Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.
Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.
Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.
Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
Watanzania mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu, Tunachagua tena Rais pamoja na wabunge.
Ni mwaka ambao una changamoto kubwa sana katika uchaguzi mkuu hususa upande wa visiwani
Watia nia ya kugombea nafasi za ubunge wengi wao wamesha jijua kilichobaki tu ni taratibu za kiofisi Wapinzani...
CCM YAAHIDI KUENDELEA KUHESHIMU MAAMUZI YA UMMA
02 Januari, 2020
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa, CCM mwaka 2020 itaongoza siasa safi za uchaguzi, ni mwaka wa kudhihirisha CCM inaongoza siasa safi na kuheshimu maamuzi ya Umma kama ilivyofanya mwaka 2019...
Tunakumbushana tu kwamba kwa sasa hapa nchini siasa ni ajira hivyo wabunge na madiwani tegemeeni changamoto kubwa kutoka kwa toleo jipya.
Ndio hao akina Harmonize, Diamond, Juma Kaseja, Mrisho Mpoto na wengine wengi wanaopiga jalamba muda huu.
Changamoto itaikumba zaidi CCM kwani ndio yenye...
Binafsi nimeshindwa kumuelewa kabisa huyu bwana mkubwa wa CCM.
Maneno aliyo yaongea na elimu aliyo nayo sidhani kama vinaendana.
HOTUBA YA DR. BASHIRU KWA UFUPI
CCM inatoa salamu za mwaka mpya 2020, niwahakikishie watanzania kuwa tutaongoza siasa safi,ni mwaka wa kuheshimu maoni na uamuzi wa...
Mwaka 2020 ni mwaka wa kufanya uamuzi kuhusiana na utawala na mwelekeo wa taifa letu. Huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, mwaka wa Uamuzi Mkuu. Watanzania wataitwa kutoa jibu la maswali makubwa mawili. Je, tuendelee na Rais yule yule aliyechaguliwa mwaka 2015 au tufikirie mtu mwingine? Na pili, Je...
UCHAGUZI WA MWAKA 2020: Chama cha Wananchi CUF chataka mazingira mazuri
Chama cha wananchi CUF kimetoa wito kwa Rais John Magufuli kukutana na viongozi wa Vyama vya Siasa ili kuweka mazingira mazuri ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha...
DKT. BASHIRU AZITAKA KAMATI ZA SIASA ZA WILAYA NA MIKOA KUWASILISHA MAONI
28 Desemba, 2019
Katibu Mkuu wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amezitaka Kamati za Siasa za Wilaya na Mikoa kuwasilisha maoni yao ya namna ya kuboresha maisha ya wananchi kabla ya tarehe 15 Januari, 2020...
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Mh Bashiru Ally ,
lengo kubwa la mpango huu ni kutunisha mfuko wa chama ili kupata fedha za kugharamia shughuli za chama , utaratibu huu mpya umeleta sintofahamu kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho , ambao walitegemea sare hizo kama mavazi...
Uchaguzi mkuu wa 2020 utabebwa zaidi na kura za maoni kwa wagombea wa CCM ambao Kamati kuu ndio imeshika mpini.
Jaribu kuangalia tafrani zilizoanza kujitokeza za wabunge kugawa pipi kwa wagonjwa mahututi na wengine kwenda kuutimbatimba uwanja wa Sokoine na kuwahamishia maafande wa Magereza...
Kichwa kinajieleza.
Mimi ni mtumishi wa umma, niliajiriwa 2015 June. Katika kipindi hiki cha Magufuli nimekopa fedha bank mara 3 kwa malengo tofauti.
- Nilikopa 5m. Kwaajili ya ada
- Nilikopa 3 kwaajili ya biashara ambayo ilifeli. Ilifeli kwaajili ya mzunguko mdogo (wateja hakuna). Biashara...
Kanisa la Anglikana dayosisi ya DSM limetoa Waraka wa Christmas ambao umeandaliwa na baba Askofu Jackson na kusomwa katika makanisa yote ya dayosisi hiyo.
Waraka huo umeelezea mafanikio ya Kanisa katika kuifikisha injili kwa wahitaji na changamoto zilizosalia.
Waraka umesema ili uwe kiongozi...
Ikiwa ni siku moja imepita tangu kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA na viongozi hao kupatikana, aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti na kushindwa Mhe. Cecil Mwambe amesema kuwa, ameshindwa kwenye uchaguzi huo kwa kuwa 'uwanja haukuwa sawa'.
Amesema "Mhe. Mwenyekiti...
Aliyekuwa mgombea binafsi wa urais wa Namibia Panduleni Itula, amewasilisha pingamizi la kisheria ya kupinga kushindwa kwake katika uchaguzi uliomalizika mwezi uliopita.
Itula ameitaka mahakama ya juu ya Namibia kuagiza kurejewa uchaguzi haraka iwezekenavyo, kwa madai kwamba haukuwa huru...
Kuna wakati ukivifikiria hivi vyama vya upinzani unaelewa ni kwanini CCM inaweza kuongoza hii nchi kwa namna inavyotaka.
KUB anaomba eti NEC ndio isimamie uchaguzi wa serikali za mitaa badala ya waziri wa Tamisemi.......yaani anaamini hapo ndio haki itatendeka.
Binafsi sioni tofauti kati ya...
Matokeo ya uchaguzi mkuu Chadema yametangazwa ambapo Freeman Mbowe amepata ushindi wa Tsunami. Mbowe ambaye amekiongoza chama hicho kwa miaka kumi na tano sasa alishangiliwa mno na wajumbe wakati matokeo yakitangazwa na msimamizi wa uchaguzi Sylivester Masinde.
Mbowe amepata ushindi wa asilimia...
WanaJF duniani kote,Wasalaam!
Ni asubuhi tulivu kabisa katika jiji la Dar es Salaam huku habari kubwa inayovuma ikiwa ni mkutano mkuu wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA chenye wanachama milioni 6 na nusu wenye kadi.
Kama ripota wa JF nipo hapa Mlimani City nimekesha kwa lengo moja tu la...
Kiukweli Chadema itaongozwa na wanachadema wenyewe kama ilivyo UDP ya mzee Cheyo, TLP ya Mrema, Nccr ya Mbatia na Chauma ya mzee Rungwe ambavyo vinaongozwa na wanachama wa vyama husika.
Ya ngoswe mwachie ngoswe.
Sherehe siyo yako kiherehere na masufuria na masinia cha nini?
Kwa niaba yangu...
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa, amewahakikishia wanachama, mashabiki na wakereketwa wa CCM kuwa Chama hakipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini kama ilivyofanyika miaka michache nyuma.
Ameyasema hayo...
Mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2015 amekitakia chama chake cha zamani uchaguzi mwema na kuwakumbusha kuwa zikutanapo pepo za Kaskazi na Kusi unaweza kuupata upepo wa kisulisuli.
Siasa sio uadui
Maendeleo hayana vyama!
Kiukweli uchaguzi mkuu wa Chadema kwa sasa unakwenda kimya kimya na hii ni kutokana na vikao vya kihistoria vya CCM vinavyofanyika jijini Mwanza.
Habari kuu katika media zote imekuwa ni vikao vya CCM, na hata uchaguzi wa Bavicha na Bawacha umejulikana zaidi kwa wana Ufipa wenyewe. Na hii ni...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.