uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. K

    JamiiForums Tanzania Ahadi za Rais Magufuli kuhusu uchaguzi huru na haki hazitekelezeki, ni ahadi hewa kimazingira

    Hivi karibuni Rais Magufuli alipozungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na mambo mengine alitoa ahadi ya kufanyika uchaguzi huru na haki mwaka huu wa 2020 jambo lililoleta mjadala sana kwenye jamii. Hii kauli haitekelezeki kwa sasa. Hakuna mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na...
  2. Mystery

    JamiiForums Tanzania Kama Serikali imepeleka miswada kadhaa kwa hati ya dharula, kwanini isipeleke wa kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi wenye maslahi mapana kwa Taifa?

    Tunafahamu kuwa serikali yetu imekuwa "bingwa" wa kupeleka miswada kadhaa Bungeni kwa hati za dharula, swali kubwa ninalojiuliza hivi sasa ni kuwa kutokana na kilio cha mamilioni ya watanzania wanaotaka Tume huru ya uchaguzi, ni kwanini serikali hii inapata "kigugumizi" cha kupeleka muswada huo...
  3. Mystery

    JamiiForums Tanzania Ni kwanini Rais Magufuli awaogope wapinzani aliowashinda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa asilimia 99.9?

    Nimeshangazwa sana na kauli aliyoitoa Rais Magufuli wakati ajihutubia makada wenzie wa CCM kuwa wasibweteke kuwa watashinda kirahisi uchaguzi mkuu ujao, ambao unategemewa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu na akawaeleza makada hao kuwa wapinzani wana mbinu nyingi za wazi na za kificho, kwa hiyo...
  4. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika atema cheche kuhusu kauli ya Mwenyekiti wa CCM ya uchaguzi kuwa huru na haki

    Hapa ndio utaelewa kwanini Mh Mbowe ameamua John Mnyika awe Katibu Mkuu wa CHADEMA , yaani anatema madini matupu ! Mnyika amesema: "Sasa nifikishe ujumbe tu kwa Rais Magufuli, ambaye amesema yeye, akiwaambia mabalozi kwamba, uchaguzi wa mwaka 2020 utakuwa uchaguzi huru na haki ujumbe wangu kwa...
  5. USSR

    JamiiForums Tanzania GE2020 Tunaojiandaa kumpa tena kura Rais Magufuli tukutane hapa

    Ndio ni mwaka wa uchaguzi na ukweli ni kuwa ilani tuliyomkabidhi Dkt. Magufuli imeshakamilika mpaka Leo 1/1/2020 na tuone sasa ipo haja ya kukutana na kujipongeza kwa kazi kubwa aliyofanya maana haikuwa rahisi. Yeye ni mwanadamu yawezekana kuna sehemu alijikwaa na kutukwaza Ila kwa kuwa...
  6. figganigga

    JamiiForums Tanzania GE2020 Rais Magufuli: Uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki

    Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 2020 unakuwa wa amani, uhuru na haki. Kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema utakapofika uchaguzi huo, nchi na taasisi mbalimbali zitakaribishwa Tanzania kushuhudia. Ametoa kauli hiyo leo...
  7. H

    JamiiForums Tanzania Shilole: Nitagombea ubunge uchaguzi wa mwaka huu

    Mwanamziki nguli wa kimataifa na maarufu na mfanyabiashara mkubwa Tanzania Zena Yusuph Mohamed a.k.a Shilole ametangaza nia yake ya kugombea Jimbo la Igunga ambapo pia ni sehemu alipokulia kwenye uchaguzi Huu wa mwaka 2020.
  8. J

    JamiiForums Tanzania Kwa sasa hakuna Mpinzani wa kuipigania Tume Huru ya Uchaguzi waliopo wanategemea huruma ya CCM

    Kiukweli kwa hawa wapinzani tulionao Tume Huru ya Uchaguzi itaendelea kuwa ndoto hadi pale CCM itakapotupa JK mwingine wa kuanzisha mchakato wa kutengeneza Katiba mpya. Hakuna namna vyama vya upinzani vitaweza kushinda uchaguzi bila kuwa na Tume huru. Sidhani kama CCM bado ina huruma au bado...
  9. K

    JamiiForums Tanzania Zitto Kabwe adai kuna mkakati wa kumweka gerezani kabla ya uchaguzi

    Hii nimeitoa kwenye official Twitter page ya Zitto ==== Serikali ya Rais @MagufuliJP wameamua kutengeneza mashtaka ya utakatishaji Fedha dhidi yangu. Ofisi nzima ya TAKUKURU Makao Makuu imehamia Kigoma kubumba Mashtaka. Lengo ni kuhakikisha nakuwa Gerezani wakati wa Uchaguzi. CCM inatapatapa...
  10. J

    JamiiForums Tanzania Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020

    Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 CCM itatumia mbinu, mikakati na ubunifu ule ule uliotumika kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Dr Bashiru amesisitiza kuwa yeyote atakayejipendekeza kugombea udiwani, uwakilishi, ubunge...
  11. TUNTEMEKE

    JamiiForums Tanzania GE2020 CHADEMA kupoteza majimbo yafuatayo

    Kimahesabu, CCM ndio washindi wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 kabla hata ya mwenda kwenye Box la Kupigia kura. Ushindi huu wa CCM ambao umetokana na utekelezaji kabambe wa miradi mbali mbali chini ya serikali ya awamu ya tano. HESABU ZA KISIASA zinaonesha majimbo yafuatayo ya Upinzani yanakwenda...
  12. Egnecious

    JamiiForums Tanzania Dkt Bashiru: Uchaguzi sio namba uchaguzi ni uamuzi wa umma

    Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewakumbusha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini maana halisi ya uchaguzi ni maamuzi ya Umma si kama ambavyo wamekuwa wakieleza kwa kupotosha kuwa, uchaguzi ni namba. Ameyasema hayo tarehe 13 Januari, 2020 alipokuwa akihutubia...
  13. Mkaruka

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kuelekea Uchaguzi: Tafadhali wale wanasiasa wote ambao hampendi, mnateseka sana mkikosolewa au mnahisi kuvunjiwa heshima mnapokosolewa, Msigombee!

    Hello Wana JF, Tanzania ni nchi ya vyama vingi tangu 1992! Tulikubaliana wenyewe kwamba tuendeshe nchi yetu kwa taratibu za kidemokrasia kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi. Na kwa mantiki hiyo, kila mtawala anaeapa kwa mujibu wa katiba tuliyonayo anapaswa kuheshimu taratibu tulizojiwelea...
  14. Superbug

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kwanamna uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyoendeshwa je ni halali kuendelea na katiba inayozuia matokeo ya urais kupingwa mahakamani?

    Kwakweli sielewi hiki kipengele kinachozuia matokeo ya urais kupingwa mahakamani kina Nia njema ipi. Yani katika mazingira ya Tanzania ya Sasa yenye uvunjifu wa sheria zote pamoja na haki za binadamu bado kipengele kama hiki tukione kina nia njema kweli? Nitakuwa was mwisho kuamini . Vyama vya...
  15. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chadema Mh Mnyika yatikisa Kibamba, awaasa wanahabari kupigania Tume huru ya uchaguzi, Kabendera na Magoti watajwa

    Hii hapa video unaweza kuitazama mwenyewe, lakini kwa wasio na bando, Mh Mnyika leo amefika kwa mara ya kwanza kwenye jimbo analoliwakilisha la Kibamba tangu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu na kupokelewa kwa kishindo na wapiga kura wake ambapo wamempongeza kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu...
  16. Superbug

    JamiiForums Tanzania GE2020 Vyama vya upinzani msipogomea uchaguzi 2020 bila tume huru tutawashinikiza sisi wanachama

    Vyama vya upinzani chondechonde msije mkakubali kuingia kwenye uchaguzi 2020 bila tume huru. Hulka na tabia ya jiwe na serikali yake mmeshaiona hawana aibu heshima staha Wala huruma kwenu Wala hawaifwati katiba. Kama jiwe ameweza kuchezea uchaguzi wa serikali za mitaa bila kufanywa lolote Wala...
  17. Barbarosa

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu mwingine mwaka huu, Duh!

    Hawa jamaa wanajua kutupa pesa aisee, duh!
  18. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kutangazwa jijini Dodoma

    Tume huru ya Uchaguzi NEC imesema matokeo ya Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi october mwaka huu yatatangazwa kutokea jijini Dodoma. Source: Habari Leo Maendeleo hayana vyama!
  19. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Isaya Mwita ni kikwazo cha CCM kuchota Pesa ya uchaguzi kwenye Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, ndio chanzo cha kuwekewa zengwe

    Wakuu hii ndio sababu kubwa ya CCM kutaka kumuondoa Meya wa Jiji la Dar es Salaam , hakuna sababu nyingine yoyote ile. Mwita anatuhumiwa kuzuia matumizi ya zaidi bil 5 ambazo ni mgawo kutoka UDART, Je, ni matumizi gani hayo yaliyotakiwa kufanywa na kwanini yamezuiliwa ? Hakuna mwanaccm...
  20. Influenza

    JamiiForums Tanzania Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

    Kikao cha Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania cha kujadili tuhuma zinazomkabili Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita kimesimama kwa muda baada ya jina la mjumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) kusainiwa wakati hayupo ukumbini. Kikao hicho kinafanyikia ukumbi wa Karimejee jijini...
Back
Top Bottom