Waraka namba moja wa NCCR-Mageuzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020. NCCR Mpya inakuja!

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Wakuu,

Huu ni Waraka namba moja wa chama. Bado ntaweka hapa namba mbili. Na nitakuwa na-update kila kinachojiri.

Sisi tunahukumiwa kwa lipi? - Ndugu James Mbatia

“Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu” Methali hii inajidhihirisha, kumezuka shutuma kubwa dhidi yetu ya kile wanachokiita usaliti. Mara baada ya kupokea viongozi wa vyama na wanachama mbalimbali kutoka katika vyama vyao na kujiunga na chama chetu cha NCCR-Mageuzi.

Hayo yote yanaibuka baada ya kuona wimbi kubwa la watu wanaimba wimbo wa UTU, UTU, UTU.

Kuhama chama kimoja na kwenda kingine si jambo geni ulimwenguni kote ikizingatia kila mmoja ana haki na uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa anachokipenda. Lakini pia NCCR-Mageuzi hapo nyuma ilipoteza wanachama wengi waliohamia kwenye vyama hivyo hivyo ambavyo leo wanatuita wasaliti na sisi hatukuwahi kulalamika".

IMG-20200428-WA0023.jpg

IMG-20200428-WA0022.jpg

IMG-20200428-WA0020.jpg

IMG-20200428-WA0026.jpg

IMG-20200428-WA0021.jpg
 
Mlejesho,,kama hawawezi kuandika kiswahili vizuri,,je wakipewa nchi hiyo mikataba si itakuwa kituko cha karne?
 
NCCR wanapiga hesabu za kijinga kweli, yaani wanategemea kubebwa na JPM?
Hawajui kuwa yeye mwenyewe anapumulia machine uchaguzi huu ujao? Ndani ya chama chake mwenyewe hali in ngumu na nje no ngumu zaidi. Na baada ya corona hii sijui hasira za wananchi kwenye sanduku LA kura itakuwaje.
 
Nccr mageuzi kazi ya kwanza ni kufuta zile siasa za uongo za Chadema

Nyie mna wasomi Wengi tunawaamini
 
Hivi kweli Mbatia alivyo makini anaweza kuandika lugha yenye matege namna hii ? Mbona mbatia yupo fasaha sana kwa Luhga ya kiswahili ? maneno kama 'yaliyojili' au mlejesho hayafanani kabisa na Mbatia.Au ameandikiwa na yeye akasaini tu ?
 
tapatalk_1588071371291.jpeg


Isomwe kwenye jalada

Tulisema Chadema mwisho wenu unakaribia kutokana na siasa zenu za kibabe, dharau, matusi

Haya sasa wenye kuipenda Tanzania wanawakimbia
 
NCCR wanapiga hesabu za kijinga kweli, yaani wanategemea kubebwa na JPM?
Hawajui kuwa yeye mwenyewe anapumulia machine uchaguzi huu ujao? Ndani ya chama chake mwenyewe hali in ngumu na nje no ngumu zaidi. Na baada ya corona hii sijui hasira za wananchi kwenye sanduku LA kura itakuwaje.
Jitie moyo mkuu!!
 
Back
Top Bottom