Sanamu ya Amani iliyowekwa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ina maana gani? Je, inauhusiano gani na utabiri wa siku za mwisho?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,856
Screenshot_20211221-180830_Chrome.jpg


Ufunuo 13:2 BHN​

Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake kama ya dubu na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu

DANIELI 7​

Wanyama wanne wakubwa

1Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wa mfalme Belshaza wa Babuloni, Danieli aliota ndoto na kuona maono akiwa amelala kitandani mwake. Aliiandika ndoto yake hii:

2“Mimi Danieli niliona katika maono usiku, pepo nne toka pande zote za mbinguni zikiichafua bahari kuu. 3 Wanyama wakubwa wanne, wakainuka kutoka humo baharini, kila mmoja tofauti na mwenzake. 4 Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, na alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikiwa namwangalia, mabawa yake yalingolewa, naye akainuliwa na kusimama kwa miguu miwili kama binadamu. Kisha, akapewa akili ya binadamu.

5“Mnyama wa pili alikuwa kama dubu ambaye upande wake mmoja ulikuwa umeinuka. Kinywani mwake alikuwa na mbavu tatu alizozishikilia kwa meno yake. Sauti ikamwambia, ‘Haya, kula nyama nyingi kadiri uwezavyo.’

6“Baada ya hayo, nilimwona mnyama mwingine. Huyu alikuwa kama chui mwenye mabawa manne ya ndege mgongoni mwake. Alikuwa na vichwa vinne na alipewa mamlaka.

7 “Kisha, katika maono yangu hayo ya usiku nikamwona mnyama wa nne wa ajabu na wa kutisha, mwenye nguvu sana. Huyu alikuwa na meno makubwa ya chuma ambayo aliyatumia kula na kuvunjavunja, na mabaki aliyakanyagakanyaga kwa nyayo zake. Alikuwa tofauti na wale wanyama wengine watatu, kwani alikuwa na pembe kumi.

8 Nilipokuwa naziangalia hizo pembe, niliona upembe mwingine mdogo ukiota miongoni mwa zile kumi. Ili kuupa nafasi upembe huu zile pembe nyingine tatu zilingolewa pamoja na mizizi yake. Ulikuwa na macho ya binadamu na kinywa kilichotamka maneno ya kujigamba.

Screenshot_20211220-214135_Chrome.jpg

Screenshot_20211220-214142_Chrome.jpg

Screenshot_20211220-214216_Chrome.jpg
 
Mwenyezi Mungu anasema ATAKUJA KUTUFUFUA na kutulipa kwa matendo yety tuliyoyafanya duniani.
Wewe hauamini?
Mwenyezi Mungu yupi!?
1. Wa wayahudi
2. Wa wakristo
3. Wa waislam
4. Wa wahindu
5. Wa wabudha
6. Wa confuism
7. Wa Taoism
Yupi unayemuongelea anakuja kufufua mifupa iliyooza na mingine decayed, imeliwa na funza!? Na kuwa mbolea.
 
Freemasons na Illuminati ni watu au sio watu!? Kama watakuwa ni watu basi, ni watu na imani yao kama wahindu, waislam, wakristo, wabudha, Wagindu nk.
Imani ya mtu ni kitu binafsi. Siwezi nikaielezea.
Wapo au hawapo? Hilo ndo swali
 
Wapo au hawapo? Hilo ndo swali
Nimekuuliza hao ni watu au siyo watu!? Mbona hujibu. Na nikaendelea zaidi kwa kukueleza kama ni watu basi hao watu wapo na wanaimani yao kama imani zingine. Kama siyo watu basi hizo ni myth. Na sipo hapa kuanza kujadili mythology.

Na kama watu wapo wa Imani zao, imani ni kitu private, I cannot judge imani ya mtu binafsi.

Bado hujaelewa!?
 
Nimekuuliza hao ni watu au siyo watu!? Mbona hujibu. Na nikaendelea zaidi kwa kukueleza kama ni watu basi hao watu wapo na wanaimani yao kama imani zingine. Kama siyo watu basi hizo ni myth. Na sipo hapa kuanza kujadili mythology.

Na kama watu wapo wa Imani zao, imani ni kitu private, I cannot judge imani ya mtu binafsi.

Bado hujaelewa!?
Sasa wewe unaamini nini?
 
Back
Top Bottom