Je, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lina uwezo wa kufanya maamuzi dhidi ya Russia?

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,766
21,763
Ni vigumu Umoja wa Mataifa kuichukulia hatua Urusi. Changamoto za Umoja wa Mataifa kupitia baraza kuu la usalama kuichukulia hatua Urusi ni mbili.

Kwanza, tatizo linakuja pale ambapo Urusi ni mmoja wa wanachama wakudumu wa baraza la usalama akiwa pamoja na China, UK, France na USA. Hivyo Ni muasisi wa umoja wa Mataifa. Je itakuwa rahisi kuichukulia hatua Urussi ambayo ni mshirika mkuu wa UN na mwasisi wa umoja huo?

Pili, Russia Kama mwanachama wa kudumu wa baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ananguvu ya VETO ya kubatilisha maamuzi ya baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa.

NB: Nadhani hizi sababu mbili ndizo zimepelekea Urusi kujiamini mpaka Sasa.
 
Hilo baraza limekuwa useless kwa muda mrefu tu kuhusu kufanya maamuzi ya kuzuia migogoro.

Jambo pekee tu ni kwamba, kupitia maamuzi hayo yaliyofeli, ukizingatia kuwa kura ya veto ilikuwa moja pekee, yanatoa muelekeo kwa jumuiya ya kimataifa kuisusia Urusi hasa katika masuala mbalimbali ya kimataifa, yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia.
 
Urusi anasusiwa vingi poland ashasusa kucheza naye mechi ya world cup qualifying, UEFA champion ishapelekwa france
 
Back
Top Bottom