TCRA angalieni Airtel wanavyowaibia wateja

Gagnija

Platinum Member
Apr 28, 2006
11,849
10,433
Leo nimepiga simu airtel huduma kwa wateja kupitia namba 100 kama wenyewe wanavyoelekeza. Ajabu hadi dakika 10 zinakwisha, sijaunganishwa na mtoa huduma, napewa tu maelekezo, bonyeza 1, mara bonyeza 6.

Baada ya maelekezo hayo, napata sms kuwa nimetumia dakika 10, na kweli dakika 10 hizo wamekata kwenye muda wangu wa maongezi pasipo kunipatia huduma yoyote.

Hii ni kuwaibia wateja; TCRA shughulikieni huu wizi.
 
Back
Top Bottom