Marekani na Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya Mwandishi wa Habari wa Al Jazeera

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Marekani na Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya mwandishi wa habari wa Al Jazeera ambaye alikuwa anaripoti kuhusu operesheni ya jeshi la Israel katika ukingo wa magharibi.

Shireen Abu Akleh, m
Mmarekani mwenye asili ya Palestina mwenye umri wa miaka 51, alipigwa risasi licha ya kuripotiwa kutambulika vyema kama mwandishi wa habari alipokuwa akifanya kazi yake katika mji wa Jenin.

“Tumeshtushwa na mauaji ya mwanahabari Mmarekani Shireen Abu Akleh katika ukingo wa magharibi na tunalaani vikali mauaji hayo,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price ameandika kwenye Twitter.

“Uchunguzi lazima ufanyike haraka na uwe wa kina na waliohusika wawajibishwe. Kifo chake ni shambulio kwa uhuru wa vyombo vya habari kila mahali,” Price ameongeza.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imeandika kwenye Twitter kuwa imeskitishwa sana na mauaji hayo.

“Ofisi yetu iko uwanjani kuthibitisha ukweli. Tunaomba uchunguzi huru na wa wazi kuhusu mauaji yake. Tabia ya kutoadhibu lazima ikomeshwe.”

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas na Al Jazeera wameelezea kifo cha Abu Akleh kama mauaji ya kinyama yaliyofanywa na jeshi la Israel, ambalo lilisema darzeni ya Wapalestina wenye silaha walikabiliana na wanajeshi ambao walimkamata mwanamgamo wa kundi la Hamas mjini Jenin.

Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet amesema Abbas ametoa madai yasiyokuwa na msingi hata kabla ya uchunguzi wa kina kufanyika juu ya tukio hilo.

“Inaonekana Wapalestina wenye silaha ambao walikuwa wanafyatua risasi kiholela wakati huo walihusika na kifo cha kuskitisha cha mwanahabari huyo,” Bennet amesema katika taarifa.

Mwandish.jpg
 
Haya wale pro Russia mkiongozwa na Muslims wa kwa mpalange, njoo muone Marekani adui yenu alivyolaani siyo mnapita kimya kimya kama hamuoni
 
Back
Top Bottom