Kwanini wafanyabiashara hawakuficha sukari Ramadhani ya mwaka jana waje wafiche mwaka huu wa uchaguzi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,873
141,805
Binafsi siamini kama mwezi huu wa Ramadan ndio sababu ya sukari kuhadimika madukani au kufichwa kama inavyodaiwa.

Zimepita Ramadan nyingi tu hatujaona sukari ikiadimika kwanini iwe mwaka huu. Ilifika wakati Bara ilizuia sukari kutoka Zanzibar kwa sababu bara ilikuwa na Supply kubwa ya sukari..... na siyo zamani ni juzi tu.

Inawezekana kabisa Ramadan ikapita na uhaba wa sugar ukaendelea hivyo ni bora waziri wa Biashara mh Bashungwa akatueleza shida hasa ni nini?!

Maendeleo hayana vyama!
 
Shida ni uamuzi wa serikali (unayoisifia sana hapa ukumbini) kuamua kuweka bei elekezi ambayo realistic. Hakuna mfanyabiashara mwenye akili timamu atakaekubali kuuza kilo moja ya sukari kwa Shilingi 2,400 wakati yeye kainunua Shilingi 2,800.
 
Kuna tetesi kuwa viwanda vya ndani vimesimamisha production kupisha corona, lazima upungufu uwepo kama ni kweli.
 
Kuna Mheshimiwa mmoja alisema TUPUNGUZE MATUMIZI YA SUKARI KWA SABABU SIO NZURI KIAFYA
 
Mwaka 2016/17 ilikuwa hivi kelele nyingi,mbwembwe nyingi....eti Bei elekezi 1800/ mpaka leo haikutekelezwa na sukar ikspaa ,na ndicho kinachoenda kutokea Sasa! Kama ilivotokea kwenye biashara ya korosho!

Kwa Hali ilivyo sasa Watanzania tuombe Mungu usitokee ukame ili mahindi,Mchele,maharage viendelee kuwepo.Kinyume chake Hali itakuwa mbaya sanaaa!
 
Ramadhani sukari huwa inasumbua sana, hata mwaka jana watu walikuwa na kero ya kupanda kwa bei ya sukari
 
Back
Top Bottom