TCRA: Hatujakataza matumizi ya VPN bali ni kusajili na kutoa taarifa ya matumizi ya VPN

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
62e2dd02-1c0e-4a2a-b37b-8b3922e131d6.jpeg


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kwa Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Rolf Kibaja imesema taarifa kwa Umma iliyotolewa juzi October 13,2023 haijakataza matumizi ya VPN kama baadhi ya Watu wanayopotosha kupitia mitandao ya kijamii.

Kibaja ameiambia Ayo TV kwamba
TCRA imetoa utaratibu kwa Watumiaji
wa VPN kutoa taarifa za matumizi ya VPN lakini haijazuia matumizi ya VPN.

"Watu wanaoshiriki kutoa taarifa kuhusu VPN wataendelea na shughuli zao kama kawaida kupitia VPN"

Kibaja amesema "Ni muhimu kwa Watumiaji wa VPN kutoa taarifa kwakuwa kusajili huduma ya VPN ni kama kujisajili kwa namba ya simu, Nchi nyingi zilizoendelea duniani zimechukua hatua kama hizi kuimarisha usalama mtandaoni, kama vile Uturuki, India, Belarus, Misri, China, na nchi nyingine"

"Ni muhimu kufahamu kuwa matumizi ya VPN nchini hayakatazwi bali yanapewa utaratibu rasmi, kutoa taarifa hizo hakuna gharama yoyote ya malipo na hakuingilli masuala ya faragha wala usalama wa watumiaji husika.”

“TCRA inaendelea kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama katika mtandao sambamba na Watumiaji wa mtandao kuendelea kuwa salama"
 
Kibaja amesema "Ni muhimu kwa Watumiaji wa VPN kutoa taarifa kwakuwa kusajili huduma ya VPN ni kama kujisajili kwa namba ya simu, Nchi nyingi zilizoendelea duniani zimechukua hatua kama hizi kuimarisha usalama mtandaoni, kama vile Uturuki, India, Belarus, Misri, China, na nchi nyingine"
Kwahiyo bila nchi hizo kufanya hivyo kwa akili yetu tusingekuja na wazo hilo?
 
Hebu achaneni na haya mambo madogomadogo,anzeni kuwa siriasi na issue za yenye tija jamani,unaposema nchi zilizoendelea please hapo hakuna hata moja,na si lazima muige, Holland ilijiepusha na mlundikano wa wafungwa magerezani kwa kuachana na mambo madogomadogo kama haya,nchi hii hatujui ka tunasonga mbele au tunarudi,kweli tanzania hapa ilipo turudi nyuma tuanze kiongelea vpn kweli?

Why kama kujifunza msijifunze kwa nchi ya kenya hapo ambayo iko karibu,maana kila kukicha Tanzania kazi kuigaiga tu,nakumbuka kenya walipokaza watoto kukaa boarding,siku chache mbele tukaiga,sasa wanafunzi ,wafanyakazi wafanya biashara,mapolisi ,walimu, wengine wapo vijijini huko,wafunge safari waje tcra,kweli jamani
 
Back
Top Bottom