NEC: Ratiba ya Uchaguzi Mkuu haijatoka

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1581508006897.png

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haijatoa wala kutangaza ratiba yoyote ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2020.

Taarifa iliyotolewa na NEC kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, utaratibu wa tume ni kupanga ratiba ya Uchaguzi mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tukio ambalo bado muda wake haujafika.

Ufafanuzi huo wa NEC umetolewa kufuatia kuwepo kwa taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zinazopotosha taarifa ya tarehe ya kufanyika kwa Uchaguzi huo.

NEC imewaomba wananchi kupuuza taarifa ya tarehe ya kufanyika kwa Uchaguzi zinazosambazwa katika mitandao hiyo kwa kuwa si rasmi, na kwamba kitendo hicho kinafanyika kwa nia ovu.

Kwa mujibu wa NEC, ratiba ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu itatolewa muda utakapowadia kulingana na matakwa ya kisheria.

Chanzo: TBC
 
Tatizo la wananchi sio tarehe ya uchaguzi. Sisi shida yetu ni uchaguzi huru na wa haki basi.
Mku wale ni chama kimeshajijenga miaka mingi sana. Unaweza pata tume huru na bado wakashinda uchaguzi sasa sijui utakasilikia hiyo tume huru?
 
Kuna watu Neno tume huru liko midomoni mwao lakini hawajui maana ya tume huru kisheria


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Washenzi wakubwa chezeeni uchaguzi mwaka huu watanzania wachomane Tanzania Iwekewe vikwazo na Marekani maana ndicho mlikuwa mnakitafuta miaka mingi mwaka huu ICC inawahusu.
 
Ninafikiri uchaguzi hata ukifanyika kesho bila tume huru mtashiriki neki na wagombea wenu mnaowajua.
Watanzania hawautaki utaratibu wa taasisi yenu jinsi inavyopatikana na namna inavyotenda kazi na kuwajibika kwake.
Watanzania wanataka utaratibu wa kupatikana kwa chombo chenu uwe huru na kwa hivyo itapelekea kutoa maamuzi ya haki katika chaguzi nchini.
Ikiwa mnaridhia 'watanga wa nyika' wamwage damu kwa manufaa yenu na watu wenu,mfahamu kabisa ICC inawasubiri-Muwe ofisini au kokote mtakopokuwa!
Mwenye ufahamu na afahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu Neno tume huru liko midomoni mwao lakini hawajui maana ya tume huru kisheria


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kisheri tunajua lakini tunataka tume itokane na uwakilishi wa vyama vya siasa , sio tume inayoteuriwa na mwenyekiti wa chama kimoja cha siasa
 
Back
Top Bottom