source: Reuters

===========================================

EU, US, British envoys boycott Lavrov speech at UN rights forum

GENEVA, March 1 (Reuters) - Dozens of diplomats from the European Union (EU), United States and Britain walked out of a speech by Russian Foreign Minister Sergei Lavrov to the top U.N. human rights forum on Tuesday, according to a Reuters witness.

Lavrov was addressing the U.N. Human Rights Council remotely, having cancelled his attendance earlier due to what the Russian mission in Geneva said on Monday were EU states blocking his flight path.

View attachment 2135280

View attachment 2135281

Putin awe makini jeshi la marekani laweza kujipenyeza kwa style ya mescenaries Vita isiishe.
 
Back
Top Bottom