Mradi wa REA umeipatia CCM kura 50% kabla hata ya uchaguzi

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kitendo cha serikali ya rais John Pombe Magufuli kuongeza pesa nyingi na kuwepo na usimamizi mzuri wa mradi wa REA tayari chama cha mapinduzi kimeshajizolea kura kwa 50% za urais hata kabla ya uchaguzi.

Hii ni kwa sababu mpaka sasa ni 72% ya vijiji hapa Tanzania vimeshawekewa umeme. Nyumba za makuti, nyumba za tembe zinawaka umeme tena kwa bei rahisi kabisa ya 27000. Ikumbukwe kuwa hii ni kwa sababu JPM alipoingia madarakani alisema lazima atekeleze ilani ya CCM ya kupeleka umeme vijijini bila Tanzania nzima.

Napita barabara ya Old Shinyanga naelekea Shinyanga nashangaa kuona nyumba za tope na tembe zote zina umeme.

Kwa hili lazima tumpongeze JPM na chama chake na tutambue maendeleo hayana vyama.
 
CCM Mpya imefeli, ilidhani miradi mingi mikubwa kutekelezwa kwa wakati mmoja itawa boost kiSiasa.

Lakini mpaka sasa miradi hiyo ya ndege ATCL, Reli SGR , Stiegler's Gorge, REA bila umeme, madaraja na flyovers n.k haijakamilika kwa wakati waliotegemea hata kwa 'vipande' sasa hawana cha kuwaonesha waTanzania ktk miaka 5 wamekamilisha kitu gani.
 
Mapambano dhidi ya corona yanaiondolea CCM hizo 50% ya kura, wamefeli totally!

Ngoma imerudi 0% tutafute hoja nyingine ya kuzipandisha tena!
 
Mapambano dhidi ya corona yanaiondolea CCM hizo 50% ya kura, wamefeli totally!

Ngoma imerudi 0% tutafute hoja nyingine ya kuzipandisha tena!
Unajidanganya maana mradi kama JNHPP unaendelea na mkandarasi ameshalipwa certificate kama 6 zenye thamani ya tril 1.2+
 
CCM Mpya imefeli, ilidhani miradi mingi mikubwa kutekelezwa kwa wakati mmoja itawa boost kiSiasa.

Lakini mpaka sasa miradi hiyo ya ndege ATCL, Reli SGR , Stiegler's Gorge, REA bila umeme, madaraja na flyovers n.k haijakamilika kwa wakati waliotegemea hata kwa 'vipande' sasa hawana cha kuwaonesha waTanzania ktk miaka 5 wamekamilisha kitu gani.
Rea mpaka 72% vijiji vina umeme, Sgr Dar to Moro imebaki kidogo sana mvua na milima inasumbua. Ndege nane zimeshanunuliwa. Ubungo interchange imekamilika 98%. Mimi nipo Nccr Mageuzi lakini kweli nitasema, Jama amepiga kazi.
 
Miaka 60 ya uhuru leo hii ndo mnapeleka umeme vijijin mlikuwa wap miaka yote hiyo? Vp kuhusu hizo nyumba za udongo zinamanisha nn? Hii nchi bwana Wakt leo hii kuku wa kisasa wanalala kwenye mabanda yalijenga vizr na kuezekwa na mabat lakn wananch wanalala kwenye nyumba za matope WTF
 
Nini maana ya maendeleo? Miradi ndio maendeleo na ndio kura zenyewe.

Narudia tena, kama miradi ndio inayotoa kura, leo hii bado weupe huko Afrika wangekuwa madarakani. Hivi wanavyofanya ccm leo, huko Afrika kusini walifanya miaka mingi sana, tena mara mia yake.
 
Kitendo cha serikali ya rais John Pombe Magufuli kuongeza pesa nyingi na kuwepo na usimamizi mzuri wa mradi wa REA tayari chama cha mapinduzi kimeshajizolea kura kwa 50% za urais hata kabla ya uchaguzi.

Hii ni kwa sababu mpaka sasa ni 72% ya vijiji hapa Tanzania vimeshawekewa umeme. Nyumba za makuti, nyumba za tembe zinawaka umeme tena kwa bei rahisi kabisa ya 27000. Ikumbukwe kuwa hii ni kwa sababu JPM alipoingia madarakani alisema lazima atekeleze ilani ya CCM ya kupeleka umeme vijijini bila Tanzania nzima.

Napita barabara ya Old Shinyanga naelekea Shinyanga nashangaa kuona nyumba za tope na tembe zote zina umeme.

Kwa hili lazima tumpongeze JPM na chama chake na tutambue maendeleo hayana vyama.
Hizi chaguzi duniani zina matatizo; nilitegemea mlipa kodi mkubwa kwenye kura angekuwa na kura nyingi kuliko yule mkulima anayelima chakula chake pekee. Shareholders wa makapuni kila mmoja ana nguvu kulingana na idadi ya shares sasa iweje mtu anayechangia zaidi gharama za uendeshaji wa serikali awe sawa na mtu tegemezi anayelishwa na wazazi au ndugu inapokuwa suala la kupiga kura? .........mnisamehe mchana umepita hivi hivi
 
Narudia tena, kama miradi ndio inayotoa kura, leo hii bado weupe huko Afrika wangekuwa madarakani. Hivi wanavyofanya ccm leo, huko Afrika kusini walifanya miaka mingi sana, tena mara mia yake.
tindo hata SA kuna watu wanakalia nyumba za mabati full suti na ANC inawajengea nyumba. Hata huko Usa barabara zinaharibika na kujengwa.
 
Rea mpaka 72% vijiji vina umeme, Sgr Dar to Moro imebaki kidogo sana mvua na milima inasumbua. Ndege nane zimeshanunuliwa. Ubungo interchange imekamilika 98%. Mimi nipo Nccr Mageuzi lakini kweli nitasema, Jama amepiga kazi.

Mkuu hizo ni taarifa za kipropaganda. Vyama dola hutumia mbinu hiyo kwa kuwapa 'matumaini hewa' kwani wanafahamu wananchi wanatamani sana kuona umeme usiokatika, treni ya umeme, bwawa la Stiegler Gorge linakamilika kwa kasi na miradi mingine mikubwa. Halafu lawama wanazipeleka kwa maruhani-mabeberu wa kusadikika kuwa ndiyo wanakwamisha juhudi za CCM Mpya.

Hivyo CCM Mpya inacheza 'mind games' kwa kuwahadaa na kuwapa matumaini hewa wananchi wanyonge kuwa kila kitu kinaenda sawa na ndani ya miezi michache itakamilika.

Mother Nature / (Mungu si Athumani) imeikwamisha vitu vingi ambavyo CCM ingejipiga kifua imekamilisha kabla ya uchaguzi October 2020. Mapungufu ni uwezo mdogo wa Politburo ya CCM Mpya kuchagua lipi ni kipaumbele cha nchi na wananchi, ubabe bila kushirikisha umma mpana nje ya CCM Mpya, ukweli Tanzania ni nchi masikini hivyo mbuzi hula nyasi kufuatana na urefu wa kamba yake, CCM Mpya kujali Maendeleo ya Vitu na kusahau kuya balance na Maendeleo ya Watu yaani mapungufu ya kiutaalamu na uwezo wa kusimamia miradi ni mkubwa ndani ya serikali inayoburuzwa ya CCM Mpya.

Read more :
Journals : Psychological Review, Political Psychology review
 
Back
Top Bottom