Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,818
- 4,569
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeonyesha taasisi za Serikali zinadaiwa mikopo ya muda mrefu yenye thamani ya Sh1.73 trilioni ambazo hazijalipwa kuanzia mwaka mmoja hadi 16.
Kwa mujibu wa kitabu cha Ripoti ya CAG ya Mashirika ya Umma, ambacho ni miongoni mwa ripoti 21 zilizowasilishwa leo Jumatatu, Aprili 15, 2024 bungeni jijini Dodoma, fedha hizo zilichukuliwa kwa nyakati tofauti kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta binafsi, na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma.
CAG amesema hali hiyo imesababisha kupunguza uwezo wa mifuko ya jamii kufanya uwekezaji zaidi.
“Pia, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta binafsi (NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) haikukusanya michango ipatayo Sh856.78 bilioni kutoka kwa wanachama, hivyo kudhoofisha uwezo wa mifuko kuhudumia wanufaika.”
“Vilevile, nilibaini Shirika la Bima la Taifa, NSSF na PSSSF hawakukusanya kodi ya Sh47.20 bilioni kutoka kwa wapangaji katika vitega uchumi vyao,” amesema Kichere.
PIA SOMA:
- Ripoti 21 za CAG zatua Bungeni kwaajili ya kuanza kujadiliwa