Umoja wa mataifa na namba 666

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,411
1643262596661.png

Katika picha hapo juu unaweza kuona umuhimu wa kujua asili ya namba 666 na kwa nininamba hiyo inatumiwa na viongozi wakuu wa umoja wa mataifa. Kwa kifupi kwenye picha hiyo wapo watu 6 wakiongoza mkutano wa umoja wa mataifa na nyuma yao kuna kitambaa kilichoandikwa ‘United Nations 666’ kumaanisha kwamba umoja wa mataifa unaandaa njia ya utawala wa mnyama wa namba 666.​

Je, asili ya namba 666 ni nini? Namba 666 inatoka wapi?
Wengi wanasoma Biblia au kusikia kutoka kwenye Biblia watu wakitaja namba 666 lakini ni wachache sana wanafahamu kwamba namba 666 ilitoka wapi au kwa nini kitabu cha Ufunuo kinazungumzia kuhusu namba hiyo na kwamba iko kinyume na Mungu. Lakini pia nini maana ya namba 666?

Watu wengi wanafikiri kwamba namba hiyo ni ya shetani, Je nikweli? Hebu tuangalie kwa ufupi historia ya namba hii kwamba ilitoka wapi. Namba 666 inatokana na ibada zilizokuwa zikifanywa na watu wa Babeli wakati wakipindi cha nabii Ibrahimu na nabii Danieli. Babeli ni mji na mnara uliojengwa na Nimrodi mara baada ya gharika akiwa na makusudi makubwa mawili.

Kusudi la kwanza ilikuwa ni kuwalinda watu wa Babeli na gharika kwa kutumia mnara uliokusudiwa kufika mbinguni kwenye miungu wa angani.

Kusudi la pili lilikuwa ni kuwakusanya watu wote wakae mahali pamoja na kuwa na serikali na dini moja kinyume na mpango wa Mungu wa kuijaza nchi.

Mungu aliingilia kati na kukwamisha ujenzi wa mnara wa Babeli ingawa Nimrodi alifanikiwa kufika mbinguni kimawazo na kupata miungu 36 ambazo ni sayari na nyota.

Makusudi hayo mawili yameendelea kufanya kazi hadi leo na hivi karibuni ulimwengu wote utashuhudia serikali na dini moja ikimuabudu mungu jua ambaye alikuwa ni mungu baba wa Wababeli. Watu wa Babeli waliabudu miungu iliyotokana na utafiti wa nyota—yaani unajimu (astrology).

Hivyo watu wa Babeli wakawa na miungu ambayo ni jua, mwezi, sayari zinazoonekana pamoja na nyota walizozigundua wakati wa utafiti wa nyota. Watu wa Babeli ndio chimbuko la mwanzo wa unajimu wa nyota ambapo hata leo tunaona wanajimu wakitabiri kwa kutumia nyota.

Wababeli walitumia hesabu pia katika shughuli zao za kila siku ikiwa ni pamoja na ibada zao. Kulikuwa na jumla ya miungu 36 na mungu aliyekuwa mkuu alikuwa ni mungu jua kwa sababu alichukuliwa kuwa ndiye baba wa mimgu wote.

Wapagani wa Babeli walikuwa wakiwaabudu miungu hao kwa sababu mbalimbali kama vile kupiga ramuli, kuomba kinga na hata kutoa utabiri wa wakati ujao kwa sababu waliamini kwamba wote walikuwa ni waovu hivyo waliwaogopa miungu wao.

Watu wa Babeli waliamini kwamba namba zina nguvu kwa miungu waliokuwa wanaabudiwa. Kila mungu kati ya miungu 36 alipewa namba yake iliyotumika kumuwalisha mungu na mahali pake (Rejea Murl Vance, Trail of the Serpent, uk. 26, 27, 72).

Namba aliyopewa mungu iliwakilisha nguvu aliyonayo mungu huyo. Kwa hiyo namba husika kwa mungu iliwakilisha ukuu wake ikimaanisha kwamba mungu aliyepewa namba za awali alikuwa na nguvu kubwa kuliko aliyepewa namba za mbele.

Kwa nini kulikuwa na miungu 36? Je, namba 36 ilitokana na nini? Wababeli walipata idadi ya miungu wao kuwa 36 kwa sababu kila mungu alitakiwa kuheshimiwa au kutawala kwa mzunguko wa nyuzi 10 au digrii 10 kwa mwaka na kwa vile mwaka una siku 360 waligawa kwa 10 na kisha ikawa sababu ya kwanza kupata idadi ya miungu wao 36.

Lakini pia wanajimu au watafiti wa sayari na nyota waligundua jumla ya sayari na nyota 36 na kwa vile walikuwa wakiziabudu wakazifanya kuwa miungu wao. Ni kutokana na miungu hao 36 Wababeli walifanya hesabu na kupata namba 666 ikimaanisha mamlaka, nguvu na ukuu wa miungu wote 36.

Watu wa Babeli walihesabu miungu wao kuanzia namba 1 hadi 36 na kisha kujumlisha. Mungu wa kwanza alipewa namba 1 na mungu wa pili alipewa namba 2 na kuendelea. Mungu wa namba 1 alikuwa ni mungu jua na mungu namba 2 alikuwa ni mungu mwezi.

Miungu kuanzia namba 3 hadi 36 walikuwa ni watoto wa mungu jua ambao walikuwa ni sayari na nyota zilizogunduliwa na wanajimu wa Babeli. Ndipo wakajumlisha namba 1 hadi 36 na kupata namba 666.

Tazama hesabu hii kuhusu asili ya namba 666:
1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7 + 8 + 9 + 10 + 11 + 12+ 13 + 14 + 15 + 16 + 17 + 18 + 19 + 20 + 21 + 22+ 23 + 24 + 25 + 26 + 27 + 28 + 29 + 30 + 31 + 32+ 33 + 34 + 35 + 36 = 666

Umuhimu wa namba 36 kwa Wababeli ulisababishwa na mgawanyo wa ishara 12 zinazoitwa ‘12 Zodiac signs’ sawa na miezi 12 kwa mwaka na ishara hizo zilitokana na unajimu wa nyota na waligawa namba 36 katika mafungu matatu ya 12 Zodiac signs
12x 3 = 36.

1643263400050.png


Wababeli waliamini kwamba mtu anapokufa anakwenda kwa mungu wake. Miungu hawa 36 waliitwa kwa jina la ‘Decans’ kwa pamoja kwa sababu kila mmoja alitakiwa kufanya kazi kwa digrii 10 katika mzunguko wa Zodiac kwa siku 10 katika siku 360 za mwaka.

Kila mtu alipewa kundi lake katika ishara 12 kutegemeana na mwezi aliozaliwa na huo ukawa mwanzo wa utabiri wa maisha ya mtu kwa kutumia nyota zilizokuwa katika mafungu matatu (3) ya miezi 12 katika jumla ya miungu 36. Sayari 7 au joka lenye vichwa 7 ndilo lililotawala miungu hawa wote 36 walioitwa Decans na kati ya miungu hao aliyekuwa mtawala wa wote alikuwa ni mungu jua.

Jumla ya namba 1 hadi 36 sawa na 666 iliitwa “The Grand Number of the Sun” yaani jumla kuu ya hesabu ya jua.

Kila mungu aliwakilishwa kwa alama na wakati wa ibada kila muumini alitakiwa kuvaa hirizi inayomuwakilisha mungu wake kati ya miungu 36. Hivyo kulikuwa na aina 36 za hirizi zilizowakilisha miungu 36. Hirizi hizo zilitengenezwa kwa mfumo wa hesabu uitwao ‘6×6 Matrix’ na mtu ambaye alikataa kuvaa hirizi iliaminiwa kuwa angepata majanga ya ugonjwa, njaa, mateso na kisha kifo.
1643263563874.png

Wapagani wa Babeli walitakiwa kuvaa hirizi yenye namba na alama ya mungu mhusika. Baadhi ya Wakristo wamechukua desturi hii kwa kuendelea kuvaa misalaba shingoni ukiwakilisha alama ya mungu Ishtar.

Unaweza kuangalia picha hii mwanamke akiwa amevaa sura ya simba kichwani kumaanisha utawala wa Babeli uliowakilishwa na simba (Danieli 7:4) na amevaa hirizi shingoni yenye namba tofauti pamoja na mduara wenye jicho kifuani mwake uliowakilisha mungu jua aonaye kila mahali.
1643263834090.png

Hirizi na alama ya mungu mhusika Hirizi hizo zilitengenezwa kwa mfumo wa hesabu uitwao ‘6×6 Matrix’ (rejea jedwali la hesabu za Illuminati)


na mtu ambaye alikataa kuvaa hirizi na alama ya mungu wake iliaminiwa kuwa angepata majanga ya ugonjwa, njaa, mateso na kisha kifo. Je, mtu alipata kujua vipi kwamba mungu fulani ni mungu wake?
Watu wote waliwekwa kwenye mafungu matatu (3) ya ’12 Zodiac Signs’ kufuata mwezi aliozaliwa mtu husika na hivyo kulikuwa na makundi matatu (3) yaani kundi la kwanza watu wote waliozaliwa mwezi wa kwanza hadi wa nne, kundi la pili waliozaliwa mwezi wa tano hadi wa nane, la tatu mwezi wa tisa hadi wa kumi na mbili.

Kila kundi likiwa na miezi mitatu lilileta namba 6, yaani 1+2+3 =6 na wakaweka makundi yote matatu pamoja na kupata 666 ikimaanisha namba iliyowahusu watu wote kutokana na kuzaliwa kwao ndani ya miezi 12 ya mwaka.

Unaweza kuchunguza alama zinazotumika kwenye utabiri wa nyota utaziona zikiwakilisha ng`ombe, nge, samaki na kadhalika. Elimu hiyo ilitokana na miungu wa Babeli waliowakilishwa kwa alama na namba.

Sayari 7 au joka lenye vichwa 7 ndilo lililotawala miungu hawa wote 36 walioitwa
‘Decans’ na kati ya miungu hao aliyekuwa mtawala wa wote alikuwa ni mungu jua.

Kwa mfano kama mtu alivaa hirizi yenye namba 2 ilimaanisha kuwa mungu wake ni mungu mwezi na hivyo alitakiwa awe na alama ya mungu mwezi akiwa amevaa shingoni mwake pamoja na hirizi na kama mtu alivaa hirizi namba 1 alitakiwa kuvaa alama ya mduara iliyowakilisha mungu jua huku aliyevaa hiziri namba 6 alivaa pamoja na alama ya msalaba ikiwakilisha mungu Ishtar.

Kwa kutumia hesabu, Wababeli walifanikiwa kutengeneza jedwali lenye namba 1 hadi 36 ambapo namba hizo zikijumlishwa kwa pamoja katika kila msitari wowote unapata jumla ya 111 na kwa vile jedwali lina misitari 6 walizidisha 111 x 6 = 666.

Namba iliyoandikwa kwenye hirizi ilimpa nguvu mvaaji zilizotoka kwa mungu aliyepewa namba hiyo.
Nguvu ya mungu iliweza kuongezeka kwa kujumlisha namba ya mungu huyo na namba zingine katika msitari na kupata namba 111 na mungu alizidi kupata nguvu zaidi kwa kuzidisha 111 x 6. Namba 666 ilikuwa ni alama ya mamlaka ya miungu wote hivyo ilimaanisha kwamba ilikuwa na nguvu kwa miungu wote.

Hapa chini ni jedwali lenye namba za miungu 36 wa Babeli.
1643264264754.png

Kumbuka kwamba Wababeli walikuwa ni waabudu sanamu na hawakumuabudu Mungu wa kweli. Hata
hivyo leo pia kuna ibada nyingi ambazo chimbuko lake ni ibada za sanamu kutoka Babeli.
Jedwali la miungu 36 wa Babeli.
1643264441626.png


Zingatia kwamba namba 666 haiwezi kusimama peke yake bila kuhesabu miungu maana bila kuhesabu huwezi kupata jumla ya namba 666. Hivyo unapotaka kuielezea namba 666 lazima ufanye hesabu na kisha upate jumla yake iwe 666. Hata hivyo haimzuii mtu kutumia njia nyingine ili kupata jumla ya 666, ila jambo muhimu ni kwamba unatakiwa ujue asili ya namba 666 na kwamba ilipatikana kwa kujumlisha miungu wa Babeli na ndio maana Mungu wa Mbinguni anaihusisha namba 666 na Babeli maana chimbuko lake ni Babeli.

Kwa watu wa Babeli, mungu aliyehitimisha hesabu na kufanya jumla iwe namba 666 ndiye aliyekuwa na nguvu hata kumshinda mungu jua ambaye alikuwa ni baba wa miungu wote.

Wakati Biblia inapotuambia kwamba mnyama ana namba 666 inatuambia kwamba namba 666 ilipatikana kwa kuhesabu na kujumlisha miungu na haimaanishi kwamba namba 666 inasimama peke yake. Kama hakuna miungu itakayohesabiwa, isingewezekana kupata jumla ya namba 666.

Biblia inatuambia pia kwamba hesabu inaanzia kwa mungu wa kwanza na kujumlisha namba ya miungu wanaofuatia na mungu ambaye angehitimisha hesabu kwa kufanya jumla iwe 666 mungu huyo angeweza kuwa na nguvu zaidi hata ya mungu wa kwanza maana yeye angetumia namba 666 yenye nguvu za miungu wote.

Wababeli pia walikuwa na miungu saba (sayari 7) wa kwanza ambao ndio
walikuwa maarufu na ndio waliotumia majina ya siku kwa wiki kama ifuatavyo:

JEDWALI LA SAYARI 7 SAWA NA MIUNGU 7 YA BABELI.
Miungu Sayari/vichwa vya Joka/majina ya siku katika wiki
Jina la Sayari Jina la mungu wa Babeli Jina la siku kwa leo

Jua Shamash—namba 1 Sunday – jumapili
Mwezi Sin—namba 2 Monday- jumatatu
Mars Nergal—namba3 Tuesday- jumanne
Mercury Nabu—namba 4 Wednesday- jumatano
Jupiter Marduk—namba 5 Thursday- alihamisi
Venus Ishtar—namba 6 Friday- ijumaa
Saturn Ninib—namba 7 Saturday- jumamosi


Unaweza kuona jinsi miungu hawa wa Babeli walivyoendelea kuabudiwa hata wakati wa Ukristo maana baada ya karne nyingi kupita, wakati mtume Paulo na Barnaba walipotembelea Listra, walifanya muujiza wa kumponya mtu aliyekuwa kiwete. Watu wa mji huo walikuwa waabudu miungu wa Babeli na mara baada ya kufanyika kwa muujiza huo, watu “wakapaza sauti zao wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mfano wa wanadamu. Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji”. Matendo 14:12.

Unaposoma Biblia ya King James, jina Zeu ni sawa na Jupiter, na Herme ni sawa na Mercury. Leo sayari au madini ya Mercury yanatumiwa sana kwa ajili ya mawasiliano na ndio maana wapagani hao walimuita Paulo jina la Mercury kwa sababu yeye ndiye alikuwa mnenaji.

Ni kwa njia hiyo hata leo ibada za miungu wa Babeli zinatawala ndani ya dini nyingi na waumini wengi hawajui kwamba wanaabudu wasichokijua kama Yesu alivyomwambia yule mwanamke msamaria (Yohana 4:19-24).

Sasa, utakapofahamu kweli hii, tafadhali itikia wito wa Mungu anaposema, “Umeanguka, umeanguka Babeli….Tokeni kati yake enyi watu wangu”.
Ufunuo 18:4.


Unaweza kuangalia jinsi joka mwenye vichwa saba alivyoaminiwa na Wababeli kuwa ni miungu saba, kitu ambacho ni kweli ukilinganisha na Ufunuo 13na Ufunuo 17. Wababeli waliendelea na hesabu, wakajumlisha namba 1 hadi 3 yaani 1+2+3 = 6 na kuhitimisha kwamba namba 6 inawakilisha nguvu ya mungu baba (jua), mungu mama (mwezi) na mungu mwana (sayari ya mars). Kisha wakatumia namba 11 kujumlisha miungu namba 1 hadi 11 yaani 1+2+3+4…..+11 = 66 wakamaanisha kwamba namba 66 ina nguvu za miungu 11 wa kuanzia namba 1 hadi 11 na kisha wakajumlisha namba 1 hadi 36 wakapata namba 666 ikimaanisha mamlaka na nguvu za miungu wote.

Hapa walichukua namba 3, 11 na 36 na kuzifanya kuwa namba muhimu kwao. Biblia inatuambia kuhusu mfalme Nebukadneza wa Babeli kwamba “alifanya sanamu ya dhahabu ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa 60 na upana wake dhiraa 6…” Danieli 3:1.

Nebukadneza alitumia hesabu za miungu wa Babeli ili kutengeneza sanamu ikimaanisha kwamba alichukua miungu watatu yaani 1+2+3 = 6 kwa upana wa sanamu hiyo na kisha akazidisha kwa nyuzi 10 ya kila mungu katika mzunguko wa Zodiac signs na kisha kupata 6×10 = 60 kwa vipimo vya urefu wa sanamu hiyo.

Kwa kifupi hiyo ndiyo asili ya namba 666 ikiwa inatokana na jumla ya miungu wa Wababeli ambao walikuwa miungu 36 na ukijulisha namba zote kuanzia 1 hadi 36 = 666.

Kazi iliyopo sasa ni kutumia kanuni ya Wababeli ili tuweze kumjua mnyama
anayewakilishwa na namba 666 kwa leo maana hatimaye ulimwengu wote utamsujudia mnyama huyo badala ya kumuabudu Mungu.

LEO NIISHIE HAPA

1643264014388.png
 
Mambo mengine tunaoneana tu hapa Duniani!!yaani Mungu akamuumba malaika mkuu halafu huyo malaika akaasi akawa shetani!!akapata kiburi!!sasa tujiulize hicho kiburi na kuasi alikutoa wapi kama shetani hakuwepo kabla???yaani alipataje mawazo ya kiburi na kuasi kama shetani hakuwepo wakati huo?nani alimfundisha kiburi na kuasi kama shetani hakuwepo????

Simple tu ni kwamba Mungu alimuumba shetani ili atudanganye tukachomwe moto ndio maana yake au? Sasa huyo Mungu kwanini atutegee mtego wa maumivu?kwanini amuumbe shetani ili tudanganywe???ina Maana sisi hatupendwi na Mungu?au elimu ya dini hizi si ya kweli?maana haina mantiki kabisa!!
 
Mambo mengine tunaoneana tu hapa Duniani!!yaani Mungu akamuumba malaika mkuu halafu huyo malaika akaasi akawa shetani!!akapata kiburi!!sasa tujiulize hicho kiburi na kuasi alikutoa wapi kama shetani hakuwepo kabla???yaani alipataje mawazo ya kiburi na kuasi kama shetani hakuwepo wakati huo?nani alimfundisha kiburi na kuasi kama shetani hakuwepo????simple tu ni kwamba Mungu alimuumba shetani ili atudanganye tukachomwe moto ndio maana yake au? Sasa huyo Mungu kwanini atutegee mtego wa maumivu?kwanini amuumbe shetani ili tudanganywe???ina Maana sisi hatupendwi na Mungu?au elimu ya dini hizi si ya kweli?maana haina mantiki kabisa!!
Kamuulize mwalimu wako wa sunday school.
 
Mkuu maelezo yote ya nini, namba 666 ni namba ya mpinga Krsito kadri ya maandiko, soma kitabu cha Daniel na Ufunuo.............sasa unapojaribu kuleta maelezo mareeeefu na manamba namba ndani yake unatafuta kuwachanganya au kuwapotosha watu.
 
Mambo mengine tunaoneana tu hapa Duniani!!yaani Mungu akamuumba malaika mkuu halafu huyo malaika akaasi akawa shetani!!akapata kiburi!!sasa tujiulize hicho kiburi na kuasi alikutoa wapi kama shetani hakuwepo kabla???yaani alipataje mawazo ya kiburi na kuasi kama shetani hakuwepo wakati huo?nani alimfundisha kiburi na kuasi kama shetani hakuwepo????simple tu ni kwamba Mungu alimuumba shetani ili atudanganye tukachomwe moto ndio maana yake au? Sasa huyo Mungu kwanini atutegee mtego wa maumivu?kwanini amuumbe shetani ili tudanganywe???ina Maana sisi hatupendwi na Mungu?au elimu ya dini hizi si ya kweli?maana haina mantiki kabisa!!
Kilogic za kibinadamu Mungu achunguziki
 
Kusdma kwamba hivi karibuni tutashuhudia tukiwa na Taifa moja na Dini moja huo ni uongo, Ni Karne zijazo huko wakati huo Waislam na Wasabato wawe wameuawa wote labda, Maana hawa ndio wanatuchelewesha.
 
Maana ya 666 sio mtu wala taasisi bàli ni fedha.
Na imetoka kwenye mali alizokuwa nazo Solomoni.
Ukisoma kwenye Kitabu cha Wafalme 10:14
1 Wafalme 10:14
Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ndio talanta mia sita sitini na sita,

Baada ya Solomoni kupata mali, zikamfanya awe mbali na Mungu. Same to pesa, ukipata pesa unakuwa mbali na Mungu.

Kwa ufupi Biblia inakuongelea wewe mwenyewe, wewe ndo solomon, wewe ndo David, wewe ndo Jesus, its all about you and what state you are in.
 
Wabongo mnaumizaga vichwa bure tu na mambo yasiyo ya msingi... 666 ni namba tu, hakuna lolote la maana na hata kama lipo linawahusu wao na sioni kama linatisha
 
Kwa taarifa ya Wana JF hiyo picha hapo juu ilichukuliwa mwaka 2005 wakati wa maathimisho ya miaka 60 ya UN. Si sahihi kuihususha na 666. Kiuhalisi ni kwamba Ile nembo ya UN imewekwa kama duara kuonedha hiyo tarakimu 0.
Unapaswa kujua kanuni tatu ( 3) muhimu ambazo ndizo msingi wa freemason/illuminati:

1)Thesis x Antithesis = Synthesis;

2) Hesabu na namba za freemason; na

3)Alama na ishara za freemason.

Huwezi kuelezea freemason kwa ufasaha kama hutazingatia kanuni hizo tatu. ‘Thesis x Antithesis = Synthesis’ ndiyo kanuni inayotawala kwa freemason na kutekelezeka kwake kunategemea hesabu na namba pamoja na alama na ishara za freemason. Kwa nini wanatumia kanuni ya alama na ishara? wanasema “By symbols…is a man guided and commanded… ” wakimaanisha
kuwa “watu huamrishwa na kuongozwa kwa kutumia alama”
.

Ndio maana hata waumini wengi wanaongozwa kwa kutumia alama ama ya nyota ya pentagram, jua, mwezi au msalaba. Kwa nini wanatumia kanuni ya namba? Kwa sababu “Occultists Worship
Numbers and numbers have power”
. Hivyo kama umepungukiwa na moja ya kanuni hizo
ni wazi SIO KILA JAMBO UTAWEKEWA WAZI
 
Watu wanatafuta namna tu kujustify mawazo yao potofu
unaweza ukawa na jamii ya Illuminati na freemason wakiwa wanafanya kazi kwa majina mengine na sio majina ya Illuminati na Freemason na hapo ndipo nguvu yao ilipo. Watu wengi wameshindwa kuwatambua kwa sababu ya kujificha kwao. Kwa nini wanajificha? Kwa sababu wanajua kwamba wanachokifanya si halali na wala hakitokani na mapenzi ya Mungu. wanatumia jamii ya watu wasomi ili kufanikisha malengo yao

Unapaswa kujua kanuni tatu ( 3) muhimu ambazo ndizo msingi wa freemason/illuminati:

1)Thesis x Antithesis = Synthesis;

2) Hesabu na namba za freemason; na

3)Alama na ishara za freemason.

Huwezi kuelezea freemason kwa ufasaha kama hutazingatia kanuni hizo tatu. ‘Thesis x Antithesis = Synthesis’ ndiyo kanuni inayotawala kwa freemason na kutekelezeka kwake kunategemea hesabu na namba pamoja na alama na ishara za freemason. Kwa nini wanatumia kanuni ya alama na ishara? wanasema “By symbols…is a man guided and commanded… ” wakimaanisha
kuwa “watu huamrishwa na kuongozwa kwa kutumia alama”
.
 
Wabongo mnaumizaga vichwa bure tu na mambo yasiyo ya msingi... 666 ni namba tu, hakuna lolote la maana na hata kama lipo linawahusu wao na sioni kama linatisha
Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa (alama) katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji.”
Ufu. 14:9-10.
 
unaweza ukawa na jamii ya Illuminati na freemason wakiwa wanafanya kazi kwa majina mengine na sio majina ya Illuminati na Freemason na hapo ndipo nguvu yao ilipo. Watu wengi wameshindwa kuwatambua kwa sababu ya kujificha kwao. Kwa nini wanajificha? Kwa sababu wanajua kwamba wanachokifanya si halali na wala hakitokani na mapenzi ya Mungu. wanatumia jamii ya watu wasomi ili kufanikisha malengo yao

Unapaswa kujua kanuni tatu ( 3) muhimu ambazo ndizo msingi wa freemason/illuminati:

1)Thesis x Antithesis = Synthesis;

2) Hesabu na namba za freemason; na

3)Alama na ishara za freemason.

Huwezi kuelezea freemason kwa ufasaha kama hutazingatia kanuni hizo tatu. ‘Thesis x Antithesis = Synthesis’ ndiyo kanuni inayotawala kwa freemason na kutekelezeka kwake kunategemea hesabu na namba pamoja na alama na ishara za freemason. Kwa nini wanatumia kanuni ya alama na ishara? wanasema “By symbols…is a man guided and commanded… ” wakimaanisha
kuwa “watu huamrishwa na kuongozwa kwa kutumia alama”
.
Sasa wakiwepo shida iko wapi?
 
Ukianza kusikia stories za hiyo namba, kila mtu huwa na hadithi zake...
 
Back
Top Bottom