Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Ukilinganisha na uchaguzi wa kwanza nchi yetu ikiwa inafuata mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 chama cha upinzani kikubwa wakati huo kilileta upinzani na hata CCM iliogopa maana Nccr mageuzi ilikuwa almanusra wachukue nchi.
Ukaja uchaguzi wa mwaka 2000 CCM walijipanga kivingine hivyo walishinda bila kuwa na misukosuko kama ya mwaka 1995. Maana hata Nccr Mageuzi ilikuwa imeshatetereka.
Na hii ni baada ya CCM kujaribu kurekebisha makosa yake na kutekeleza ilani yake vizuri. Maana hiki ndicho kipindi hata miundo mbinu mingi ilianza kujengwa, mfano barabara ya kuelekea kusini na daraja la mkapa ambalo lilikuwa kwa wananchi kabla ya kujengwa kero.
Na hiki ndio kipindi aliyekuwa waziri wa Ujenzi wakati huo maarufu kama askari wa mwamvuli alidiriki kusema, watu watapanda taxii toka mtwara mpaka Bukoba mkoani kagera.Kwa hiyo CCM ilijrekebisha hadi baadhi ya nchi wahisani walidiriki kufuta madeni ya nchi yetu maana hata uwazi na ukweli katika matumizi ya pesa ya umma ulibadilika tofauti na awamu iliyopita.
Uchaguzi wa 2005 CCM iligawanyika tena sana. Na wajanja wachache wakatengeneza mtandao na mgombea wao akachukua nchi.Na hawakupata upinzani mkali sana.
Uchaguzi wa wa 2010 ulikuwa mgumu kiasi kwa CCM maana sio siri watu walifanya ufisadi mbaya sana. Nchi ilikuwa kama ya kundi fulani ambao wao ni kujichotea pesa tu. Maana stori zilikuwa ni Epa,Escrow n.k
Uchaguzi wa 2015 ulikuwa na ugumu kiduchu kwa CCM maana ilikuwa imechafuliwa na watu wabaya. Na hapo ndipo busara ikatumika ili kumuweka mgombea ambae ni msafi, hata fomu alichukua kimya kimya na hata kuzunguka kwenda kutafuta wadhamini mikoani alienda kimya kimya.
Kwa uzalendo wake alionao alipochaguliwa tu akaanza kudhibiti ubadhirifu na ufisadi,akaanza kujenga Zahanati,vituo vya afya,madaraja na miradi kama Sgr na JNHHP. Na kwa mantiki hiyo akawa ameua kabisa nguvu za upinzani.
Maana wao ili wapate umaarufu ni kuibua ufisadi tu,sasa hizo habari hazipo.
Uchaguzi wa mwaka huu 2020 kwa ngazi ya urais JPM anakwenda kushinda kwa 100%/ ni kama tembo anakanyaga sisimizi.