TCRA hili la VPN nalo litawashinda kwa sababu hamtaki kuukabili uhalisia wa mambo

Nobunaga

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,169
4,986
Swali kwa TCRA: Mnajua sababu ya matumizi ya VPN kuwa makubwa nchini?

Uhalisia ulivyo: Kwenye teknolojia ukiwabinya sana wananchi pale, wao wanatokea kule kwa sababu ya kukua kwa teknolojia kila siku, kila kitu kina option B.

Katika mambo ambayo serikali ilikuwa haijawahi kuwaza basi ni kuibuka kwa matumizi makubwa ya VPN. It was not anticipated at all.

Wao walidhani wakifungia mitandao ya kijamii kipindi cha uchaguzi hasa 2020 basi watu hawatajua pa kutokea. Hilo lilikuwa kosa kubwa ambalo serikali watalijutia mpaka keshokutwa. Hapo ndipo VPN ilipotambulishwa rasmi kwa watanzania wanaotumia internet.

Walidhani wakizifungia sites za PILAU, basi viewers watapungua ama hawatokuwepo kabisa. Hilo likawa kosa la pili kubwa. Watumiaji wa VPN wakaongezeka mara dufu.

Walidhani wakibinya mabando ya internet, basi watapunguza kasi ya engagement ya watu mitandaoni. Hilo likawa kubwa la 3. Watu wakaja na matumizi ya internet ya bure kupitia hizihizi VPN.

Kiufupi VPN imekuja kuwa na matumizi mengi tofauti na yale tuliyoyajua. Watu wameenjoy sana internet ya bure na yenye kasi kwa kutumia V2Ray(Aina ya VPN) mpaka juzi juzi tuu TTCL waliposhituka kuifungia.

Haya yote yanasababishwa na wao wao TCRA kuja na miongozo ambayo haiko applicable kabisa kabisa katika dunia hii ya utandawazi na teknolojia ya juu kabisa.

Kwa sasa ukifanya research, kati ya watumiaji 10 wa internet basi 8 hawakosi kuwa na applications za VPN kwenye simu zao. Swali ni je, hawa TCRA watawakamata mamilioni ya watu kisa tu wanatumia VPN?

Katika dunia ya sasa ambayo teknolojia inakua kwa kasi, mara nyingi wananchi ndiyo wako mbele ya teknolojia kushinda serikali zao hasa katika nchi za Afrika. Serikali zetu zina lag behind sana. Ndiyo maana chombo kikubwa kama TCRA hakikuweza kupiga projections za mbele kwamba wakibania internet nini kitatokea, what are the possibilities?

Mfano hai ni ujio wa Starlink ya Elon Musk. Serikali badala ya kuwapokea kwa mikono miwili ili iwe mbele kuliko wananchi, wao wakaamua kuipiga pini kwa sababu zisizo na mashiko. Lakini mwisho wa siku watu mtaani wanatumia Starlink kama kawaida. Simu mpya zitakazotoka kuanzia mwakani zitakuwa na satelite connectivity, hivyo Elon hatahitaji kuleta madishi tena ili kuipata huduma yake.

Sasa swali kwa TCRA: Mnajua kitakachofuata endapo mtazuia matumizi ya VPN?
 
sawa twasubiri huku tukilalamika
 
Back
Top Bottom