Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona- Zitto

#COVID19TZA Serikali imethibitisha uwepo wa virusi vya Korona Tanzania. Utulivu ni muhimu kwani kukiwa na maandalizi ya kutosha tunaweza kukabili madhara ya mlipuko huu. Nashauri mambo 3 muhimu sana, kwa maoni yangu.

- Tunaona Nchi nyengine kukiwa na ‘panic’ ya chakula. Watu wetu ni fukara sana, bei za chakula zitapanda na wengi hawatamudu.

Pia Serikali haina Akiba ya kutosha ya chakula kwenye ghala la Taifa. Kuna nafaka ya kutosha Siku 3 tu kwa kila Mtanzania. Ni vema Serikali kufanya uamuzi wa haraka kununua chakula ili kukigawa maeneo itakapohitajika.

- Tanzania inategemea Sekta ya Utalii kwa kiasi kikubwa katika Mapato ya Fedha za kigeni na ajira kwa raia wake. Mlipuko huu unaathiri sana sekta hii ambayo inaingizia Taifa wastani wa Dola za Marekani 2.5 bilioni kwa Mwaka sawa na 25% ya Mapato yote ya Fedha za kigeni yanayoingia nchini.

Naishauri Serikali kukutana na Wafanyabiashara wote kwenye sekta ya Utalii na Vyama vya Wafanyakazi kwenye sekta hiyo kwa lengo la kupata tathmini ya Pamoja ya madhara ya mlipuko huu kwa sekta ya Utalii na huduma zake.

Serikali itazame namna ya kuwafidia ( stimulus package) wafanyabiashara Katika sekta hiyo ili kulinda ajira za Wananchi. Ikiwezekana fidia iwe ni kulinda ajira kwa kufidia gharama za wafanyakazi ( payroll costs).

- Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona kwa Uchumi wa Tanzania kwa ujumla na Bunge lijadili Kwa maslahi ya Taifa ili kutoa mapendekezo ya kibajeti kuhami Uchumi wa Nchi yetu na haswa kulinda biashara ndogo, Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini kama Utalii, huduma za vyakula, usafirishaji na uchuuzi.

Zitto Kabwe, MP
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
17/3/2020
 
Umeegemea katika taaluma yako ya Uchumi, Naona umesahau jambo moja la muhimu zaidi, elimu zaidi kuhusiana na virusi hivi, Watanzania wengi wanafanya mzaha kuhusiana na hili.

Leo nilienda Mlimani City kwa shughuli zangu binafsi, niliyoyaona yamenisikitisha sana. Watu wamejawa na ulimbukeni wa ajabu, wanavaa zile mask kama fashion huku wakiwa hawazingatii tahadhari nyingine.

Nikiwa nyumbani kwangu namsikia jirani anamwambia mwanae kuwa ili kujikinga na Corona anatakiwa kunawa kwa maji moto na sabuni kila atokapo chooni!
 
Nawaza tu kama tuna akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kusaidia nchi endapo janga hili litakuwa endelevu huku uchumi wa dunia ukiendelea kuyumba.

Hata hali hii ya kushindwa kuzuia ndege kuingia nchini,kufunga mipaka,n.k, bila shaka ni matokeo ya hofu ya serikali kukosa mapato na hali hii inaathiri nchi nyingi sana za kiafrika na ndio maana zinashindwa kuchukua hatua kama ilivyo kwa nchi za Ulaya na Marekani zenye uchumi imara.

Wakati nchi za Ulaya na Marekani wanazuia ndege kuingia katika nchi zao pamoja na kufunga mipaka huku baadhi yao wakikiri walichelewa kuchukua hatua kama hizo,Afrika, sio kama tunashindwa ku-take advantage na kujifunza,bali umasikini ndio unaotufanya tunasita kuchukua kama zinazochukuliwa na mataifa hayo yenye uchumi mkubwa.

Swala la hii serikali kutoa stimulus package sio rahisi labda kwakuwa huu ni mwaka wa uchagu.

Usisahau serikali haijaleta coronavirus!!!
 
Hapo kwenye "stimulus package" nimemuelewa vizuri Zitto.

Kuna hoteli za kitalii zimeshaanza kufungwa kwa kukosa wateja, hivyo wafanyakazi kupewa likizo ya bila malipo.

Hii serikali kama inavyojinasibu kila siku ni ya wanyonge, naona hapa ndio pazuri pa kuanzia kuthibitisha kwa vitendo, na zaidi tunaaminishwa kila siku sisi ni "donor country", basi tuanze practical kwa watanzania wenzetu walioathirika na hili janga la Corona kiuchumi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Machalii wa huko kwny utalii wakiambiwaga oyaa mjitahidi ku save pesa kidogo hua wanajibu kwani mlima k’njaro umehamishwa au umekwisha? So long mlima upo hela ipo tu.

Ngoja tujionee wazungu wakiacha kuja hali itakuaje wkt mlima uko vile vile tu.
 
Sijui serikali itanunua chakula na kugawa kwa muda gani maana hatujui janga litaisha lini. Hali kadhalika sijui iitawafidia wafanyabiashara na kulinda ajira za wafanyakazi sekta ya utalii kwa muda gani. Je, ugonjwa ukiwa endelevu kwa mwaka mmoja aù miaka kadhaa?

Nawaza sipati jibu. Na hizo sanitiza tutanawa mpaka lini sijui. Naona tunautazama huu ugonjwa kwa namna ya mlipuko wa muda mfupi, na ninaombea iwe hivyo. Ukituganda kwa muda mrefu sijui hali itakuwaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri wako umeegemea kubagua sekta nyingine.

Unadhani corona imeathiri utalii tu!

Vipi kuhusu wafanyabiashara tunaotegemea ku-import mzigo toka China?

Hili janga limeathiri sekta mbalimbali hivyo kusema serikali iwafidie waajiriwa wa sekta ya utalii ni sawa na kuweka tabaka ili badae wapinga juhudi mje kukosoa, si tunawajua bhana au unazan uongo mh?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom