Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,621
- 46,266
Lengo la serikali la mfumuko wa bei wa 3% kwa wakati wote halina mashiko sana kwa sababu mfumo wa bei unatakiwa uendane na uhalisia wa hali ya ajira pamoja na hali ya rasilimali fedha na ardhi.
Lengo la mfumuko wa bei Marekani ambako asilimia kubwa ya raia wana ajira linakuwa tofauti kabisa na nchi ambapo asilimia kubwa ya raia hawana ajira au wana ajiri za kujishikiza na kufanya kazi masaa machache.
Kuweka lengo dogo la mfumuko wa bei ni kuzuia pia ukuaji wa ajira kwa sababu ya inakubidi uweke sera za kiasi kidogo cha mzunguko mdogo wa fedha katika uchumi.
Kutokana na miongozo ya BoT kuhusu kiwango cha mikopo chechefu Mabenki Tanzania yanakimbizana kupata wateja wa sekta zenye risks ndogo kama consumers loans kutoka kwa waajiriwa rasmi wa serikali na mashirika makubwa ya sekta binafsi kitu ambacho mchango wake katika kukuza uchumi ni mdogo. Benki zinatakiwa kutoa mikopo hata kwa biashara zinazoibukia.
Ni kama vile Tanzani hatuna benki za kibiashara(commercial banks) na badala yake tuna Benki za hifadhi zaidi(savings banks). Hii ni kwa jinsi ambavyo benki zinajikusanyia na kurundika mitaji kwa kiwango kikubwa wakati kuna sekta kubwa ya biashara yenye uhitaji wa mikopo lakini haikopeshwi kwa kuogopa risks.
Benki za serikali au zenye mitaji kutoka serikalini zijiongeze kusaidia kuibua biashara mpya na kuziwezesha biashara mpya za kiotofauti zinazoibuka (startups) kupata mikopo,kukua na kufanya vizuri kwa sababu ndio njia mojawapo muhuimu ya kuuchangamsha na kukuza uchumi badala ya kufanya mambo yale yale kama kugawa majiko.
Inashangaza na kutafakarisha tunasifiwa sana na taasisi mbalimbali uchumi wetu kukua kwa asilimia 5 ila hatukusifiwa ulipokuwa ukikua kwa asilimia 6 hadi 7 ambapo hata hautajifikia lengo lengo la asilimia 8 serikali ililojiwekea.