UN: Uchaguzi wa Libya waweza kusogezwa hadi mwezi Juni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya Libya Stephanie Williams amesema anapendekeza kufanyika uchaguzi wa Libya ifikapo Juni, baada ya kushindikana kufanyika uchaguzi huo wa rais mnamo mwezi Desemba mwaka uliopita.

Stephanie Williams ameliambia shirika la habari la Associated Press, kwamba inawezekana kwa wapiga kura milioni 2.8 wa nchi hiyo kupiga kura zao ifikapo mwezi Juni kulingana na mapatano ya mwaka 2020 yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Williams amewataka wabunge, ambao wanakutana katika mji wa mashariki wa Tobruk, kukubaliana juu ya mchakato unaozingatia wakati wa kupiga kura na sio mchakato usiokuwa na muda maalum.

Kwa upande wake spika wa bunge la mashariki mwa Libya, Aguila Saleh, amesema serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa sio halali hivyo ni lazima iundwe tena upya.

Lakini mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa bunge kuzingatia zaidi uchaguzi badala ya kuteua serikali mpya ya mpito.

Amesema walibya wametamka waziwazi kwamba wanataka kupiga kura ili kuichagua serikali yao ya kidemokrasia itakayowakilisha Libya yote.

DW Swahili
 
Eti mshauri maalum wa masuala ya libya,
Nchi ya watu inawahusu nini nyie wazungu?
Hembu waacheni wenyewe wachague kiongozi wamtakaye sio kuweka vibaraka wenu,
Mtaendelea kuripuliwa kila uchao
 
Eti mshauri maalum wa masuala ya libya,
Nchi ya watu inawahusu nini nyie wazungu?
Hembu waacheni wenyewe wachague kiongozi wamtakaye sio kuweka vibaraka wenu,
Mtaendelea kuripuliwa kila uchao
Wewe uliyechangia yanakuhusu nini?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom