Uchaguzi 2020 Harakati za uchaguzi mkuu 2020 majimboni, Ukerewe, Mwanza

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,891
1,211
Habari wana bodi,

Baada ya makala kadhaa za harakati za viongozi na vigogo katika awamu hii ya 5 jimboni Iramba leo macho yangu nayaelekeza Jimboni Ukerewe, hili n jimbo toka mkoa wa Mwanza, ni miongoni mwa visiwa vinavyounda mkoa wa Mwanza.

Ukerewe pamekuwa na mageuzi makubwa kisiasa kwa kuwa miongon mwa majimbo machache sana Tanzania ambayo hayajaruhusu mbunge wake kutumikia zaidi ya awamu tatu, toka alipokuwa mbunge ambae alikuja kupata bahati ya kuwa Speaker wa Bunge la JMT Ndugu pius Msekwa, akaja Balozi mama Getrude Mongela aliewah kuwa spika wa Bunge la africa ye huyu alihudumu vipindi viwili tu, akaja bwana Machemli huyu alihudumu kipindi kimoja tu akiwa mpinzani toka Chadema, baadae akaja huyu mbunge aliepo Mh Mkundi ambae alipata ubunge akiwa Mpinzani(Chadema) lakini baada ya biashara ya wanasiasa akahamia chama tawala na kuongoza jimbo akiwa mbunge halali wa CCM.

Swali linakuja, je atapewa tena ridhaa na Wakerewe ili aendelee kuwaongoza kwa awamu ya pili? Je wana CCM waliowekeza Nguvu na akili zao pale jimboni wataruhu ye aendelee kuongoza ilihali hakuwahi kuwa mwana CCM ndaki ndaki? Maswali yatajibiwa wakati muafaka ukifika.
Ukerewe imebahatika kuwa na viongozi wengi na wasomi mashuhuri waliowah kuwepo Tanzania, hivo ilitakiwa kuwa miongoni mwa wilaya za mfano wa kuigwa hapa Tanzania lakini imekuwa kinyume chake, sasa wasomi na watu wote toka Ukerewe ni wakati wenu sasa kufanya maamuzi sahihi ili kuivusha wilaya toka shimoni.

Wana ukerewe na wapenz wa siasa za ukerewe mnakaribishwa kutoa ushauri wa ni nan hasa mnahis atawafaa kuwaongoza katika uchaguzi mkuu ujaoo. Hapa nina baadhi ya majina ya wanaosikika/wanaombwa kuiongoza wilaya hiyo ilio kisiwani, Dokta Meru(katibu mkuu mstaafu), Mkundi(mbunge aliepo madarani, A.Nyarubamba(Mkurugenzi mstaafu na afisa kilimo wilaya ya Uk, Deo Ryato(TFF), Makene(msomi toka SUA, E. Kabaka (Mwalimu chuo kikuuu) na wengneo wengi.......
 
ukerewe ni kama kigoma mjini.udhaniavyo ndivyo kumbe sivyo.kuna majimbo yanajulikana kabisa ni ya upinzani na kuna majimbo ni chama tawala piga ua ila ukerewe ni kuzungumkuti.mtu au chama chochote kinaweza ibuka na ushindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukerewe ni kama kigoma mjini.udhaniavyo ndivyo kumbe sivyo.kuna majimbo yanajulikana kabisa ni ya upinzani na kuna majimbo ni chama tawala piga ua ila ukerewe ni kuzungumkuti.mtu au chama chochote kinaweza ibuka na ushindi

Sent using Jamii Forums mobile app
ok nakubaliana nawewe ndugu, make hakuna mbunge aliepitisha awamu zaid ya mbili.
 
Back
Top Bottom