COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
753
3,096
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.

Vifo vingine 6 vya wagonjwa COVID-19 vimeongezeka na kufanya jumla ya vifo kufikia 16 Tanzania, wagonjwa waliopona wamefikia 167. “uzushi wa kwamba kila kifo ni cha corona sio sahihi kuna magonjwa mengine yanayoua”

Waziri Mkuu akinukuliwa, amesema...

''Kuanzia Aprili 23 - Aprili 28,2020 tumepata wagonjwa wapya wa Corona 196 ambapo kati ya hawa Bara wapo 174 na Zanzibar 22 ambao Waziri wa Afya Zanzibar ameshawatangaza, hii inafanya jumla ya visa vya Corona Tanzania kufikia 480 kutoka 284 ambavyo vilitangazwa Aprili 22''

















-------------
Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amesema kuwa, Watu waliokamilisha siku 14 na kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na kuonekana hawana virusi vya corona wameruhusiwa kurudi nyumbani.

Hadi tarehe 28/04/2020 watu 644 waliruhusiwa, na watu hao ni kutoka mikoa ya Zanziba, Dar es salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Songwe, Kagera, Kigoma, Mwanza,Kigoma na Dodoma.

Watu hawa walikuwa wamefikisha siku 14 hivyo wameruhusiwa kurudi nyumbani na wanayo matumaini wale ambao wanaendelea kufatiliwa ambao pia hawakupatikana na maambuzi nao wataruhusiwa kutoka katika karantini.

Amesema kuwa, mikoa aliyoitangaza ni ile ambayo ipo pembezoni hii ikiwemo na watu ambao wanaotoka nje na kuingia ndani na kuwaweka karantini kama vile kule HoloholoTanga, Sirari Mara, Kagera na maeneo mengine.

Lakini pia amesema, katika kipindi hiki wameshuhudia upotoshaji mwingi unaoendelea kutoka kwa watu wasio na matendo mema hivyo wameepuka watu kutoa takwimu ambazo sio sahihi ambazo zimekuwa zikileta mtafuruko kwa jamii usio kuwa wa lazima.

Amesema kuwa " na mimi nataka nieleze tu kwamba uzushi wa vifo na kwamba kila kifo kimekuwa ni kifo cha corona sio sahihi sana, tunasahau kuwa kuna magonjwa mengine ambayo yanaua pia, tunajua tuna magonjwa kama vile BP, maralia, kisukari, UKIMWI na magonjwa mengine pia mbayo yanaua pia"

Ameongeza kuwa "Kwa hiyo idadi ya wanaokufa tuwaachie madaktari watuambie, badala ya kila mmoja kuwa anaweza kusema kila anachokiona yeye, kwa hiyo tuache tabia ya kupotosha umma tuwaache watalaam wetu waendelee na kazi yeo na watupe taarifa ili sisi tuwafikishie".

Amesema jukumu lao bado lipo pale pale la kuhakikisha kwamba serikali inasimamia afya ya watanzia kwa utaratibu ambao unaweza kutufikisha mahali.
EWxPicBXsAE5sQ4.jpg
EWxPjUtXYAIICJY.jpg
 
Duuuuh! Tunaongoza EA kwa sasa! Wacha tu nchi majirani watutenge maana tunasambaza hili gonjwa makusudi sasa! Kama hatuchukui hatua proven na WHO na wataalamu wabobezi maana yake tunafanya makusudi mazima kulisambaza!

Hiki kiburi sijui kinatoka wapi! Ewe Mola wetu tuepushe na balaa hili.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.
Kuna uwezekano hizi data zimechakachuliwa...

Chukua figure yao then zidisha kwa factor ya 1.40 ili kupata data kamili...

480*1.4 = 672.

Kwangu mimi hili ndilo jibu sahihi.
 
Back
Top Bottom