Gazeti la The Economist: Rais Magufuli na CCM kuendelea kushika madaraka baada ya Uchaguzi Mkuu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,759
2,000
INTELLIGENCE UNIT ni sehemu ya kitengo ndani ya Gazeti la The Economist ambacho hufanya uchunguzi na utafiti wa kisiasa na kiuchumi kwa nchi mbali mbali duniani na kutoa matokeo au matarajio.

Kitengo hiki cha kiuchunguzi kina wafanyakazi wabobezi zaidi ya 100 duniani ambao hutoa tafiti na utabiri baada ya uchunguzi kuhusu masuala ya kiuchumi kwa nchi mbali mbali kila mwanzo wa mwaka kulingana na mazingira halisi.

Ikumbukwe kuwa gazeti la The Economist limekuwa mwiba mkali hasa kwa Rais Magufuli kwa sababu linaamini sera za kisiasa na kiuchumi za Rais Magufuli zinaenda kinyume na mtazamo/msimamo wa kisiasa na kiuchumi wa gazeti hili.

Kwenye suala la kiuchumi, The Economist linaamini katika Ubinafsishaji na kuachia uchumi huru bila ya serikali kuingilia kati. Kwenye suala la kijamii, The Economist linaamini katika ndoa za jinsia moja na kuhalalisha utumiaji wa baadhi ya madawa ya kulevya kama bangi.

Ukitaka kujua msimamo wa Gazeti la The Economist kuhusu masuala ya kisiasa na kiuchumi;
GONGA LINK HII>>>Is The Economist Left or Right Wing

Hata hivyo linapofika suala la uchambuzi na utafiti, gazeti la The Economist hutoa matokeo ya tafiti na utabiri kama ambavyo jopo la wachunguzi wake limeona na kufikia hitimisho.

Kwenye masuala ya kisiasa nchini, jopo la wachunguzi wa INTELLIGENCE UNIT limesema baada ya Uchaguzi Mkuu, Rais Magufuli na CCM wataendelea sio kutawala tu bali pia watahodhi kwa kiwango kikubwa madaraka ya nchi. Kutakuwa na utulivu wa kisiasa kuanzia 2020-2023 huku CCM ikiendelea kujiimarisha zaidi kutokana na udhaifu na kudhoofika kwa vyama vya upinzani.

Kwenye masuala ya kiuchumi limesema pamoja na kwamba serikali ya Rais Magufuli imeonesha mipango na nia ya kuboresha uwajibikaji katika sekta za umma na kuboresha maisha ya wananchi lakini itakabiliwa na uwezo mdogo kifedha.

INTELLIGENCE UNIT imebainisha kuwa, kutokuwa na utungaji sera ulioeleweka nchini kutawafanya wawekezaji kuogopa kuwekeza nchini, hata hivyo matarajio kwa nusu ya mwaka yanaonekana kuwa imara kutokana na kukua kwa sekta ya utoaji huduma nchini na uwekezaji kwenye miundombinu kitaifa.

Ukitaka kusoma repoti yote;
GONGA LINK HII>>>ENTELLIGENCE UNIT: Tanzania political and economic forecast

Screenshot (36).png
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,759
2,000
Nadhani huu utafiti na angalizo la hili gazeti umewafanya viongozi wetu wa upinzani kuingiwa na hofu/wasiwasi na kuanza kutafuta nguvu za kisiasa na kiuchumi kutoka nje ya mipaka ya nchi!

Hii sentesi ya INTELLIGENCE UNIT isemayo, ‘’Under the leadership of John Magufuli, the long-standing ruling party, the CCM, will retain a firm grip on power’’, imetoa ujumbe ambao vyama vya upinzani kama havitajipanga vizuri kuna uwezekano wa kujikuta bunge lina idadi ndogo sana ya wabunge wa upinzani na pia halmashauri za miji na Majiji zikiangukia kwenye mikono ya CCM!

Sio ajabu kuona kwa sasa viongozi wetu wa upinzani wanashindana kwenda nje ya nchi kutafuta msaada wa kisiasa na kifedha!
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,469
2,000
MsemajiUkweli,
Labda kwa vile hizi ni forecast za jarida maarufu sasa ndio hawa Wapinzani watasikia, lakini kuna akina sisi, forecast tumeanza kutoa tangu hajaapishwa...


P
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,230
2,000
Hizi zinaitwa, Tanzania political trends for 2020 and beyond…
Hilo gazeti lilichokifanya pamoja na kuwa halimpendi Magufuli LINALENGA kuwaonya wafadhili wa nchi zao kuwa wasiingie mkenge kuwachangia pesa upinzani walioanza kujipitisha pitisha huko nje ya nchi kwenye nchi zao kuwa ni matapeli wala hawana nia ya kushinda wanawinda pesa tu dakika hizi za majeruhi wazitafune kuelekea uchaguzi mkuu

LInatoa warning signals
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,759
2,000
Hilo gazeti lilichokifanya pamoja na kuwa halimpendi Magufuli LINALENGA kuwaonya wafadhili wa nchi zao kuwa wasiingie mkenge kuwachangia pesa upinzani walioanza kujipitisha pitisha huko nje ya nchi kuwa ni matapeli wala hawana nia ya kushinda wanawinda pesa tu dakika hizi za majeruhi wazitafune kuelekea uchaguzi mkuu

LInatoa warning signals
Gazeti pia linatoa ujumbe kwa wapinzani kuwa wajiandae kwa ''mafuriko ya kisiasa''!
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,333
2,000
Itakuwa hivyo kwa sababu tume ya uchaguzi ni ya ccm by 100% na vyombo vya usalama pia ni sehemu ya hiyo tume.

Ila swala lisiwe ccm kurudi madarakani swala liwe je, kurudi kwao madarakani kunaisaida nini watanzania, hilo ndilo swala la msingi.

Wako madarakani kwa karibu miaka 60 sasa lkn still the country has nothing to show in development terms, zaidi ya nusu ya watanzania wanaishi ktk ufukara wa kutupwa hivyo kuwa kwao madarakani hakuna chochote positive kwa nchi. Ni bure kabisa.
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,736
2,000
MsemajiUkweli,

Swala la idadi ndogo ya wabunge wa upinzani me sitaki kuamini Coz kila uchaguzi huwa tunahisi hivyo na matokeo yake ndio kwanza wanajaa,

Me nadhani watanzania wanawaamini sana upinzani kwenye ubunge kuliko kwenye urais

Na la urais linakuwa gumu sana hasa kwenye kuunda serikali bcoz upinzani hawana watu ambao wanaweza kusema wanaunda serikali
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,759
2,000
Nyanjomigire,
Gazeti la The Economist halijasema lolote kuhusu uhalali/muundo wa tume ya Uchaguzi lakini una haki ya kuwa na mtazamo wako! Kumbuka mtazamo wako hauwezi kuondoa angalizo la gazeti la The Economist kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu.

Labda tujiulize, kutorudi kwao CCM madarakani kutasaidia nini Watanzania? Ni chama gani kitaziba nafasi ya CCM baada ya kutorudi madarakani?

Ni kweli, hakuna lolote lililofanywa kwa zaidi ya miaka 60 kwa mtu ambaye akili ya kawaida (common sense) ni bidhaa adimu katika ubongo wake!
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,469
2,000
‘’Under the leadership of John Magufuli, the long-standing ruling party, the CCM, will retain a firm grip on power’’.
This is very true, not only CCM will retain a firm grip on power, but for a long time to come, in facts, CCM Itatawala Milele, anayebisha abishe tuu for the sake of kubisha, unless ni kwa msaada wa watu wa Marekani!.
P
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,759
2,000
Swala la idadi ndogo ya wabunge wa upinzani me sitaki kuamini Coz kila uchaguzi huwa tunahisi hivyo na matokeo yake ndio kwanza wanajaa,

Me nadhani watanzania wanawaamini sana upinzani kwenye ubunge kuliko kwenye urais

Na la urais linakuwa gumu sana hasa kwenye kuunda serikali bcoz upinzani hawana watu ambao wanaweza kusema wanaunda serikali
Kuna sehemu ndani ya maoni yako ninakubaliana nawe lakini pia sehemu nyingine sikubaliani nawe.

Ni kweli kwenye Urais wa Tanzania haina mjadala! Labda Urais wa Zanzibar!

Kumbuka Wabunge na madiwani wengi wa upinzani walishinda kwa sababu ya CCM kuvuruga mchakato wao wa ndani katika kuwapata wagombea kwa tiketi ya CCM. Kama CCM watajirekebisha katika mchakato wa kuwapata wagombea basi wapinzani watakuwa na wakati mgumu sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom