Kumekucha: CCM kuwafungia Maisha wagombea watakaokutwa na hatia ya rushwa kwenye uchaguzi mkuu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,745
139,525
CCM imetoa onyo kwa wagombea wake wote wa uchaguzi mkuu kwamba yoyote atakayepatikana akitoa rushwa atafungiwa maisha yake yote kushiriki uchaguzi kupitia chama hicho.

Hii ni hatua muhimu sana katika kudhibiti wale wote wenye nia ya kununua nafasi za uongozi.

Source Mtanzania Jumapili
 
Wakati huko ndio kwny waasisi wa rushwa.

Mnyeti alionekana akitoa rushwa kwa madiwani kule Arumeru kelele zilivyopigwa akapandishwa cheo na kua mkuu wa mkoa.

Huko rushwa ndio nyumbani,kumenogaaaaa

dodge
Hakuna mwanachama yeyote wa CCM anaeingia madarakani kwa Rushwa anzia ngazi ya Mwenyekiti wa kitongozi mpaka juu wote wasafi ,hivyo hiyo kauli eti watafungiwa maisha la kwa vyama vya upinzani.CCM Safiiii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mwanachama yeyote wa CCM anaeingia madarakani kwa Rushwa anzia ngazi ya Mwenyekiti wa kitongozi mpaka juu wote wasafi ,hivyo hiyo kauli eti watafungiwa maisha la kwa vyama vya upinzani.CCM Safiiii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jana huko Darisalama nimesikia sijui Diwani labda Mwenyekiti anayetokana na CCM kakamatwa kwa Rushua? Au ni CCM ya Malawi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rushwa ndani CCM katika chaguzi ni sawa kabisa na maji na samaki, kutolewa kwa kauli hakuonyeshi uhalisia wowote, bali porojo kama tulizozoea kuzisikia kutoka kwa makada mbalimbali ktk nyakati kama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom