Rais Samia Atoa Bil 2.4 Malipo ya Wafanyakazi wa Urafiki

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,506
3,056
CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), kimeipongeza Serikali kwa kutoa sh. bilioni 2.4 za malipo ya wanachama wao waliokuwa wanafanya kazi katika Kiwanda cha Nguo Urafiki ambapo madai yao yamedumu kwa kipindi cha miaka 10.

Mball na serkali kutoa fedha hizo, TUICO imeanza rasmi kuhakiki majina ya wanachama hao ili kuanza kuwaingizia fedha walizokuwa wakizidai. Madai hayo yanahusisha posho za kodi ya nyumba, usafiri na chakula yaliyoanza mwaka 2008 hadi 2013.

Akizungumza na wanahabari kuhusu uhakiki wa majina ya wanachama wanaostahili kulipea Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TUICO, Boniphace Nkakatisi, alisema chama chao kimepata mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sekta kuu nne.

Sekta hizo ni Sekta ya Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha na TUICO kama taasisi iliyosajiliwa na Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Tanzania, walishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao, kufanikisha malipo hayo

"Tunaishukuru Serikali kwa ushirikiano wa kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya shughuli zetu za chama na jitihada zinazoonekana waziwazi kuhakikisha wafanyakazi wanaostahili wanakupata haki zao kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sheria ya Utumishi wa Umma na nyingine mbalimbali.

"Tunayo furaha kubwa kwa chama kumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Nguo
Urafiki dhidi ya mwajiri wao na Serikali. Machi 24, 2023, chama kilifanikiwa kusaini mkataba wa kumaliza mgogoro uliokuwa mbele ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kuhusu ukazaji deni, tuzo namba. 164/2021 uliotokana na mgogoro wa marejeo namba 58/2019," alisema.

Alisema serikali imeweza kutekeleza kwa vitendo, kulipa madeni ya madai ya wafanyakazi, kuheshimu maamuzi ya
Mahakama baada ya wafanyakazi kushinda shauri hilo. Alieleza kuwa, chama kitaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa serikali, waajiri wote, vyama vya wafanyakazi na chama cha Waajiri ili haki, mikataba na maslahi ya wafanyakazi nchini iweze kuheshimika. Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa TUICO, Noel Nchimbi, alisema kuanzia Januari-Septemba,2023, chama hicho kimefanikiwa kushughulikia migogoro ya kazi 301 ikiwemo ya ana kwa ana. Awali walipokea migogoro 42, kufanikiwa kusuluhisha migogoro 41, unaondelea ni mgogoro mmoja, pia chama kilishughulikia migogoro ya ngazi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) baada ya kupokea migogoro 134.

Kati ya hiyo, wamefanikiwa kumaliza migogoro 60, inayoendelea katika hatua za usuluhishi ni 74. Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho aliyekuwa Idara ya Candisi, Majuto Honelo, alisema alianza kazi mwaka 1973-2012.

Aliishukuru TUICO kwa jitihada ya kusimamia kesi hiyo hadi kupata haki yao.
"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa jitihada ya kutulipa mafao yetu ambayo yamedumu tangu 2013 tuliposhinda kesi," alisema.
 
Mbona mnapenda kumsifia Mama kiasi hicho? ACHA UCHAWA

KWANI UNGESEMA SERIKALI IMETOA KIASI FULANI UNGEPUNGUKIWA NINI?

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Ni serekali si Samia Punguza uchawa.
 
Sema issue kama za viwanda serikali iachane nazo tu, iache pvt sector tupambane
 
Huyo Samia katoa hizo hela toka Kizimkazi?

Machawa bhana! Mko kila mahali.

Unaanzaje kuandika kuwa Samia atoa bilioni 2.4 kwa wafanyakazi? Hizo ni fedha zetu watanzania maana tunalipa Kodi na tozo

Huyo Samia hana chochote. Siku nyingine uandike hivi:- serikali yatoa bilioni .....kwa wafanyakazi
 
Back
Top Bottom