TCRA sasa kutangaza masafa ya redio kwa zabuni

Jun 20, 2023
54
51
MAMALAKA ya mawasiliano nchini(TCRA)imetangaza kuwa kuanzia sasa masafa ya radio yatashindaniwa kwa kutangazwa zabuni huku wadau wakitaka kuwepo na uwazi ili kuwa na uwanja sawa.

Kwenye kikao cha wamiliki na maneja wa vituo vya radio pamoja na waandishi wa habari kilichokaa hivi karibuni mjini moshi,meneja wa kanda wa TCRA Mhandisi Imelda Salum,amesema mamlaka hiyo itatangaza masafa hayo mara mbili kwa mwaka.

Akawataka pia wamiliki wa vituo vya radio kujikita pembezoni mwa miji ambako masafa yanapatiakana tofauti na sasa ambako waombaji wengi wa masafa ya radio wanajikitia kwenye miji mikuu ya mikoa ambako masfa hayapatikani kwa sasa kutokana na wingi wa vituo vya radio.

"Masafa ni sawa na raslimali ina ukomo na masafa yakiisha yameisha tu huwezi kupata mengine na kwa kutambua changamoto hiyo TCRA kwa sasa tutatangaza zabuni kwa ajili ya masafa hasa kwenye maeneo ambako masafa yanapatikana",alisema.

Amesema wamiliki wengi wa vituo vya radio hawapendelei sana maeneo ya pembezoni hasa wale ambao wanajiendesha kibiashara na kutoa wito kwa wmiliki hao kuchangamkia fursa kwenye maeneo ambako masafa yanapatikana hasa waombaji wapya na wale ambao wanahitaji kupanua huduma zao.
Kwa upande wao

Baadhi ya wamiliki wa vituo vya radio walisema katika kikao hicho kuwa suala la zabuni linaumiza wengi kwa kile walichodai baadhi ya weye fedha wasiokuwa na uhitaji mkubwa wa masafa wanaweza kutumia uwezo wao wa kifedha kuwashawishi watoa zabuni kuhodhi masafa huku wenye uhitaji mkubwa na wsiokuwa na uwezo kifedha wakikosa masafa.

"Kwa hili tunaomba TCRA mliangalie kwa jicho la tatu ili washindani wote wawe sawa kama kwenye masumbwi ambako mabondia hupimwa uzito kabla ya pambana ili kuwa na uzito sawa ulingoni",alisema mdau mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
 
Back
Top Bottom