uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Mystery

    JamiiForums Tanzania GE2020 Rais Magufuli heshimu maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura kwenye Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu

    Miongoni mwa mambo yanayowatia sana wasiwasi wananchi katika kipindi hiki ni Uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Ingawa Rais Magufuli umetoa uhakikikisho kwa Jumuiya ya kimataifa kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na haki, lakini maneno na vitendo vya viongozi...
  2. The Assassin

    JamiiForums Tanzania GE2020 Uchaguzi Mkuu mwaka huu unawatesa sana CCM

    Uchaguzi wa mwaka huu unawatesa zaidi CCM kuliko upinzani. CCM wanateseka hasa kuhusu idadi ya wapiga kura watakaojitokeza kupiga kura hasa ukizingatia kua uchaguzi wa serikali za mitaa ilibidi itumike nguvu ya ziada ya wakuu wa wilaya kutisha wanachi kwenda kupiga kura na kutishia kuwakataa...
  3. K

    JamiiForums Tanzania Bila kuchelewa, Serikali ya Tanzania ijipambanue kupata uchaguzi huru na haki ili kuondoa upotoshaji

    Kwanza naomba Mods, uzi huu usiunganishwe na nyengine. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kauli mbali mbali kuhusu Madai ya tume huru ya uchaguzi Tanzania. Si vyama vya upinzani tu lakini hata wadau wa maendeleo na demokrasia wamesikika wakihimiza kwa serikali kuleta tume huru ya uchaguzi...
  4. J

    JamiiForums Tanzania Prof. Kabudi: Uchaguzi mkuu utakuwa Huru na Haki kama ilivyokuwa miaka yote Jumuiya ya kimataifa msiwe na wasiwasi

    Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi ameihakikishia Jumuiya ya kimataifa kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuwa huru na wa haki hivyo wasiwe na wasiwasi. Prof Kabudi amesema bunge limeboresha sheria ya vyama vya siasa ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wanasiasa. Kabudi...
  5. Ossaessa

    JamiiForums Tanzania Nini faida na hasara ya Tume ya Uchaguzi?

    Salam wana JF Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wananchi, wanasiasa, viongozi wa dini, taasisi mbalimbali pamoja na baadhi ya Viongozi wastaafu kutaka iundwe Tume Huru ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, 2020. Upande wa pili kumeibuka kundi linalopinga uwepo wa Tume Huru ya...
  6. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Tume ya Uchaguzi tunaomba ufafanuzi kwenye hili

    Huyu mtu mmoja kwanini ana vitambulisho viwili ?
  7. K

    JamiiForums Tanzania Hofu ya uchaguzi ujao: Nadharia kuu ya hama hama ya wapinzani maslahi

    Habari iwe nanyi wakuu! Kwanza niseme wazi kuwa hakuna jambo kubwa katika maisha kama kujitambua, kutambua utu na thamani yako. Mtu anayejitambua na kutambua utu wake hata akiwa na njaa kiasi gani hawezi kula chakula kilichopakwa mate na mtu aliyeshiba. Kama atafanikiwa kukishika atakirusha...
  8. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Sheikh Alhad Salum wa Bakwata asema litakuwa jambo Jema kama itapatikana Tume Huru ya uchaguzi 2020 ili kulinda amani

    Shehe wa mkoa wa Dsm, Alhad Salum amesema amani yetu ni tunu ya Taifa hivyo ni jambo jema kabisa kama itapatikana Tume huru ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu ie 2020. Sheikh Salum ametoa maoni katika mahojiano ya waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wa dini akiwemo Katibu...
  9. Miss Zomboko

    JamiiForums Tanzania Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani: Aliyekuwa mshauri wa Trump ahukumiwa miezi 40 jela

    Roger Stone, aliyekuwa mshauri wa Rais wa Marekani, Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi ambaye jina lake lilitajwa wakati wa kesi ya Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka 3 na miezi 4. Uamuzi kuhisiana na kesi zilizokuwa zikimbali Stone umetolewa katika mahakama jijini Washington...
  10. B

    JamiiForums Tanzania Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaongeza siku za kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

    Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeongeza siku tatu za zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Zoezi hilo lililokuwa lifikie tamati leo kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani sasa litafikia tamati Jumapili February 23 Mwaka huu. =====...
  11. T

    JamiiForums Tanzania Tume Huru ya Uchaguzi itaundwa pale tu CHADEMA na wapinzani kwa ujumla watakaposusia Uchaguzi Mkuu 2020

    Kabla ya uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, nilipost uzi unaosema kuwa CCM wameweka mapandikizi yao yagombee lakini niliishia kupigwa BAN ya miezi mitatu na hawa moderator mpaka uchaguzi ukaisha bila bila. Sasa leo nawaambia hivi, CHADEMA na upinzani kwa ujumla mnatakiwa kutoa tamko la...
  12. T

    JamiiForums Tanzania Msifadhaike kabisa kipyenga kikilia tu wengi watakuja upinzani tila lila

    Mimi ni wa Kijijini na ninatolea mfano kwa mazingira ya huku kwetu Idukilo-Kishapu-Shinyanga. Watu wanafadhaiiiiikaaa eti sijui nani karudi au kaenda kwenye LiChama Tawala na upinzani unazidi kuchoka ! Walaaaaa! Sio hivyo kabisa! Upinzani utakuwa kwa asilimia kubwa sana Mwaka huu - subiri...
  13. M

    JamiiForums Tanzania Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

    Kupitia matangazo ya moja kwa moja yanayoendelea ya channel 10, imemuonesha aliyekuwa Katibu Kkuu wa CHADEMA, Dkt. Mashinji akiingia ofisi hizo akiwa akiwa amevalia nguo za CHADEMA tayari kwa kuijiunga na CCM. Anaeleza baada ya kutafakari kwa kina amebaini CHADEMA haina utayari wa kuleta...
  14. Kichuguu

    JamiiForums Tanzania USA: Uchaguzi 2020

    Mbio za uchaguzi wa wa marekani kumchagua rais, wabunge congress wote 435 na maseneta 35 kati ya 100 zimeanza kuwapa nguvu bainba ya Democrats na Republicans. Kwa sasa hivi Democrat ina wabunge 232 wakati republican inao 197; kwa jumla Democrat imeposhateza mbunge mmoja aliyehama kuwa...
  15. Tulimumu

    JamiiForums Tanzania Kampeni za kujiandikisha na kuboresha daftari la wapiga kura: Kutakuwa na uchaguzi au ni yale yale ya serikali za mitaa?!

    Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana watu walihimizwa kwenda kujiorodhesha kwaajili ya uchaguzi huo. Baada ya kujiorodhesha kukatokea kituko cha karne ambapo wagombea wa upinzani zaidi ya asilimia 99 waliondolewa kwenye kinyang'anyiro na wale wa chama tawala kutangazwa kuwa...
  16. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Sheikh Ponda: Zanzibar itakuwa ni mlango wa kuvunjika amani uchaguzi mkuu 2020

    Katibu Mkuu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania sheikh Issa Ponda amedai kuwa kuna wazanzibar wengi hawajaandikishwa kwenye daftari la wapiga kura kinyume cha utaratibu. Ponda amesema kwa Siasa zinazoendelea Zanzibar kwa sasa ni wazi kabisa kama amani itavunjika wakati wa uchaguzi basi mlango wake...
  17. J

    JamiiForums Tanzania Waitara: NEC ni Tume Huru ya uchaguzi, 2015 niligombea ubunge kupitia CHADEMA Tume Huru ikanitangaza mshindi

    Naibu waziri. wa Tamisemi Mwita Waitara amesema NEC ni Tume huru ya uchaguzi, watakaosusa wasuse lakini wengine watakula. Source: Malumbano ya Hoja mubashara
  18. YEHODAYA

    JamiiForums Tanzania Mbatia asema NCCR lazima watashiriki Uchaguzi Mkuu

    Akiongea na vyombo vya habari na taarifa ya habari ya ITV Mbatia katofautiana na wenzie wanao Lia Lia katiba mpya Sijui na tume huru Yeye kasema NCCR itashiriki na haiungani na wengine wanaopinga Na imejipanga kuweka wagombea nchi nzima Ikumbukwe kuwa yeye ndie makamu mwenyekiti wa UKAWA Ina...
  19. beth

    JamiiForums Tanzania NEC: Ratiba ya Uchaguzi Mkuu haijatoka

    Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haijatoa wala kutangaza ratiba yoyote ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2020. Taarifa iliyotolewa na NEC kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, utaratibu wa tume ni kupanga ratiba ya Uchaguzi mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa...
  20. MsemajiUkweli

    JamiiForums Tanzania Gazeti la The Economist: Rais Magufuli na CCM kuendelea kushika madaraka baada ya Uchaguzi Mkuu

    INTELLIGENCE UNIT ni sehemu ya kitengo ndani ya Gazeti la The Economist ambacho hufanya uchunguzi na utafiti wa kisiasa na kiuchumi kwa nchi mbali mbali duniani na kutoa matokeo au matarajio. Kitengo hiki cha kiuchunguzi kina wafanyakazi wabobezi zaidi ya 100 duniani ambao hutoa tafiti na...
Back
Top Bottom